31 Aug 2023 in Senate:
. Mazingara ni mbinu za uchawi.
view
31 Aug 2023 in Senate:
Yanaitwa mazingira. Kwa hivyo, kuna umuhimu zaidi kuliko mbeleni kuthibiti mazingira kwa sababu kuna kazawadi. There is an incentive . Tukiangalia hizi ekari 400,000, kando na kuwa tunafaidi kiutalii, pia kuanzia sasa tukipitisha Mswada huu leo, tutapata faida kupitia kwa mkopo wa kaboni. La mwisho kabisa, serikali za kaunti zimepatiwa kazi. Katika kutengeneze mipango yao ya miaka mitano ama County Integrated Development Plan (CIDP), waweke pia mambo ya kuthibiti tabia nchi ama climate change action . Ya kwamba watapanda miti mingapi kama miradi ya miaka mitano. Katika bajeti zao, waweke mambo ya kuthibiti uharibifu wa mazingira ambao unapelekea mabadiliko---
view
29 Aug 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa fursa hii uliyonipa kuchangia Hoja hii ya kuundwa kwa Kamati ya uwiano katika Jamhuri yetu ya Kenya. Ninaunga mkono majina yote yaliyotolewa na upande wa walio wengi na upande wa walio wachache. Kamati hii ni ya mazungumzo ya kuleta uwiano na amani nchini Kenya. Swala la amani ni muhimu sana. Lakini kuwa na amani siyo ukosefu wa vita. Kunaweza kuwa na amani, lakini kuna watu walio na masononeko na manung’uniko mengi. Wakati tulifanya uchaguzi na tukapata Mhe. Rais, kulikuwa na kesi ndogo. Upande wa Azimio ulisema ya kwamba kuna maswala fulani ambayo hawajakubaliana nayo katika uchaguzi. ...
view
29 Aug 2023 in Senate:
Jambo la kwanza ni kufungua server. Hii ni Kwa sababu katika uchaguzi, ni lazima tuangalie kama tulienda vizuri na tutafanya hivyo kwa kuaangalia server. Taasisi ambazo zinatumia pesa huwa zinafanya uhasibu ambao ni jambo muhimu. Katika yale mazungumzo ni vyema ripoti itayokuja iaangalie ni vipi tutafungua ile
view
29 Aug 2023 in Senate:
Jambo la pili ni kuhusu mfumuko wa bei ya bidhaa. Baada ya kufanya uchaguzi na tukawa na Serikali, hali ya maisha imekuwa ya juu na ghali muno. Lakini, Serikali inapandisha ushuru na---
view
29 Aug 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa huo mwelekeo. Lakini, katika maswala ambayo yako katika meza, kutoka kwa upande wa Azimio, moja ilikuwa ni kufanya uhasibu ama audit ya server. Kwa hivyo, nikitaja server ni kwa sababu swala moja ambalo liko katika majadiliano litakuwa ni kufungua server. Mambo ya maandamano ni haki yetu kama Wakenya katika Ibara ya 37. Ninaona maandamano yakitokea hata katika Kaunti ya Uasin Gishu kwa sababu watu wanataka pesa zao ambazo walilipa kwenda ngámbo. Lazima hiyo server ifunguliwe tujue ni nini ambacho kilitokea.
view
10 Aug 2023 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda kwa fursa hii uliyonipa ili kuchangia taarifa ambayo imeletwa na Senenta wa Kaunti ya Machakos, Sen. Kavindu Muthama, kuhusu mipaka kati ya kaunti mbali mbali.
view
10 Aug 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
10 Aug 2023 in Senate:
Swala la mipaka kati ya kaunti zetu ni swala nyeti. Kaunti nyingi zina utata wa mipaka. Kaunti za sasa hivi zinategemea sheria ya Mikoa na Wilaya ya mwaka wa 1992 ama District and Provinces Act ya 1992. Kwa sasa, kuna kaunti nyingi ambazo zina shida ya mipaka. Ukosefu wa kuelewana katika mipaka ya kaunti umeleta utovu wa usalama mara nyingi.
view
10 Aug 2023 in Senate:
Kule kwetu, Kaunti ya Taita Taveta, tuna shida ya mipaka kati ya Taita Taveta na Kwale; Taita Taveta na Makueni na Taita Taveta na Kajiado. Nimeleta mara zaidi ya mia katika hili Bunge, swala la kuangazia mipaka kati ya Taita Taveta na kaunti ambazo ni jirani.
view