John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 131 to 140 of 2259.

  • 11 Jul 2024 in Senate: Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu kuhusu wachuuzi wa rejareja. Kwanza, nampongeza Sen. Esther Okenyuri kwa Mswada huu. Amewapa heshima na hadhi wachuuzi ambao kwa wakati mwingi wanaonekana kama watu wasiofaa ama biashara wanazofanya hazifai. Kwa kuwasilisha Mswada huu hapa Seneti, inaonyesha kwamba anawajali. Ukitazama Vifungu vya tatu na nne, Waziri anayehusika atapaswa kujua idadi ya wachuuzi katika Jamhuri ya Kenya. Baada ya kujua idadi, itamwezesha kuleta usawa katika sehemu zinazofanyiwa kazi; iwe kule Nyahururu, Nanyuki, au Nyaribari Chache. Wachuuzi wote wanapaswa kufanya uchuuzi katika mazingira sawa. Sio mara moja tumewapata wachuuzi wetu wakiishi ... view
  • 11 Jul 2024 in Senate: moja hadi nyingine ilhali wanalipa kodi. Naunga mkono kwamba watengewe sehemu za kufanyia biashara. Sehemu ambazo wanafanyia biashara ziwe na huduma zinazohitajika. Kuwe na vitu kama vile vyoo kwa sababu ni watu wanaofanya biashara zao kwa muda mrefu hadi usiku. Tumesema kwamba tunataka uchumi unaondeshwa masaa 24. Hilo litawezekana ikiwa wachuuzi hao watashughulikiwa. Sehemu kama hizo zinafaa kuwekwa taa. Kwa lugha ya mtaani, wanasema “mulika mwizi.” Staki kusema hivyo kwa sababu yatakuwa maendeleo. Tunafaa kuwa na taa za kumulika maendeleo. Si hayo tu. Ukitembea sehemu nyingi, utapata kuwa wachuuzi hawakutiliwa maanani na kaunti zetu. Kama alivyosema Sen. Ogola, kwa mfano, ... view
  • 11 Jul 2024 in Senate: Mswada huu ukipitishwa utatoa mwongozo vile sehemu ikitengwa, ni nini kinapaswa kuwekwa pale ili wachuuzi wetu wanufaike. Hii pia inatatua ule ushindani ulioko. Unapata mchuuzi anauza bidhaa zilizosawa pale nje kwa duka ya mfanyibiasha aliyepangisha nyumba. Si sawa kwa sababu huu ni ushindani usio mzuri. Kwa hivyo, kutengwa kwa sehemu hizi kutasaidia ili kila mtu apate riziki yake. Imesemwa na ningependa kurudia, hii kazi ya uchuuzi inafanywa na vijana na watu wasio na hela nyingi. Mara nyingi unasikia unapoenda kutafuta kazi yoyote unaulizwa kama uko na ujuzi au uzoefu. Hizi sehemu zikitengwa na mtu aanzie hii kazi ya rejareja pale ... view
  • 11 Jul 2024 in Senate: Jambo lingine ambalo Mswada utasaidia ni kuongezeka kwa ukusanyaji wa kodi na ushuru. Hii ni kwa sababu, wafanyikazi wa gatuzi zetu hawatawakimbiza ama kuwavuruga hawa wafanyibiashara ama kuwaona kama sio watu. Nimeona imesemekana wakubaliane ni pesa ngapi watakuwa wakitoa kwa sababu watakuwa wanafanya kazi kwa maeneo yanayofaa kisheria, hakutakuwa na haja ya kuwakimbiza. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate. view
  • 11 Jul 2024 in Senate: Kwa kuangazia, Mswada huu uliwasilishwa na Sen. Esther Okenyuri. Sisi kama Chama cha United Democratic Alliance ( UDA) ambacho Okenyuri ni mwanachama, tulipokuwa tunafanya uchaguzi, tulisema tutazingatia wale walioko chini kama vile mama mboga, watu wa boda boda na vinyozi. Hivyo basi, nampongeza kwa sababu Mswada huu umelenga papo ndipo kwa kuwashughulikia vilivyo. Kwa hivyo, mimi niko na kila sababu kuunga mkono Mswada huu. Ukitembelea sehemu nyingi za Laikipia na Nyahururu, shida kubwa wanayopata wachuuzi wetu ni ukosefu wa sehemu za kuuzia. view
  • 11 Jul 2024 in Senate: Nimekuwa nikiongea na Gavana na kumrai pengine tuwe tukifunga barabara siku ya Jumamosi na Jumapili ili wachuuzi wetu waje kuuza. Lakini Sen. Okenyuri ameng’amua na akajua tukileta Mswada huu, tutakuwa na sehemu zilizotengewa wachuuzi wetu. Itakuwa sasa ni rahisi kwa hawa wachuuzi wetu kufanya biashara bila kusumbuliwa na mtu yoyote. view
  • 11 Jul 2024 in Senate: Mahali nimekuwa na tashwishi kidogo na labda wakati atakapokuwa akijibu ataangazia, nilijiuliza, kwa nini anahusisha sana Waziri wa Serikali ya Kitaifa ilhali mambo ya biashara kama hizi yako katika gatuzi zetu. Anapaswa kupatia Waziri wa Ugatuzi kwa sababu nchi yetu ni tofauti na mambo hufanywa tofauti. Kama Serikali ya Kaunti ya Laikipia ni tofauti na ile ya Kisumu, kwa nini unamhusisha Waziri wa Serikali ya Kitaifa? view
  • 11 Jul 2024 in Senate: Sen. Esther, ukileta Mswada kama huu halafu uhusishe Waziri wa Serikali Kuu, huenda ikawa kama vile huduma ya Afya imeletwa katika gatuzi zetu lakini hela nyingi zinabaki kwa Serikali ya Kitaifa. Nataka tu usahihishe hiyo sehemu tusije tukaleta Mswada hapa halafu mambo mengi yanafanywa katika Serikali ya Kitaifa badala ya kugatuliwa. Mambo ya biashara kama hizi tayari yamegatuliwa. Hivyo basi, yashughulikiwe huko kwa hali inayofaa. view
  • 11 Jul 2024 in Senate: Mimi naunga mkono ili watu wetu wasaidike. Ukiangalia katika Kipengele cha 15, kinazungumzia vile hawa wachuuzi watapewa leseni na kusajiliwa. Hili ni jambo nzuri ili mipango yoyote inapopangwa, kuwe kunajulikana idadi ya wachuuzi na ni biashara gani wanafanya. Kama kuna mifereji ya maji inatakikana ijulikane ni mingapi. view
  • 11 Jul 2024 in Senate: Nashukuru kwa kipengele hiki na inaonekana Mswada huu umezingatia kila kitu. Kwa hivyo hakuna mahali palipo na dosari. Haya yote yakizingatiwa, Mswada huu utaleta afueni na kuwasaidia watu. Itakuwa ni moja ya nguzo ya chama chetu kulingana na ahadi tulizotoa. Sen. Okenyuri kwa kweli amegonga papo ndipo. Nampongeza kwa sababu alikuwa Waziri katika serikali ya kaunti. Kwa hivyo, yeye ana uzoefu na ujuzi mwingi. Nimesikia yale mambo aliyosema. Tukiyaongeza na kuyazingatia tutapata Mswada uliobora zaidi. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus