12 Mar 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, I rise, pursuant to Standing Order No.53(1) to seek a Statement from the Standing Committee on Land, Environment and Natural Resources on the status of the processing of land ownership documents for residents of Nanyuki and Makutano/Ngobit Wards in Laikipia County. In the Statement, the Committee should- (1) Provide a status update on the processing of title deeds and green cards for residents of Kanyoni and Shalom villages of Nanyuki and Makutano/Ngobit Wards respectively, stating challenges encountered, if any. ( 2) State when the State Department of Lands and Physical Planning, in partnership with the National Land ...
view
7 Mar 2024 in Senate:
Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, nampongeza Seneta wa Samburu kwa kuchukua jukumu na kufuatilia mambo ya usalama katika sehemu ya Samburu. Usalama umekosekana sio Samburu peke yake, bali pia Laikipia na Baringo. Tunaisha kwa hali ya sitofahamu. Kwa hivyo, namshukuru hasa Seneta wa Nandi kwa sababu ameleta Mswada unaosema kwamba wizi wa mifugo wa kimabavu uwe ugaidi. Kwa hivyo, kazi kuu ya Serikali ni kulinda maisha na mali ya wananchi. Ninakemea vitendo ambavyo vinafanywa na hawa wahalifu. Inapaswa Serikali iwachukue hawa kama magaidi kwa sababu sisi kama Wabunge tayari tumejitolea kupitisha Miswada. Inapaswa Serikali ...
view
7 Mar 2024 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nataka kuunga mkono Mswada huu wa bei nafuu za nyumba. Nilipokuja katika Seneti hii, nilisimama pale nikasema kwamba nitaiilinda, nitaitetea na ninataka kuongeza, nitaitekeleza Katiba. Katika Kipengee 43 cha Katiba, kinasema ya kwamba, wananchi wa Kenya, wanapaswa kupewa nyumba ambazo zinawafaa. Ni vizuri ijulikane---
view
7 Mar 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, Mswada ulio mbele yangu ni kuhusu nyumba. Mambo ya njaa tumeyashughulikia vilivyo na tumewapatia pembejeo. Yeye mwenyewe alipokuwa akizunguka na sufuria kichwani, sisi tulishughulikia mambo ya wananchi wa Kenya. Ni kazi ya Serikali kushughulikia wananchi wake kwa kuwapatia makao. Tukipitisha Mswada huu, Wakenya wengi wanaoishi katika hali ya uchochole, watapata makao. Mswada huu utashughulikia haya mambo. Tulipokua tukitembea katika Jamhuri ya Kenya tukifaya campaign, tuliwaahidi Wakenya nyumba za bei nafuu. Hayo ndio mambo tunayoangazia siku ya leo na tunapaswa kuyafanya.
view
7 Mar 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
7 Mar 2024 in Senate:
Jambo lengine ni hizi nyumba zitanufaisha Wakenya wetu. Niko katika Kamati ya Uchukuzi, Barabara na Ujenzi wa Nyumba. Watu wa matatu na jua kali walikuja kuleta mapendekezo yao kwa hii Kamati. Walisema ya kwamba itawasaidia ndugu zetu wahandisi, maseremala na waashi kupata kazi. Kwa hivyo, Mswada huu utawasaidia Wakenya kwa kuwapa kazi na nyumba ili watu wetu waache kuishi katika hali duni. Lakini, niliposikiliza ndugu zangu, wanasheria hawa wawili walipoongea, nilipigwa na butwaa kwa sababu tunaongelea kuhusu shida ya nyumba. Kwao, nyumba sio shida. Shida yao--- Bw. Spika wa Muda, maneno yananisumbua kwa sababu pengine hawa ndugu zangu hawajatembea mashinani ...
view
6 Mar 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia. Mwanzo, nakashifu mazoea ya Mawaziri kukosa kuja kwenye vikao vya Seneti ilhali, kwenye orodha ya shughuli bungeni tulikuwa tumenukuu mambo kadhaa ili tuweze kuyaangazia. Naungana na Sen. Mungatana kupinga kutumia Kanuni za Kudumu nambari 51(d) kwani tutakuwa tumetumia nguvu nyingi kwa Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Ustawi wa Jamii. Wengi walioongea wamesema Waziri wa Barabara na yule wa Fedha walipeana sababu tosha, lakini waziri wa jinsia achukuliwe hatua kali. Kama vile Sen. Mungatana alivyopendekeza kwenye SBC, tuweke faini ambayo tutapiga Waziri kabla ya kumtimua. Faini ya shilingi milioni moja ama tano. Waziri ...
view
21 Feb 2024 in Senate:
Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ningetaka kuunga mkono Ripoti hii ya NADCO. Nawapongeza viongozi ambao
view
21 Feb 2024 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view