26 Oct 2011 in National Assembly:
Hawa wananchi wa Juja ni chanzo tu cha matatizo yanayowakumba Wakenya. Ukienda kwa kila mji, utaona kwamba wananchi wanaajiriwa kwa kazi ya kibarua. Hata kampuni za kibinafsi zimepenya katika Wizara na kuwajiri watu wao kusimamia dhuluma kwa Wakenya. Mwananchi wa kawaida akienda kudai haki yake kwa shirika la kibinafsi, anaambiwa aende ofisi ya wafanyikazi. Akienda ofisi ya wafanyikazi, anakuta yule mtu ambaye amewekwa huko anapata mshahara na anarudia kwa mlango na hawezi kupata haki yake. Ukiingia katika kila sehemu ya uakilishi Bunge, utaona kuwa wananchi wako na matatizo hayo.
view
26 Oct 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, hawa wananchi wanastahili kulipwa haki yao na Waziri ambaye atajibu mambo haya kwa niaba ya Serikali yuko hapa. Hatutategemea kuambiwa kwamba haya matatizo yamesikizwa na yataangaliwa. Tunaweza kuambiwa kuwa hawa wananchi watalipwa pesa hizi. Kama Bunge hili haliwezi kutoa kauli mwananchi alipwe pesa zake, basi, tunataka Bunge lingine ambalo litatengeneza sheria na kutoa maamuzi ambayo yatatimizwa. Mimi sitakubali kukaa kwenye Bunge ambalo linatoa maamuzi ambayo hayatimizwi.
view
26 Oct 2011 in National Assembly:
Nimekaa hapa kutoka asubuhi ili nizungumze kuhusu jambo hili na wananchi taifa nzima wanisikie. Kwa hivyo, ningependa kuona matokeo. Hatutakubali mambo haya kamwe. Kama ni kulipwa, walipwe na wale wengine ambao wanadai, vile vile, walipwe. Waziri wa Kazi na Mawaziri wengine ambao wanahusika wajue kwamba viti ambavyo wanakalia si vya maridadi tu. Sio viti vya bendera, gari na ofisi tu, ila mwananchi wa Kenya anataka kupata huduma kutoka kwa Wizara hizo. Moja ya utumishi huu ni kuondoa dhuluma. Bw. Naibu Spika wa Muda, Ripoti hii inaendelea kusema kwamba Karani wa Mji apelekwe kortini na kushtakiwa. Ikiwa mtu ambaye amesoma na ...
view
12 Oct 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Hoja hii imezua maswala mengi ambayo yanaweza kuleta majonzi kwa wananchi wetu. Ninakumbuka nilisimama hapa na kupinga uteuzi wa Bw. Kosgei kama mkurugenzi wa shirika hili. Hii ni kwa sababu katika mahojiano, yeye alikuwa wa nne. Bw. Abdi ndiye alikuwa wa kwanza na kufuatiwa na Bi. Eva Owuor. Kulikuwa na mwingine aliyekuwa wa tatu. Je, ni kwa nini Abdi hakuteuliwa kama mkurugenzi wa shirika hili? Je, alikataa kuteuliwa kwa sababu ya kabila lake au hakuwa na uhusiano wowote na wakubwa wa Wizara hii? Je, huyu ...
view
12 Oct 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nimerudi kutoka Uganda. Nimesoma magazeti. Kumekuwa na wizi wa pesa kupitia mambo ya mafuta yaliyotokea huko Uganda. Lakini waliowekwa ndani ni wale waliohusika, na huwezi kusikia kabila hili likisema mtu wetu ndio amechukuliwa na mtu wa kabila fulani, au mtu wetu anaonewa.
view
12 Oct 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, mimi kuitwa Otieno haimaanishi kwamba akina Otieno wote ni wezi. Mimi kuitwa Mutua ama Mutiso, haimaanishi kwamba watu wote wanaoitwa hivyo ni wezi. Lakini leo kashfa ya wizi katika ofisi za Serikali yetu, kuanzia polisi mpaka kila kitengo unakuta kwamba huyu ameiba na bado yuko serikalini. Huyu ametajwa bado yuko Serikali. Haya yametokea bado yuko serikalini. Sasa unashindwa askari ni nani na mkurugenzi ni nani. Wizi ukitokea tu tunaambiwa ni mtu wetu.
view
12 Oct 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, kama ni kweli mimi namwomba Mungu mwenyezi kuweka hukumu yake inavyowezekana. Kshs16 milioni inatumika kumtafuta mkurugenzi mmoja, na si wawili. Katika Kshs16 milioni, Kshs15 milioni zimeenda kwa wale ambao wanapata chakula ambacho hawalipii. Juzi nilienda Laisamis kwa Mhe Lekuton; nasema hapa kama thibitisho kwamba kama leo kuna watu wanataka kuona Serikali na macho, na wanahitaji kujua kwamba Kenya ni Kenya, mimi nilienda Laisamis na shida za eneo Bunge ninalowakilisha zikaisha.
view
12 Oct 2011 in National Assembly:
Leo tuna simu na unaiweka mfukoni na unaweza kuongea hata ukiwa kwa ndege. Nakuambia leo kati ya koo pale Laisamis watu 40,000 hawajahi kupiga simu hata siku moja. Hakuna nework! Kutoka pale mpaka Isiolo, hao watu pahali wananunua nyanya na kitunguu ya kupikia chakula, ni kilomita 170. Hiyo ndio soko. Wezi hapa wanachukua Kshs15 milioni na kuigawa ikiwa juu ya meza kwa madai kuwa wanatafuta mkurugenzi mmoja wa kampuni, na hali watu kama wale wa Laisamis hawana maji au hospitali. Nakuambia kitu kinachoitwa dispensary hamna katika hiyo sehemu. Mhe Lekuton anawakilisha sehemu ambayo ukubwa wake ni kilomita 24,000 mraba. Akitoka ...
view
12 Oct 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kumalizia nikiwa na machungu sana katika moyo wangu. Ningependa kusema kwamba Kamati hii imeweza kutoa mwelekeo ambao ukifuatwa, utakuwa ni funzo kwa wale wanaofanya mambo kama haya. Ile Bodi yenyewe inafaa kuthibitisha ilitumia Kshs15 milioni kununua nini na walikuwa wanaajiri watu wangapi. Kazi yao ilikuwa ni nini ili watumie Kshs15 milioni. Kama ni mwanzo wa mambo, wahusika wanafaa kurudisha pesa hizo ndipo mambo haya yakome. Itakuwa ni vigumu sana mimi mwenyewe kupanga kuiba. Kama Whip katika ofisi hii, nikienda kwa ofisi za makarani na kuwaambia kwamba nataka waniwekee hizi pesa, nikitoka haiwezekani kwamba yule ...
view
12 Oct 2011 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, namaliza kwa kutoka shukurani zangu kwa Kamati iliofanya kazi hii na kuunga mkono Hoja hii.
view