4 Dec 2024 in National Assembly:
Mr. Temporary Chairperson, Sir, I vote, yes.
view
20 Nov 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa hii fursa uliyonipa ili nikaribishe Kamati Maalum ya Sheria iliyokabidhiwa ya Bunge la Kaunti ya Taita Taveta. Walikuja jana na leo. Nafikiri wataondoka kesho. Wamepata fursa nzuri ya kukutana na Kamati Maalum ya Sheria ya Seneti. Najua wamejifunza mengi kwa sababu wamekuja kwa safari ya kujifunza. Karibuni sana Seneti. Seneti na Bunge za Kaunti zinafanya kazi sawa ambazo ni uangalizi, kutunga sheria na uwakilishaji. Najua tunapeleka pesa nyingi sana kwa gatuzi. Ugatuzi ndio kitu cha maana sana ambacho tulijipatia kwa Katiba ya 2010. Najua wamejifunza mengi kutokana na hii safari yao ya Seneti. Najua wakirudi watatekeleza. ...
view
20 Nov 2024 in Senate:
Pia najua Kamati ya Sheria iliyokabidhiwa nao pia wamejifunza mengi. Kama kuna mambo yatakayohitaji kutunga sheria zaidi za kulinda gatuzi, najua Kamati hii ya Seneti itatuelezea. Bunge la Kaunti ya Taita Taveta lilikuwa liwe mwenyeji wa Seneti Mashinani huu mwaka. Tulikuwa tunashindana na Kaunti ya Busia. Lakini changamoto iliyokuwa pale ni ya nafasi ya Bunge la Kaunti ya Taita Taveta kuwa ndogo. Lakini nafurahia na Kaimu Spika yuko pale ya kwamba Kaunti ya Taita Taveta wameanza kujenga Bunge lingine. Najua katika siku za usoni, wakati tunaangalia kaunti ya kwenda, basi Taita Taveta itakuwa ni mmojawapo za kaunti za kupeleka Seneti ...
view
13 Nov 2024 in Senate:
Asante Mhe. Naibu Spika, kwa hii fursa uliyonipa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate.
view
13 Nov 2024 in Senate:
Tulipoanza huu Muhula, tulibadilisha kanuni tukasema, Wednesdays Mawaziri wawe wakija kujibu maswali ya Maseneta. Ikiwa Mawaziri, watendakazi, au the Executive wanaona kwamba hawawezi kuja hii siku kujibu maswali, tubadilishe kanuni kwa sababu kuna kazi nyingi sana za kufanya. Kuna maswali mengi ya Kamati ambayo hayajajibiwa na mengine yamemaliza miaka, kama vile maswali ya mashamba na tourism, mambo kupigano kati ya wanyama pori na wananchi. Kuna maswala mengi ambayo tungekuwa tunayafanya katika Kamati siku kama ya leo. Kwa hivyo, kama Mawaziri hawawezi kuja, ni vizuri tuangalie ili tubadilishe Kanuni ama Standing Orders ili tupate Wednesdays kama siku ya kuita Mawaziri na ...
view
13 Nov 2024 in Senate:
, hii SHA haifanyi kazi. Huduma za afya zimedorora, haielewki inafanya kazi vipi na wananchi wetu wanateseka. Kwa hivyo, nakashifu kwa kinywa kipana kutokuja kwa Waziri wa Afya katika hili Bunge. Asante.
view
31 Oct 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir, for this opportunity. I rise pursuant to Standing Order No.53(1) to seek a statement from the Standing Committee on Land, Environment, and Natural Resources regarding the Kshs908 million compensation fund released by the Government for victims of wildlife attacks in Taita-Taveta County and across the country. This compensation was announced on July 12, 2023, by the then Cabinet Secretary for Tourism and Wildlife, Hon. Peninah Malonza, at a ceremony held in Voi, Taita-Tabeta County. In the Statement, the Committee should- (1) List all claimants, specifying the nature of each claim, the date of the incident, ...
view
31 Oct 2024 in Senate:
breakdown of how the Kshs51.5 million set aside for 350 victims in Taita-Taveta County was allocated. (2) Provide status on all paid and unpaid claims, detailing the reasons for any unpaid claims, and indicate the expected timeline for their settlement. (3) State the annual budget allocated for compensation related to wildlife attacks on individuals. (4) Specify the maximum and minimum period within which claims should be settled, stating reprieve measures by the Kenya Wildlife Service (KWS) if payments are delayed beyond this period. (5) Provide an update on the status of Kshs322 million promised to settle claims dating back to ...
view
30 Oct 2024 in Senate:
Asante Mhe. Naibu Spika kwa fursa hii ili nichangie mjadala muhimu kuhusu Mswada wa kupatia bunge za kaunti uhuru. Kumekuwa na mjadala kwamba bunge za kaunti haziwezi kutimiza majukumu yao ambayo ni uangalizi, kutunga sheria na uwakilishaji vizuri kwa sababu hawana uhuru. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only.A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and Audio Services,Senate.
view
30 Oct 2024 in Senate:
Mhe. Naibu Spika, nakushukuru kwa hekima na ubunifu wako wa utunzi wa sheria. Tukibadilisha hii sheria ya the County Public Finance Laws (Amendment) Bill (Senate BillsNo.39 of 2023), bunge za kaunti zitapata uhuru wake. Pesa nyingi huenda kwa magatuzi na kusipokuwa na bunge za gatuzi zinazofanya kazi vizuri, pesa nyingi hupotea, na wananchi nyanjani hawapati maendeleo ipasavyo. Mwaka wa 2010 tulijipatia Katiba iliyoleta ugatuzi. Hii ilimaanisha kwamba pesa zitoke Serikali kuu na kuenda mashinani, lakini magavana wameendelea kunyanyasa bunge za kaunti. Kwa mfano, mwaka wa 2021 nilikuwa katika Kamati ya Uhasibu ya Seneti na bunge za kaunti zingine hazikuwa zinalipwa ...
view