John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 441 to 450 of 2259.

  • 30 May 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika. Kwanza, naunga mkono Hoja hii. Ibara ya 96 ya Katiba ya Kenya inasema kwamba kazi kuu ya Seneti ni kulinda na kutetea gatuzi zetu. Itakuwa jambo la kuvunja moyo ikiwa tutasema ya kwamba tunatetea gatuzi zetu na hatuzifahamu na hata hatujui pahali ziko. Kwa hivyo, tutakuwa tukifanya jambo la muhimu kuitembelea Turkana. Nilisikia Kiongozi wa Wachache akisema hajatembea sehemu hiyo. Si yeye pekee bali wako wengi. Itakuwa ni jambo nzuri sisi kutembelea gatuzi zetu ili tuweze kujua masaibu na changamoto wale wanaoishi pale wanapitia ama vile vile mambo ya manufaa wanayoyatenda ambayo sisi tunaweza tukaiga katika kaunti ... view
  • 30 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 30 May 2023 in Senate: Pengine, ifikapo mwaka ujao, ningeomba tutembee Laikipia kwa sababu ikiwa ni mambo ya ukame, ufugaji na usalama ndiyo ilikuwa inaangaziwa, basi Laikipia pia kuna ukame, ufugaji na usalama. Bw. Spika, kwa hivyo, ningeomba tukitoka Turkana tutembee Laikipia, ndio wananchi wa Laikipia waweze kuwaona viongozi wao waliobobea kama vile Sen. Ali Roba, Sen. Mandago, Sen. Cherarkey, Sen. Joe Nyutu, the bull fighter, Sen. Wamatinga, Sen. Chesang, Sen. Maanzo kutoka Makueni, Sen. Sifuna wa hapa Nairobi na Sen. Faki kutoka Mombasa. Kwa hivyo, ninashukuru kwa sababu tutaenda Turkana. Nina uhakika tutaenda Laikipia hata ijapokuwa wanasema chelewa chelewa utapata mwana si wako. Mimi ... view
  • 23 May 2023 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kuanzia mwanzo, ninaunga mkono dua hili ambalo limeletwa na Sen. Thnag’wa kwa sababu ya shamba la familia ya Mbogo Wainaina kuchukuliwa. Mambo ya mashamba katika Jamhuri yetu ya Kenya imekuwa ni donda sugu. Watu wengi wamekuwa wakigandamizwa na wale ambao wanafikiria wako na nguvu kuliko wegine. Kwa hivyo, ninakubaliana na Sen. Thang’wa ya kwamba, familia ya Mbogo Wainaina imefanya vizuri kuleta taarifa hii. Wamefanya jambo lingine muhimu kwa kusema kwamba wanapatia jukumu Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili ambayo iko katika Senenti hii. Wanauhakika na wanaamini ya kwamba itaweza kutenda haki. Ndiposa kulingana ... view
  • 23 May 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 23 May 2023 in Senate: Bw. Spika, ningependa hii familia ya Mbogo Wainaina itendewe haki na waweze kupewa fidia kwa kugandamizwa. Ni vizuri wakati Kamati hiyo inashughulikia jambo hili, iangalie maswala mengine katika sehemu hiyo ya Kaunti ya Kiambu. Ukitembea sehemu nyingi za nchi yetu ya Kenya, kuna shida za mashamba ambazo zinafanya watu wauane. Kwa hivyo, ningependa kuuliza Kamati hiyo, wakati wanashughulikia swala hili, washughulikie hata sehemu zingine. Ukitembea Kaunti ya Laikipia, upande wa Marmanet, watu walifurushwa kutoka mashamba yao na wanapaswa kilipwa fidia. Ukitembea sehemu za Matanya, vile vile, kuna ile shida. Unapata watu wametolewa katika mashamba yao na wanaishi katika maisha ya ... view
  • 27 Apr 2023 in Senate: Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Katika Seneti iliyopita nilikua mwenyekiti wa Ugatuzi. view
  • 27 Apr 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 27 Apr 2023 in Senate: Ni ukweli sheria alizozitaja ni zile ambazo zinapaswa kurekebishwa. Nashukuru kamati hiyo kwa kazi nzuri walioifanya wakiongozwa na Sen. Abbas na naibu wake. Ni vizuri maana hiyo kamati haijaketi tu bali pia wameangalia kile ambacho kinaleta uzuizi katika gatuzi zetu. Sheria hizi zikibadilishwa, ugatuzi utaendelea vizuri. Kazi kubwa ya Seneti hii ni kufanya gatuzi zetu ziendelee kua na nguvu na kunawiri. Nimesimama kuunga mkono na kuwapongeza kamati hiyo kwa juhudi zao nzuri. Kamati zile zingine zikifanya hivyo, Seneti itakua katika kipao mbele kunawirisha gatuzi zetu. Asante na napongeza hiyo kamati. view
  • 27 Apr 2023 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nachukua fursa hii kuunga mkono Hoja hii na Kamati iliyoteuliwa. Hawa ni watu ambao wana uwezo na ujuzi wa kutekeleza haya majukumu. Kwanza, ijulikane wazi ya kwamba jukumu hili tunalowapa kama Seneti sio jukumu ndogo. Ni nzito. Nimemsikiza Sen. Mungatana, MGH, na tayari amekubali. Anajua ni jukumu nzito na wataenda kukabiliana na majukumu mazito. Nikijaribu kulinganisha, wataenda kukabiliana na mazini yenyewe. Bi. Spika wa Muda, ukikumbuka wakati Seneta alienda kuangalia mambo ya Jim Jones, ilifika wakati fulani Seneta huyo akauwao. Kwa hivyo, hata hawa Maseneta wetu, tunawaambia majukumu ambayo mtapambana nayo ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus