16 Oct 2018 in Senate:
Bw. Naibu Spika, wewe na Seneti hili mnapaswa mshughulikie jambo hili kwa dharura. Pili, yale mapendekezo yatakayoletwa katika Jumba hili na Kamati hiyo yanafaa yafuatiliwe kabisa ili tuweze kuwasaidia wale Wakenya haraka iwezekanavyo kabla hawajaenda kwa Baba.
view
11 Oct 2018 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza, natuma risala za rambi rambi zangu na watu wa Kaunti ya Laikipia kwa familia za wale walipatwa na mkasa huu. Ni jambo la kuhuzunisha sana kwa sababu imekuwa ni kama jambo la mazoea kwetu hasa kama nchi kuwa hatupei umuhimu mambo ya watu ambao wana husika katika ajali. Ajali hutendeka, na mambo yana endlea. Swali ambalo tunafa kujiuliza ni kwamba: Wakati tulikuwa na Waziri Michuki sheria ilifuatwa zaidi kama vile tuko na Waziri Matiangi. Unapata ya kwamba ikiwa Waziri fulani ako katika Wizara fulani, sheria zina fuatwa. Ningependa kusisitiza kwamba ...
view
26 Sep 2018 in Senate:
On a point of information, Mr. Deputy Speaker, Sir.
view
26 Sep 2018 in Senate:
Mr. Deputy Speaker, Sir, I was with her so I can inform her.
view
26 Sep 2018 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, nataka kumpongeza Bw. Eliud Kipchoge kwa kuweza kuvunja rekodi ya dunia na kutuweka katika ramani ya dunia mzima.
view
26 Sep 2018 in Senate:
Bw. Naibu Spika, kuna jambo ninalosema ambalo ni la maana sana lakini wezangu wanawasiliana kwa sauti ya juu sana.
view
26 Sep 2018 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika. Jambo ambalo limeonekana katika nchi yetu ya Kenya ni ya kwamba ijapokuwa wanariadha wetu wanabobea sana katika mbio za nyika na nyinginezo, viwanja na vifaa vingine ni za duni sana. Ukitembelea Kaunti ya Laikipia, hasa Nyahururu, mahali hawa wanariadha wote wanaenda kufanya mazoezi, unapata ya kwamba hakuna uwanja wa kisasa wa kufanyanyia mazoezi yao. Nyahururu kuna hewa safi na iko katika nyanja za juu ambazo zinahitajika kwa ukimbiaji. Ni kama hapa Uasin Gishu. Kwa hivyo, ningeomba ya kwamba wakati ambapo tunajadili, na hasa Serikali inapoangalia mambo yake, ikifanya The electronic version of the Senate Hansard ...
view
26 Sep 2018 in Senate:
mpangilio, tusiwe tukifurahia wakati wanariadha wanafanya vizuri lakini hatuwakifikirii wanapokuja hapa nyumbani. Nimesikia viongozi wenzangu wakisema ya kwamba tuwe na vyuo ambapo watakuwa wakifunzwa vile ambavyo watakuwa wakitumia pesa zao. Hata wanasiasa wanapaswa waonyeshwe jinsi ya kutumia pesa zao kwa sababu wasipochaguliwa tena na wananchi, huwa wanakuwa katika shida na umaskini wa kupindukia. Ningependa kumwambia mwenzangu kwamba nimesikia akisema ya kwamba hapa ndiko nyumbani kwa wakimbiaji, lakini wametoka Kaunti ya Nandi. Na wana mashamba makubwa na mifugo huko nyumbani kwao. Ningependa kumuarifu ya kwamba si majengo peke yake ambayo yanaonyesha ya kwamba mtu amejikimu kimaisha. Unaeza kuwa na shamba kubwa ...
view
25 Sep 2018 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Swala hili la madini kupatikana katika nchi yetu ya Kenya limekuwa donda dugu. Ninaona ni kama tulipopewa Uhuru tulipewa uhuru wa bendera pekee. Kwa mambo ya uchumi, inaonekana kama tumeachia wale wageni wanaokuja katika nchi yetu na wao ndio wanaopatafaida. Wakenya wamebaki wanyonge baada ya kupatikana madini kama mafuta.
view