John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1811 to 1820 of 2259.

  • 11 Nov 2020 in Senate: Madam Temporary Speaker, I am rising because I already keyed in. I wanted to talk just before that Motion. However, you did that deliberately to gag me. Even if we lost on that Motion¸ we did not lose genuinely. view
  • 10 Nov 2020 in Senate: Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia kwa Taarifa ya Sen. Were. Nataka kuchangia kuhusu utawala wa Safaricom ambao unaonekana umekuwa mkubwa katika uchumi wetu wa nchi. Kwanza, tujiulize ni kwa nini wanaongoza katika hiyo idara. Hii ni kwa sababu, huduma zao ni za kufaa na katika ule ushindani ulioko, wameegeza hela nyingi katika biashara yao ukilinganisha na wengine katika sekta hiyo. Pengine wale wanaochelewa kidogo hujipata taabani na hawawezi kushindana na kampuni hiyo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from ... view
  • 10 Nov 2020 in Senate: Jambo la kuvunja moyo ni kwamba, huwezi kujua kama maajenti wa Safaricom ni watu wanaohusika sana na mambo ya pesa. Sijui niseme kwamba wanafanya vizuri ama vibaya kwa sababu ukitembea sehemu zote za nchi, utapata maajenti wa Mpesa wako kila mahali. Uzuri ni kuwa, mtu akiwa mgonjwa anaweza kupata pesa kwa haraka. Pia wameleta mambo mengine mapya. Kuna mikopo kutumia simu kama vile Fuliza . Jambo la muhimu ni kuwaambia kuwa kama wanashughulika na mambo ya pesa-- - view
  • 8 Oct 2020 in Senate: Bw. Spika, Nashukuru kwa kunipa fursa hii niulize tu kwa hoja ya nidhamu hata ijapokuwa amemaliza. Nilitaka kujua, Kamati ile ina Maseneta wengi lakini inaonekana ya kwamba yeye anafuatilia vizuri ile gender rule. Nimesikia ya kwamba ni Sen. Farhiya na Sen. Omanga ambao wanafuatilia muda vizuri. Kwa hivyo, inaonekana ya kwamba wale wengine wamezembea katika kazi yao, na ndio tulikuwa na jukumu kubwa kupitisha hii formula--- view
  • 8 Oct 2020 in Senate: Hoja yangu ni kusema ya kwamba pengine sababu yetu kuwa na shida kubwa kupitisha Mswada huu ni kwa sababu wengine wamezembea katika kazi yao. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Ningependa kuchangia Taarifa ambayo imeletwa na Seneta wa Bomet. Inaonekana kwamba miradi mingi anaanzishwa pasi kumalizwa katika nchi yetu ya Kenya. Ni kama hakuna haja ya kuwa na miradi mingine. Si barabara na daraja pekee. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Kule Laikipia, kuna barabara ya kutoka Naromoru kupitia Kihato, kuelekea Makutano. Hakuna kazi inayofanyika kwa barabara hiyo ambayo imekuwa ikijengwa kwa muda mrefu. Ukiuliza utaambiwa kuwa aliyepewa kandarasi alilipwa ilhali hakuna kazi inayoendelea. Wengine wanafanya kazi kiholela. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Kamati itakayopewa jukumu hili inafaa kuangalia swala hili kwa mapana na marefu. Waziri wa Barabara na Miundomsingi anafaa kuitwa hapa ili atuelezee kinachoendelea kwa sababu mambo ya barabara na daraja yamekuwa kizungumkuti. Daraja zinajengwa na kusombwa na mafuriko wakati wa mvua. view
  • 7 Oct 2020 in Senate: Barabara na mabwawa si mkate ambao mtu anaweza kula kisha aweke karatasi kwa mfuko. Inapaswa maneno haya yaangaliwe vizuri. Barabara na hata mabwawa ya maji yakianza kujengwa, inafaa watu wajue muda yatakayochukua. Wanaopewa kandarasi hawafai kutoweka baada ya kulipwa. view
  • 6 Oct 2020 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I would hate to interrupt Sen. Cheruiyot. I am not getting him because he said resources have been taken to certain parts of this country. Maybe he would have elaborated because I do not know which parts of this country he is talking about. If he would mention which parts of this country he is talking about, I would be happy to try and persuade and use the same language to get the resources to come to Laikipia County. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus