Johnson Nduya Muthama

Born

20th October 1954

Post

Parliament Building, P. O. Box 41842-00100 Nairobi

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

info@jnmholdings.co.ke.

Telephone

0733900300

All parliamentary appearances

Entries 711 to 720 of 1060.

  • 7 Mar 2012 in National Assembly: On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. It is very clear that those who are debating in support of this Report are supporting what is written here. Those who are opposing are out to challenge what is written here. So, there is no point to rise on a point of order seeking justification all the time. Would I be in order to say that they should sit down and listen to what we are going to challenge here? You did not write this Report to bring it here and then we accept it! view
  • 16 Feb 2012 in National Assembly: Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Mswada huu kuhusu kubuniwa kwa Serikali za Kaunti hapa nchi. Ningependa pia kutoa shukrani nyingi kwa Waziri kwa kuleta Mswada huu hapa Bungeni. Huu ni Mswada ambao umeratibiwa baada ya kuzingatia maoni na fikra za wananchi wote. Hata hivyo, kuna baadhi ya mambo ambayo ningependa kuyazungumzia kwa kina kirefu kwa sababu tunajua kila jambo lina uzuri na ubaya wake. Jambo la kwanza ni kuhusu uhusiano wa kaunti na kampuni za kibinafsi. Hapa inapendekezwa kuwa kaunti inaweza kuwa na ushirikiano na kampuni au mashirika ya kibinafsi. Wasiwasi wangu ... view
  • 16 Feb 2012 in National Assembly: Ukulingana na Kipengee cha Tatu cha Mswada huu, kaunti yenyewe inaweza kubuni kampuni yake kwa minajili ya kutoa huduma fulani kwa wananchi wake. Kipengee hiki kinaweza kutumiwa na gavana na maofisa wake ili waanzishe kampuni zao. Wakati mwingine utaona ya kwamba gavana anaweza kuwahimiza watu wake kubuni kampuni huko akiwaahidi kuwa kaunti yake itafanya biashara na wao. Tunajua ya kwamba sheria za wafanyakazi wa Serikali zinawanyima haki ya kufanya biashara na Serikali hata kama wana kampuni zao za kibinafsi. Hii ni kwa sababu matendo yao yataleta mvutano kazini. Ni lazima Waziri pamoja na Serikali kuwa macho na kuhakikisha kwamba watakaofanya ... view
  • 16 Feb 2012 in National Assembly: Jambo la tatu ni kuhusu kuteuliwa kwa Wabunge sita maalum wa Bunge la Kaunti hapa nchini. Ikiwa uteuzi huu hautafanywa ka njia mwafaka utaleta hali ya kuvuta ni kuvute. Wakiteuliwa mara moja, tena baadaye kutakuwa na mjadala wa kuangalia idadi kamili ya Wabunge maalum watakaoteuliwa. Wakati huu kuna malumbano makali kuhusu mipaka ya maeneo ya Bunge. Ripoti imetolewa na watu wengi hawajaridhika na mapendekezo yake. Kwa hiyo, ni lazima mambo haya ya mipaka ya uwakilishi Bungeni yafanywe kwa njia itakayoridhisha watu wote. Tusipofanya hivyo kutakuwa na malumbano makubwa na tutapoteza wakati na pesa kutafuta tena maoni ya wananchi. Haifa kuunda ... view
  • 16 Feb 2012 in National Assembly: Kwa hivyo, naomba kwamba kiwango fulani kiwe. Kama ni Kaunti mbili zinafaa kupata uteuzi wa mtu mmoja. Kama ni Kaunti tatu, zinafaa kupata watu wawili. Hesabu hiyo ni rahisi. Kwa mfano, kama ni Kaunti ya Machakos ambako nataka kuwa Seneta, nitajua kwamba wadi ambazo niko nazo ni 30 au 40 na kati ya hizo ninaweza kuwateuwa wajumbe kiasi fulani, ili mambo yaweze kufanyika kwa urahisi sana bila kupoteza wakati. view
  • 16 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, Kaunti itakuwa kama Serikali, kwa sababu itakuwa na bendera, seal na labda hata wimbo wake maalum. Kaunti itapewa uhuru hata wa kukopa pesa. Hata hivyo, Mswada huu hauonyeshi wazi mamlaka haya yanafika wapi. Hata pesa zinaweza kukopwa kutoka kwa mtu binafsi kisha Kaunti inawekwa kwenye matatizo. Wanaweza kuonyesha kwamba wako na pesa, kumbe ni watu fulani ambao wameingia na kufanya ufisadi. Utaona kwamba hizo pesa ambazo zinakopwa labda hata haziendi kufanya kazi inayotakikana. Ni lazima kuwe na mikakati, kutoka nyanja za juu kuteremka chini, ili kuhakikisha kwamba wakati Kaunti inakopa pesa kuna mkataba. view
  • 16 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, katika Mswada huu kuna kipengele kinachosema kwamba kura itapigwa dhidi ya wajumbe ikiwa watashindwa na kazi. Hiyo inafaa na ni vizuri. Pia asilimia fulani ya kura inatakikana ili kupitishia Mswada Bungeni. Ningependekeza iwe thuluthi mbili na sio thuluthi moja, ili kuwe na uongozi wa kufaa. view
  • 16 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, kusema kuna sub-counties ambazo zitakuwa zinalingana na constituencies--- Kuweka tena sub-counties ni kuleta matatizo mengine. Hii ni kwa sababu constituency iko na Mbunge. Ukiongeza muwakilishi wa sub-county, ataleta matatizo. Hii ni kwa sababu sub-county yenyewe itakuwa na jopo lake na Mbunge pia atakuwa pale. Kwa hivyo, hii italeta matatizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine linaloandamana na hilo ni kwamba itakuwa na vigumu sana kupata pesa na kufanya kazi, kwa sababu ya majopo yatakayoundwa. Zile tume na kamati ambazo zitakuwa ni karibu kumi. Je, hizi kumi zitakuwa zikifanya kazi gani kutoka pembe moja hadi ... view
  • 16 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, tatizo lingine ni kwamba serikali za kaunti hazijawekewa vipimo vya matumizi. Kwa mfano, haijabainishwa gavana katika kila kaunti atakuwa na gari moja ama magari mawili. Labda hilo ni jambo ambalo litafanyika baadaye. Shida ni kwamba iwapo hali hiyo haitashughulikiwa hivi sasa, magavana watajipatia madaraka watakayotaka. Utaona gavana akitaka kununuliwa Range-Rover yenye thamani ya Kshs 20 million, na kama magari saba hivi ya kumfuata nyuma kwenye misafara yake. Atataka naibu wa gavana pia awe na magari kama hayo kwa sababu hakuna kiwango cha matumizi ya pesa kilichowekwa. Watatumia pesa bila kujali na kuziweka kaunti kwenye shida. ... view
  • 16 Feb 2012 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, iwapo magavana watapigiwa kura, tutapata magavana ambao wakichaguliwa tu wataanza kutumia vibaya fedha za umma na kuanza kutafuta njia za kuwa rais. Kaunti hazitafanya kazi. Tunataka ikiwezekana watu hao wachunguzwe na kufanyiwa mtihani wa kufuzu kuwa magavana, lakini wasipigiwe kura. Haya maneno ninayosema leo katika Bunge yatakumbukwa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus