22 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
22 Jun 2023 in Senate:
kongole kwa sababu wakulima wa ndengu walikuwa hawajulikani. Nimewasikiza Maseneta wote walioongea na ni kama hawakufahamu ndengu kwa lugha ya kingereza ni nini. Kwa hivyo, Sen. Wambua nakupongeza kwa sababu wakulima walioonekana ni wa kahawa, majani chai, mahindi, pareto na pamba. Ninakushukuru kwa kuwapa hadhi wakulima wa ndengu. Nikianglia Mswada huu kwa undani, Sen. Wambua amependekeza kuwa ukulima wa ndengu utakuwa kilimo biashara. Mambo yote ambayo yametajwa hapa yanazingatia kuleta gharama nafuu ya ukulima wa ndengu. Ni vizuri ijulikane wazi kuwa anasisitiza ni mbegu gani zitakazotumiwa. Mbegu za hali ya juu ambazo utafiti umefanywa tayari. Sen. Wambua anasema ya kwamba ...
view
22 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, anaendelea kusema kwamba soko ya hawa wakulima wa ndengu inapaswa iangaliwe na ilindwe. Mkulima hutumia wakati wake mwingi kulima shamba lake. Baada ya kulima, wale walaghai ambao huwa katikati ya mkulima na yule ambaye atatumia chakula hiki, anaingilia kati. Unapata ya kwamba mkulima anagandamizwa kwa sababu hata bei anayouza bidhaa yake ni hafifu. Unampata huyu mkulima hawezi hata kujikimu kimaisha.
view
22 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nikiuangalia Mswada huu kwa kindani utaona ni Mswada ambao unapendekeza kilimo-biashara. Namshukuru Seneta kwa sababu amezingatia haya mambo. Anaendelea kusema kunapaswa kufanywe utafiti wa kutosha na kujulikane kabisa ni wakulima wangapi wanaokuza mimea hii. Ikijulikana ni wakulima wangapi, itakuwa rahisi sana kujua wakati tunatafuta soko zetu, tunatafuta soko za kiasi gani ya ndengu yetu.
view
22 Jun 2023 in Senate:
Nilimsilikiza Sen. (Prof.) Kamar akimuuliza maswali mwanafunzi wake, Sen. Wambua; “Itawezekanaje sasa kwa sababu mipaka imefunguliwa, mbegu zikatoka Tanzania na Uganda zikauzwa hapa kwetu Kenya?” Lakini, nikiangalia Mswada huu unavyopendekeza naona kwamba ukulima wetu utakuwa umefanywa kwa bei nafuu. Kwa hivyo, ndengu zozote zikiletwa kutoka nchi jirani, hazitaweza kushindana kwa bei na ndengu zetu. Wanaoagiza ndengu kuto nje wataona hii itakuwa kazi bure.
view
22 Jun 2023 in Senate:
Hana shida yoyote na ndengu ambazo zinatoka nchi ya nje. Lakini anasema tutakuwa tukijua kiasi cha ndengu ambacho tuko nacho. Anaendelea kusema kujulikane wale wanunuzi watakaonunua kwa idadi kubwa ni akina nani. Sina shaka rohoni yangu kuwa Mswada huu umezingatia mambo mengi. Hata nimemsikia Sen. Thang’wa akiuliza kwa nini hakukuwekwa maharagwe ya kawaida. Lakini, maharagwe yanajullikana. Nakubaliana na Sen. Wambua kwa kusema hangetaka kuleta mimea mingine kajadiliwa katika Mswada huu kwa sababu ingeleta vurgu. Yeye alitaka mmea huu wa ndengu uangaziwe pekee yake katika Mswada huu.
view
22 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
22 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nasimama kuunga mkono Mswada huu. Hili ni jambo nzuri, hasa katika Kaunti ya Laikipia. Tukizangatia mambo haya yote anayopendekeza katika Mswada huu kila kaunti ikiyangalia kwa undani, basi sisi sote tutafaidika. Wakulima wa Kaunti ya Laikipia wanaweza kuwatembelea wakulima wa Kaunti ya Kitui na kuona jinsi wanavyokuza ndengu zao. Mchanga ni upi uko pale katika Kaunti ya Kitui. Sisi katka Kaunti ya Laikipia tuna wanao wanasayansi ambao wanaweza kutushauri kama tunaweza kukuza ndengu. Wakulima wa ndengu katika Kaunti ya Laikipia watajulikani. Yeye amesema wakulima wa ndengu nchini Kenya haijulikani. Hili litakuwa ni jambo nzuri kwa sisi ...
view
21 Jun 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Naunga mkono Kauli iliyoletwa na Sen. Cherarkey. Ninawapa kongole wanariadha na wanamichezo wetu ambao wanaleta sifa katika nchi yetu. Faith, tulimuona katika uga akikimbia. Kila mtu alimshabikia. Kama vile Viongozi wa Walio Wengi na Walio Wachache walivyosema, wale ambao wameletea nchi yetu sifa ni vizuri waje kwenye Seneti. Tusiwe tunawaita wale ambao tunataka kuwauliza maswali pekee. Tunapaswa kuwaalika pia wale ambao tunapaswa kuwapa kongole na sifa. Hata wale hawakufanya vizuri leo, ni vizuri tuwape motisha kwa sababu wanawezakufanya vizuri leo, lakini kesho wanaweza kufanya vizuri zaidi. Tusiwe tunawashabikia sana wale waliofanya vizuri tu, wale wengine wangefanya vizuri ...
view
21 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view