John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 751 to 760 of 2259.

  • 8 Sep 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 8 Sep 2022 in Senate: twende katika upeo wa pili au wajuu zaidi na ukapata ndio. Kwa hivyo, sikuwa na shaka rohoni ya kwamba Spika tuliyenaye amebobea katika kazi yake. Mimi najua ya kwamba tutatoka kikao hiki tukiwa sisi wote tumekubaliana na ninajua ya kwamba sisi sasa tukiwa hapa kama Seneti tutatembea pamoja. Nimemsikia Mhe. Sen. Soipan akisema ya kwamba yeye mwenyewe amekubali ya kwamba hili ndilo jumba kuu ambalo litaendelea kufanya maswala ambayo yanafanywa katika majumba makuu ya jumhuri ya Kenya na hata dunia kwa jumla. Kwa hivyo, nakupongeza na kukutakia mema. Nina kuhakikishia kwamba nitakuunga mkono na naibu wako Mhe. Kathuri ili Seneti ... view
  • 21 Jun 2022 in Senate: Asante sana Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Nataka kuungana nawe kukaribisha ujumbe kutoka Narok Kaskazini; wakulima wa viazi na shayiri. Ni dhahiri shahiri kwamba ukitembelea sehemu nyingi za Kenya, hasa sehemu ambazo kuna wakulima, unapata barabara sio nzuri. Kwa hivyo, inakuwa vigumu kwao kupeleka mazao yao sokoni. Nimekuwa nikiongea na Sen. Olekina tukiwa naye kwenye Kamati ya Kawi. Alikuwa akiangazia akisema ya kwamba hakuna umeme. Hilo ni jambo ambalo limekuwa kizungumkuti pale. Kwa hivyo, vile ambavyo ningependa kuwaambia, kwa sababu wanawakilisha watu wa kutoka upande huo, ni vizuri waseme ya kwamba Seneta amekuwa akipigania mambo ya umeme iweze kupelekwa ... view
  • 21 Jun 2022 in Senate: mahali ambapo wanaweza kuweka viazi vyao na wakati bei imekuwa nzuri wakaviuza. Hilo ndilo jambo linalopaswa kushughulikiwa. Tunampongeza Sen. Olekina leo kwa sababu yeye ni mmoja wa wale ambao wamesema ya kwamba utamaduni mpaka udumishwe. Yeye ni kielelezo tosha katika nchi yetu ya Kenya kwa kuzingatia utamaduni. Si utamaduni peke yake, vile vile, amekuwa akipigania haki za kabila la Wamaasai. Sisemi yeye ni mkabila, lakini anajua mahali ametoka na amekuwa akiwapigania zaidi. Nikimalizia, wakulima watafaidika Zaidi, na tunapaswa kuwainua watu ambao wanaishi maisha ya chini. Wajiunge na serikali ambayo inakuja itakayoongozwa na Mhe. William Samoei arap Ruto, kwa sababu inazingatia ... view
  • 21 Jun 2022 in Senate: Asante Bw. Spika. Ninajiunga na wewe kuwakaribisha wanafunzi katika Kikao hiki cha Seneti. Ningependa kuwaambia kwamba ni muhimu kuweka masomo mbele. Masomo ndio uti wa mgongo wa maendeleo katika nchi yetu ya Kenya. Viongozi wote walio hapa walitilia mkazo masomo wakati walipokuwa vijana. Huu ndio wakati wa kutengeneza maisha yenu ya usoni. Waswahili husema, udongo ufinyange ukiwa mbichi. Mkitia bidii katika masomo yenu, mtapata kile ambacho mnatazamia katika maisha ya mbeleni. Mambo mawili ya kufanya ni kutilia masomo mkazo, kisha kuwa na nidhamu pia. view
  • 16 Jun 2022 in Senate: Bw. Spika, nafikiri Kiongozi wa Wachache anataka kusema kuwa nimeshazungumza. Ni kama hataki niseme jambo lolote. Ukweli kuhusu mkopo ambao utachukuliwa wa zaidi ya Kshs1.1 billion ni kuwa watu wa Laikipia wamesema kwamba wakati huu hawawezi kujihimidi. Jambo lingine ni kuwa Kamati ya Fedha na Bajeti ya Seneti haikuniuliza kama vile tumekuwa tukifanya shughuli zetu katika Bunge hii. Ikiwa kuna Hoja ambayo inahusisha kaunti fulani, Seneta mwakilishi huitwa ili asaidie kuchanganua mambo. Bw. Spika, watu wa Laikipia wamesema kinagaubaga kuwa kukopa si kubaya, lakini hawataki mkopo wakati huu kwa sababu hawakuhusishwa. Kwa Kiingereza tunasema, public participation . Wamekubali kuwa kuna ... view
  • 16 Jun 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 16 Jun 2022 in Senate: Naomba Seneti hii ipinge Hoja hii. view
  • 16 Jun 2022 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. view
  • 16 Jun 2022 in Senate: Bw. Spika, Sen. Farhiya anasema ukweli kwamba kuna ushuru unaotozwa Laikipia. Hata hivyo, utozaji wa ushuru umekuwa ukikandamiza watu wa Laikipia kwa kuwa hawapumui. Ni kama jamaa wa kule Marekani kwa jina George Floyd alivyowekewa goti. Tunapowaambia hatupumui, bado goti linawekwa. Ijapokuwa kuna utozaji wa ushuru, ushuru huo umetukandamiza zaidi. Sasa wanataka kuchukua mkopo. Nataka kukuhakikishia kwamba hiyo itawafanya watu wa Lakipikia si tu kushindwa kupua bali pia kuaga dunia. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus