John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1921 to 1930 of 2259.

  • 19 Feb 2020 in Senate: Bw. Spika, nimemsikia mwenzangu Seneta wa Kaunti ya Makueni akisema alimwona Mchina akiwa amejifunga kinywa. Akasema ilionekana kana kwamba ana ugonjwa huu wa Corona . Je, inamaanisha kwamba ukijifunga kinywa ama ukitoka China una ugonjwa wa Corona ? view
  • 19 Feb 2020 in Senate: Bw. Spika, asante sana kwa kunipa fursa hii. Nawapongeza Sen. Kwamboka na Sen. Kasanga kwa kuleta Taarifa hii. Linalonivunja moyo ni kwamba tunazungumzia Virusi vya Corona kwa uchungu mwingi na bado haijafika nchini. Sijui Serikali yetu ya Kenya imejitayarisha vipi kupambana na Virusi vya Corona . Seneta wa Kaunti ya Lamu alilalamika jana kuhusu hali ya zahanati katika kaunti yake. Ikiwa Virusi vya Corona vitafika katika nchi hii, nahofia Serikali yetu ya Kenya haitakuwa imejitayarisha vilivyo. Nzige wamevamia mashamba yetu na ulielekeza kwamba Waziri wa Kilimo, Mifugo and Uvuvi aje aangazie jambo hilo. Sina uhakika view
  • 19 Feb 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 19 Feb 2020 in Senate: kama Serikali yetu imejitayarisha kupambana na Virusi vya Corona na kwa hivyo haiwezi kuwaruhusu wanafunzi Wakenya anaohangaika Wuhan kurudi nchini. Labda Serikali inadhani ikiwaruhusu nchini huenda wanafunzi hao wakawaambukiza Wakenya Virusi vya Corona. Zahanati nchini Kenya hazina dawa. Kwa hivyo, Serikali itakuwa na jukumu kubwa kupambana na Virusi vya Corona iwapo itafika nchini Kenya. Hali katika sekta ya afya inadhoofika. Mimi ni mwana kamati katika--- view
  • 18 Feb 2020 in Senate: I have heard my Chairman saying “somebody somewhere”, maybe he could elaborate on that “somebody somewhere”. view
  • 10 Feb 2020 in Senate: Asante sana Bw. Spika. Naungana nawe pamoja na ndugu zangu Maseneta, kutoa risala zangu za rambirambi, za familia yangu pamoja na za Kaunti ya Laikipia kwa familia ya mwenda zake rais mpendwa wetu, hasa, kwa Seneta mwenzetu, Sen. Moi ambaye tumekuwa na yeye hapa. Naongea kwa niaba ya wengi ambao view
  • 10 Feb 2020 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 10 Feb 2020 in Senate: hawakuwa na ile fursa ya kukutana na yeye moja kwa moja. Tulikutana na yeye haswa katika idhaa ya Kiswahili ya Kenya Broadcasting Corporation (KBC). Nakumbuka nilianza kusikia taarifa za habari nikiwa katika shule ya chekechea na tukajua ya kwamba kila wakati taarifa zinaposomwa ni mpaka wahariri wakuu waanze na kueleze pale ambapo Rais wetu alipokuwa. Kwa hivyo, sisi tulimjua. Jina la Moi lilijiandika katika nyoyo zetu. Nakumbuka ya kwamba nikiwa mdogo, tulikuwa tukiuliza: “Na Moi wa Uganda anaitwa nani? Moi wa Tanzania anaitwa nani? Tulifikiria ya kwamba mtu yeyote ambaye ni rais anapaswa kuitwa Moi. Bw. Spika, ninamkumbuka Rais Moi ... view
  • 29 Jan 2020 in Senate: Asante Bw. Spika. Gavana mwenyewe alisema kuwa si bibi yake ama watoto wake. Itakuwa aje Seneta kutoka mbali ama upande ule mwengine anajua ni bibi yake? view
  • 29 Jan 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Sauti ninazosikia hapa zinasema “tumsulubishe Gavana Waititu”. Lakini, swali ninalojiuliza ni Hoja hii ilipofika hapa kama ilitumia njia inayofaa na viwango vinavyohitajika katika kaunti zetu? Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi, sheria zetu zinasema kinagaubaga na dhahiri ya kwamba kunapaswa kuwa na kiwango fulani ya Wabunge wa Kaunti. Lakini kama kulingana na wakili alivyouliza maswali, ikiwa kile kiwango hakikufikishwa, je, sisi kama Seneti tunapaswa kusikiza Hoja hii? Itakuwa jambo la kuvunja moyo wakati swala hili litapelekwa kortini. Sisi tutaulizwa kwa nini hatukufanya vile inapaswa kuwa. Ninauoga na ninatetemeka. Ni vizuri tufuate mfano mwema. ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus