Johnson Nduya Muthama

Born

20th October 1954

Post

Parliament Building, P. O. Box 41842-00100 Nairobi

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

info@jnmholdings.co.ke.

Telephone

0733900300

All parliamentary appearances

Entries 801 to 810 of 1060.

  • 10 May 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa wale waliozungumza hapa na kuweka mipaka, wakisema kwamba tunazungumzia kabila fulani, ambako mauaji yalitokea, ningependa kusema kwamba sio watu walioko vijijini pekee wanaopoteza maisha yao. Hata Wabunge wanauawa kiholela. Wafanyikazi wa Serikali wanauawa kiholela. Wengine wanauawa wakiwa na walinzi wao. Maafisa wa polisi wenyewe wako hatarini ya kuuawa. Kwa hivyo, suala la mauaji na watu kuviziwa katika nchi siyo suala la Waziri peke yake, bali ni suala linaloihusu nchi nzima. Kama tunataka kuweka ulinzi katika taifa letu, ni lazima tuache kugombana kwa misingi ya kikabila na tuache kusema kwamba watu wa kabila fulani hawalindwi. ... view
  • 10 May 2011 in National Assembly: Hiyo ndiyo njia ya kidiplomasia tunayofaa kutumia kuzungumzia suala hili, na tutaheshimiwa. Hatutaki kuonekana na mataifa mageni kwamba tunaamka asubuhi na kutoa maneno ya dharau, tukionyesha kwamba tunaweza kupigana na mtu fulani. Anayechukua sheria mikononi na kupigana na jirani yake hatii hata sheria za Mwenyezi Mungu, bali anatumia uwezo wake mwenyewe na kuwadharau wanyonge. Kwa hivyo, tuchunge sana. Sisi tunatazamiwa kuiunganisha Afrika nzima, na ni lazima tusimame kwenye nafasi yetu. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii. view
  • 5 May 2011 in National Assembly: Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir, the Minister has given us quantities of fuel, which are in stock. My first question is whether he could say for how many days the current stocks that are being held by the KPC will last. Secondly, I would like him to confirm whether they expect any consignment of oil, having said that they are able to float only one consignment of oil at any given time. Lastly, I want him to confirm whether he is truly in firm control of the private businesses being operated by oil dealers. Is he able to impose prices ... view
  • 26 Apr 2011 in National Assembly: On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. Is it in order for the Member to keep on saying that the report was adopted when Kenyans are listening? It is very clear that the report came here, it was pushed back and that is why the new Commission is coming in to deal with this. view
  • 21 Apr 2011 in National Assembly: On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. view
  • 21 Apr 2011 in National Assembly: Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir, I would like to ask the Assistant Minister if he could be kind enough to consider awarding the sportsmen and sportswomen of this country, not only the present ones but even those who performed better in the past. There is only one club in this country that has ever won a football championship in Africa. It is not our national team but it is a club known as Gor Mahia. When this club won this cup, things went quiet and up to date, there is no other team that has managed to win a regional ... view
  • 12 Apr 2011 in National Assembly: Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ninashukuru kwa nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii ambayo ni ya maana sana. view
  • 12 Apr 2011 in National Assembly: Ningependa kushukuru Kamati ya mhe. Rege na Waziri kwa kukutana na kuongea mambo muhimu sana. Haya ni maswala makubwa yanayohusu nchi yetu. Wizara ya Kawi inategemewa sana na wananchi wa Kenya kwa mambo mengi. Vile vile, ningependa kumshukuru Waziri kwa kazi na bidii yake ya kusambaza umeme katika nchi yetu ya Kenya na kuhakikisha kwamba kila pembe ya nchi inapata umeme. view
  • 12 Apr 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, kama vile wenzangu waliozungumza mbele yangu wamesema, ingawa pesa zilizotakikana zilipitishwa na mamlaka ya Waziri yemepeanwa kuhusu mafuta yakiwemo ya taa--- Mafuta ya magari ni petroli na diseli na hayana shida sana. Ni jukumu la Waziri kuona kwamba sisi tumehifadhi mafuta ya kutosheleza mahitaji yetu. Pia, inafaa alinde kampuni za hapa nchini zisivurugwe na kampuni za kutoka nje. Kama Shirika letu halitapewa pesa za kutosha ili liagize mafuta, bila shaka tunaweza kudhulumiwa na kampuni za hapa nchini hazitafanya kazi. view
  • 12 Apr 2011 in National Assembly: Wenzangu wamezungumzia kuhusu mafuta ya taa. Ninawaunga mkono kwa kusema kwamba wengi wa watu wanaotupigia kura au wengi wa watu tunaowaongoza – bali na kumshukuru Waziri kwa kusambaza stima - wanategemea mafuta ya taa. Mafuta ya taa ni muhimu sana. Mbali na kuwemo kwa soko huru katika kila sekta ya nchi hii, kuna sekta zingine zinazomhusisha mwananchi wa kawaida moja kwa moja. Mafuta ya taa ni bidhaa moja ambayo inamhusu mwananchi wa kawaida. Ningemwomba Waziri afanye vyovyote iwezekanavyo, hata kama ni kuleta Hoja hapa Bungeni, ailete na tuipitishe ili bei ya mafuta ithibitiwe na Wizara ya Kawi. Kati ya asilimia ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus