12 Nov 2019 in Senate:
Asante sana Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ninataka kumpongeza Senata wa Mombasa, Sen. Faki, kwa taarifa yake nzuri. Mchezo wa kandanda unaweza kutumika na vijana wetu kama kitega uchumi. Lakini kitega uchumi hiki kimeanza kufuatiliwa na ufisadi. Itakuwaje uchaguzi katika Shrikisho la Kandanda utafanywa na vilabu 18, ilhali nchi yetu kuna vilabu vingi sana?
view
12 Nov 2019 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
12 Nov 2019 in Senate:
Katika kila kaunti kuna vijana ambao wanacheza, ilhali wao hawatahusishwa wakati kuna uchaguzi. Hii inaonyesha kwamba, kuna vibaraka ambao kazi yao ni baada ya pesa kupeanwa na Shirika la FIFA hawasikiki tena. Hawataki kujua vijana wetu watafaidikaje kwa michezo. Bw. Spika, Kamati ambayo imepewa jukumu kuhusu taarifa hii inafaa waangalie mambo haya kwa marefu na mapana. Wanafaaa wazingatie uchunguzi kuhusu ufisadi. Inafaa wajue kama ufisadi uko. Kama uko, waonyeshe wazi ni nani wafisadi ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. Tukifanya hivyo, tutasaidia mchezo wa kandanda na vijana wetu kwa sababu michezo ndiyo kitega uchumi ambacho kinaweza kusaidia aliyesoma na yule ...
view
6 Nov 2019 in Senate:
Asante sana Bw, Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono Taarifa hii ambayo imeitishwa na Sen. Wetangula, wa Kaunti ya Bungoma. Ni jambo la kuvunja moyo kuona walinda usalama wengi zaidi wamewekwa katika shule zetu. Wengi wao wamejihami vilivyo. Wakiwa wengi vile, wanaogofya wanafunzi, ilhali The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
6 Nov 2019 in Senate:
ukitembea sehemu zingine za nchi hii, wale wanafunzi hawajawahi kuwaona askari wetu wakiwa wamejihami jinsi walivyojihami sasa. Bw. Spika, hatusemi kwamba ni vibaya kwa askaris wetu kuwa katika shule zetu, kwa sababu kuna hili janga la watu kuvamiwa na majambazi na majangili katika sehemu nyingi za nchi. Tunachosema ni kwamba idadi iliyopelekwa katika shule zetu ni ya juu sana, na ni ya kuogofya wanafunzi wetu. Ningeisihi Kamati yetu husika ipendekeze kuwa askari pale shuleni watengewe sehemu maalum ili wasiwashtue wanafunzi wanapofanya mitihani yao. Itakuwa kheri ikiwa wengine wao watavaa mavazi ya kiraia, ili waweze kulinda wanafunzi wetu na kuimarisha usalama ...
view
24 Oct 2019 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I thought that Sen. (Dr.) Kabaka is in the Committee on Devolution and Intergovernmental Relations. I also thought that he was standing to confirm that we are going to summon the Cabinet Secretary so that he can give us more information.
view
24 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, kuna swali ambalo najiuliza. Seneti imetoa uamuzi wake. Je, tunaelewa mgogoro ulioko kule Taita Taveta? Uamuzi wetu ni kuwa madai yaliyoletwa hayana msingi wowote. Ukweli ni kwamba kuna mgogoro katika Kaunti ya Taita Taveta. Licha ya kuwa tumesema kuwa madai yaliyotolewa hayana msingi wowote, tunafaa kuwaunganisha watu wa kaunti hii. . Mimi ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali. Tulijaribu kuwaunganisha. Tulifanya hivyo mara si moja. Tulikutana na Wawakilishi wa Wadi na Naibu wa Gavana ili kujaribu kuwaunganisha. Hata hivyo, Seneti imeeleza katika Ripoti yake kwamba madai yaliyotajwa hayana msingi wowote. Hiyo itampa gavana nguvu ...
view
24 Oct 2019 in Senate:
Bw. Spika, nakubaliana na Sen. Cheruiyot kwa sababu Ripoti yenyewe ina kurasa 76. Pengine tungevunja rekodi ya dunia kuisoma kwa dakika 15. Huenda hapo ndipo makosa yalitokea. Nakubaliana na Ripoti hii. Nimechangia yangu kuihusu.
view
23 Oct 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ninaungana na wenzangu kumpongeza Sen. Shiyonga kwa kutunukiwa. Sen. Shiyonga ni mtu tunayemjua kwa kujitolea vizuri. Kwa hivyo, hii shahada ama kikombe alichopewa ni kwa sababu ya mambo aliyoyafanya, kwanza kabisa kwa kuwaangalia wajane na vijana. Hii ni kwa sababu hao ndio watu wanaonekana kama watu waliotengwa katika jamii zetu; wameachwa na hawaangaliwi kwa njia ifaayo. Kwa hivyo, ninataka kumpongeza na kumwambia kwamba, ni vizuri wakati akiangalia Kakamega, pia aangalie Bungoma na Kenya nzima, ndiposa anapopewa zawadi tofauti, ionekane---
view
23 Oct 2019 in Senate:
Nikisema Bungoma, ninamaanisha Kenya nzima. Nimesema hivyo kwa sababu Bungoma ni jirani yake, na ni vizuri mtu aanze kuhubiri Yerusalemu kabla hajaenda Judea na sehemu zile zingine. Kwa hivyo, sisi tunakupongeza na tunasema uendelee Kenya mzima, jumuia ya Afrika Mashariki na hata Afrika ndio uweze kupokea shahada tofauti. Sisi tunakufurahia na tunasema asante.
view