John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1831 to 1840 of 2259.

  • 23 Sep 2020 in Senate: As I speak, we should take care of locals. The money used to market our country so much in other countries should be used in marketing our sceneries to the locals. We want to encourage them to be visiting those areas. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Asante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza nakemea taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Magavana. Hana uwezo wowote kufunga zahanati au hospitali katika kaunti yoyote ya nchi hii yetu ya Kenya. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Nina hofu kidogo kuongea kuhusu yule Mwenyekiti, kwa sababu itakuwa kana kwamba ninajitosa katika zizi kupigana mieleka na nguruwe. Nitakuwa na uwoga kidogo kwa sababu yeye mwenyewe amejitosa katika ulingo ambao hana uzoefu, kujua ya kwamba hana sheria na uwezo wowote kisheria kusema kwamba kaunti yoyote inapaswa kufungwa ama huduma yoyote kwa mwananchi yeyote katika kaunti zetu za Kenya inapaswa kufungwa. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Ninamhakikishia ya kwamba pale Laikipia na nimwambie Gavana wangu, mheshimiwa Nderitu kwamba kuanzia Nanyuki, Nyahururu na Rumuruti, mtu yeyote atakayekuwa mgonjwa ama mja mzito anapaswa kwenda katika hospitali bila kusikiliza maagizo yoyote ya mtu yeyote. Sisi tulimchagua Gavana Nderitu. Hatumjui gavana mwingine hata iwe Gavana Oparanya. Hicho ni kikundi tu kilichokutana hapa Nairobi au mahali pengine na kuchaguana. Sisi watu wa Laikipia maagizo ambayo tutafuata ni yale yaliyomo katika Katiba ya Kenya. Gavana Oparanya hana uwezo. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Wakenya wote waendelee na shughuli zao, kwa sababu sisi kama Seneti--- Ninawahakikishia kwamba kesho tutakubaliana na tupitishe pesa ambazo zitakuwa zikienda kaunti. Hata kabla hatujapitisha, ijulikane wazi ya kwamba Mahakama Kuu Ya Kenya ilisema kwamba wanapaswa kuwa wakipewa asilimia hamsini ya pesa ambazo tulikuwa tumekubaliana. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Hakuna haja yoyote yake kuleta kizuizi chochote watu kupewa huduma. Rais wa Jamhuri ya Kenya jana alisema ataongeza zaidi ya Kshs50 bilioni na huyo mungwana alikuwa ameketi pale. Sasa anasema ati zahanati na hospitali zetu zitafungwa. Alisikia wapi? Sijui hayo maneno yameweza kumsumbua. Tunamwambia kwamba hospitali zetu zitaendelea. Kwa kusema kuwa hospitali zitafungwa, je, alisikia wapi? Kusema eti huduma zitafungwa katika kaunti zetu, je, alisikia wapi? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Adhubutu tumwonyeshe cha mtema kuni. Kama vile Sen. Mutula Kilonzo Jnr., amesema, gavana yeyote atakayejaribu kufunga zahanati, hospitali ama huduma zozote katika kaunti zetu tutamwonyesha cha mtema kuni. Watakuja hapa Seneti na tutawashughulikia vilivyo. view
  • 16 Sep 2020 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda. view
  • 15 Sep 2020 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I rise to support the amendment by Sen. (Dr.) Ali. We have a lot of work pending before the Senate. The COVID-19 curve is flattening, therefore, I believe that if we sit three times a week, we are going to achieve more progress than what we are able to do by sitting once a week. view
  • 15 Sep 2020 in Senate: Many Kenyans are complaining that we have taken too long to come up with a third basis for revenue allocation among the counties. We have taken so long in coming up with a formula because we only meet once a week. If we had sittings three times a week, we would have taken a shorter time in coming up with a third basis for revenue sharing. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus