20 Jun 2023 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, you tell us that we should not shout but put--- When I talk, you say I am not following the correct procedure---
view
20 Jun 2023 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, it is concerning tomorrow.
view
20 Jun 2023 in Senate:
Bw. Spika, nachukua fursa hii kuunga mkono Taarifa iliyoletwa na Seneta wa Bungoma County.
view
20 Jun 2023 in Senate:
Ni kweli kwamba mambo ya pombe haramu yameathiri watu engi katika sehemu zote. Ni vizuri ijulikane wazi kwamba Serikali imejizatiti kupambana na jambo hili. Hivi majuzi, tulikuwa Nakuru kama viongozi wa Bonde la Ufa, kama ilivyokuwa ikijulikana, ili tuweza kupigana na pombe haramu. Lakini, pombe haramu isiwe kisingizio kwa polisi kuwashambulia wananchi wanaoendelea na shughuli zao za kawaida.
view
20 Jun 2023 in Senate:
Ukitembea sehemu nyingi, utapata vijana wameketi katika mitaa wakiwa walevi chakari. Ni vizuri pombe haramu zipigwe vita kama tunataka kupiga hatua kimaendeleo. Wakati mambo haya yanapofanywa, ni vizuri vijana wetu watafutiwe kazi. Hii ndio sababu serikali inasema ni vizuri nyumba zijengwe ili vijana waweze kupata ajira. Vijana wengi wanakaa mitaani na mijini bila kazi na wanakunywa pombe; ni vinyo kila mahali.
view
20 Jun 2023 in Senate:
Kuna zile pombe za kitamaduni zinazokubalika zisizoathiri afya ya watu. Lakini, hata hivyo, serikali imejizatiti na kujitolea kupigana na pombe haramu. Naunga mkono Taarifa hii kwa sababu ukitembea sehemu za Laikipia, utapata vijana wamelala na hawafanyi chochote. Naunga mkono serikali kuendelea kupigana na hizi pombe haramu lakini wasiwavamie wananchi wasiokuwa na makosa yeyote.
view
20 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
20 Jun 2023 in Senate:
Nikiwa papo hapo, ningependa kuongelea jambo ambalo ulisema ya kwamba utataja wakati Senate Business Committee (SBC) watakapoketi. Niliangalia vikao vya kesho asubuhi; nilikuwa na maswali ambayo nilikuwa nimeuliza Waziri wa Usalama, Prof. Kindiki; swali nambari 11 na 12. Hayo maswali yamekuwa yakiahirishwa kila wakati kwa sababu Waziri amekuwa hapatikani ata ijapokuwa katika taarifa yako ulisema wanatoa sababu za kutokuja. Nashukuru kwa sababu umesema hivyo visiwe vijisababu vya mtu kuwa na shughuli nyingi kwa sababu hata kuja Seneti ni shughuli anayopaswa kuzingatia.
view
20 Jun 2023 in Senate:
Nilitaka kujua SBC ilisema vipi kuhusu haya maswali yangu Nambari 11 na 12 kwa Waziri wa Usalama. Nikiangalia taratibu za shughuli za kesho katika Kikao cha asubuhi, maswali hayo hayako. Sijui SBC ilisema vipi kwa sababu wiki jana ulipokuwa ukitoa taarifa yako, ulisema tunaweza kutumia Kanuni za Kudumu No. 51(d) tuweze kumng’atua Waziri ambaye hatakuwa akija kujibu maswali kama inavyozingatiwa na taratibu za Bunge.
view