10 Oct 2013 in Senate:
On a point of order, Madam Temporary Speaker.
view
10 Oct 2013 in Senate:
Madam Temporary Speaker, with all due respect, you will notice that Sen. Mutula Kilonzo Jnr. is not in the House yet he is the one who sought this Statement. I do not know how appropriate it will be to receive the answer in his absence. He needs to be here to ventilate and query the Statement.
view
10 Oct 2013 in Senate:
Madam Temporary Speaker, I seek clarification following the Statement presented here. The amount allocated for this contract was Kshs1,895,094,559. Already almost Kshs1.5 billion has been paid and the allocation this year is only Kshs300 million. That covers the whole amount for the tender. From the Statement, it is not even 50 per cent of the road that has been done but Kshs1.8 billion has already been paid. The work has now stopped and will never reach where it was supposed to reach. You also heard that 24 months have elapsed but 68 weeks have been added to the contract period ...
view
10 Oct 2013 in Senate:
On a point of order, Madam Temporary Speaker. You have heard the Chairperson say that she does not have substantial evidence that can make her blacklist this contractor but we came out very clearly and gave evidence that the work done here is less than 50 per cent and the amount of money paid is about 84 per cent. What other evidence does she want to prove to her that this is a notorious contractor, several jobs have been cited and the contractor has failed completely to meet the requirements of the tender terms?
view
10 Oct 2013 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, nakushukuru sana kwa nafasi hii ili niweze kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Sen. (Prof.) Lonyangapuo, ambaye ameonyesha kuwa anajali taifa hili na wala sio tu kaunti yake anayoiwakilisha hapa. Hoja hii inahusu nchi nzima na rasilmali zetu. Bw. Spika wa Muda, nimeamua kuzungumza kwa Kiswahiil ili niweze kutafakari na kukumbuka maneno ya wimbo mmoja ambao ulikuwa unaimbwa zamani nikiwa kijana. Ulikuwa unasema kuwa ukitaka kuisaidia nchi hii, nunua mali ya Kenya. Ulikuwa unasema kuwa Bw. Kamau ananunua mali ya Kenya na kwa hivyo, anaongezea uchumi wa nchi hii nguvu sana. Wimbo huo ulikuwa unataja ...
view
24 Sep 2013 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ningependa kuungana na wenzangu kutoa rambi rambi zangu kwa Wakenya waliopoteza maisha yao na hasa taifa nzima. Nimeshangaa sana kuona ya kwamba, vile tunavyozungumzia mambo haya, nchi yetu imesimamiwa na Wakenya. Juzi tulishangaa tuliopoona mlanguzi wa madawa ya kulevya akipelekwa kwao kule Nigeria na baada ya wiki tatu, huyo mlanguzi alipatikana katika nchi yetu akiwa ametengenezewa makaratasi ya kuingia nchini na Wakenya wenyewe. Jambo lilioko mbele yetu ni kwamba nchi ya Kenya imepigwa na kama wananchi, tunataka kuungana pamoja ili tulinde taifa letu. Ningependa kusema wazi wazi kwamba tunaweza kutofautiana hapa kama wanasiasa lakini akitokea ...
view
24 Sep 2013 in Senate:
Adui amefika kwa nyumba na ni jukumu la Wakenya kuungana pamoja na kumtoa. Hawa maharamia wanatuchukia na taifa letu kwa sababu tumeingia nchi ya Somalia. Hatukuingia nchi ya Somalia kwa sababu tulikaribishwa ama kulikuwa na mali ambayo Kenya ilitaka kuchukua kutoka nchi ya Somalia. Hakuna chochote cha thamani Wakenya wanaweza kuchukua kutoka nchi ya Somalia. Lakini wao wameingia ndani ya nyumba yetu na kuanza kuchukua watoto wetu. Walianza kuchukua wageni hapa nchini na kuwapeleka kwao. Ilikuwa ni kawaida ya taifa nzima kumfuata yule adui na kumfunza adabu. Kwa hivyo, kama wanafikiri watakuja kutuchokoza ili watuumize, inafaa wafahamu kwamba, taifa hili ...
view
24 Sep 2013 in Senate:
Bw. Naibu Spika, tukiongea haya maneno yote, ni aibu kusikia kwamba eti vitambulisho vyetu vinauzwa na Idara ya Uhamiaji kwa Kshs200. Hakuna Msomali wa Kenya anayeweza kupata kitambulisho katika taifa letu bila kuulizwa babu yake alikufa akiwa na meno mangapi lakini Wasomali wanaotoka nje, wanapewa vitambulisho bila kuulizwa maswali. Wale wahuni wanataka kutugawanya kwa misingi ya dini. Ninakubaliana na Sen. Haji kwamba hakuna Mwislamu – vile ninavyowafahamu – ambaye anaweza kukubali The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
24 Sep 2013 in Senate:
mtu mwingine ateseke. Kurani na Biblia ni kitu kimoja ila tofauti ni kidogo sana. Tunavyoamini kama Wakristo ndivyo Waislamu wanavyoamini. Kwa hivyo, wale wanaotaka kuleta siasa kwamba watu walikuwa wanaulizwa kama ni Waislamu au Wakristo, Wahindi ama wakosa dini, si ukweli. Watu waliuwawa na hakuna vile mtoto wa miaka miwili, kwa mfano, angeulizwa dini yake. Wale wanaoongea mambo hayo wanatuhuzunisha na nia yao ni kutugonganisha.
view
24 Sep 2013 in Senate:
Vile Sen. Mbuvi amesema hapa – na ninarudia – hakuna kitengo ambacho hakisimamiwi na Mkenya. Kwa hivyo, kama mwenye kuongoza idara ya kuchunguza na kufahamu ni nani anayeingia na kutoka nchini amelala, ni jukumu la Wakenya kumwondoa na kuweka Mkenya mwingine kufanya kazi hiyo. Sisi hatuwezi kuhatarisha maisha ya watu ovyo ovyo. Unawezaji kuwa nahodha wa meli na inazama na ukose kuulizwa kazi yako ni nini? Kama hutaki kuulizwa, usiwe nahodha wa hiyo meli. Inafaa ukae kando ili iendeshwe na mwingine halafu ikizama, yeye aulizwe. Watu 15 ambao wamejihami wakiingia katika shopping mall, hili ni jeshi nzima.
view