4 May 2021 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, napongeza Kamati ya Haki, Maswala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu ambapo Mwenyekiti wake ni Sen. Omogeni kwa kazi nzuri waliofanya kuchanganua mabadiliko ya kikatiba. Maswala ya kikatiba ni mambo muhimu ambayo tunapaswa kuangalia kwa mapana na marefu.
view
4 May 2021 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kabla sijajitosa katika hayo mabadiliko ya kisheria, ni vizuri ijulikane wazi kwamba jambo la dharura wakati huu ni maswala yanayowakumba Wakenya. Kuna ugongwa wa COVID-19 unaowasumbua Wakenya. Watu wengi wanasumbuliwa na ugonjwa huo. Kule India watu wengi wanaendelea kusononeka kutokana na ugongwa huo. Jambo ambalo tunafaa kuzingatia ni kuhakikisha kwamba Wakenya wetu wanajikinga kutokana na ugonjwa huo kwa kuwapa chanjo.
view
4 May 2021 in Senate:
Ugonjwa huo umeleta suitofahamu katika nchi yetu kwa sababu watu wanaendelea kufa. Wizara ya Afya ambayo inahusika inafaa kukubali Wakenya kutumia
view
4 May 2021 in Senate:
wakati watu ni wagonjwa kwa sababu watu hawalipiwi wanapopata ugonjwa huo. Hatufai kuwa tunaongelea marekebisho ya Katiba bali jinsi ya kusaidia watu wetu ambao wamekosa ajira kutokana na ugonjwa huo.
view
4 May 2021 in Senate:
Hata hivyo, kwa kuwa tunajadili marekebisho ya Katiba, nitayazungumzia moja kwa moja. Jambo la kwanza ni kuwa tutakuwa na uwiano – kwa Kiingereza wanasema
view
4 May 2021 in Senate:
– kwa sababu tutakuwa na Waziri Mkuu pamoja na wengine ambao wameongezwa.
view
4 May 2021 in Senate:
Nilisikia wenzangu wakisema yakwamba ukiongeza hao viongozi wakenya hawata pigana tena. Hilo si jambo la kweli kwa sababu hao ni watu ambao wanajitakia makuu wenyewe. Yale ambayo tungekubaliana ni kwamba mtu anafaa kukubali anaposhidwa. Mswahili anasema ya kwamba asiyekubali kushindwa sio mshindani. Hatuwezi tukasema ya kwamba tutakuwa na mawiyiano kwa sababu tutatengeneza nyadhifa nyingi. Hilo sio ukweli kwa sababu nchi zingine zina viongozi wengi lakini watu bado hupigana.
view
4 May 2021 in Senate:
Madam Deputy Speaker, I have heard my colleague, Sen. Linturi. He has asked for your guidance on when we will speak, yet we are paid to sit in this House.
view
4 May 2021 in Senate:
Katika kaunti zetu na maeneo bunge, watu hushindani wengi lakini huwa hawapigani. Kwa hivyo, kuongeza hizi viti vya waziri mkuu na manaibu wa waziri mkuu ni kuongeza ushuru kwa wakenya ambao wamegharimikia makubwa na wameathirika na ugonjwa wa Covid-19 . Wakenya wengi wamepoteza kazi na wamefunga biashara zao, haswa wale ambao hufanya biashara usiku. Sioni haja ya kuongeza viti hivyo.
view
4 May 2021 in Senate:
Tumekuwa tukiambiwa ya kwamba pesa zinazoenda katika kaunti zetu zitaongezeka kutoka asilimia 15 hadi asilimia 35. Tulikuwa hapa tukijadili mswada wa ‘ one man, one vote, one shilling .’ Tulikuwa na Sen. Cherargei, Sen. Kihika, Sen. Loitiptip na Sen. Wetangula. Tulijadili kwa urefu na upana ila ulikuwa kizungumkuti. Ulikuwa ni nguo kuchanika. Sisi tilikaa hapa na kuzungumza bali ilimchukua rais mwenyewe kuongeza zaidi ya Kshs50 billioni. Kwa nini alifanya vile na haikuwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view