Johnson Nduya Muthama

Born

20th October 1954

Post

Parliament Building, P. O. Box 41842-00100 Nairobi

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

info@jnmholdings.co.ke.

Telephone

0733900300

All parliamentary appearances

Entries 811 to 820 of 1060.

  • 12 Apr 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, vile vile, ningependa kumshukuru Waziri kwa kumteua Mkurugenzi wa National Oil Corporation of Kenya (NOCK). Kulikuwa na mtafaruku kuhusu uteuzi huo na Waziri amechukua hatua hiyo na sasa hivi tuna Mkurugenzi katika Shirika la NOCK. Wizara ya Kawi inatakikana ihakikishe kwamba inasaidia miradi ya stima katika kila sehemu ya uwakilishi bunge kwa sababu ina uwezo wa kufanya hivyo. Kama ni mambo ya elimu, inafaa yasiachiwe Wizara ya Elimu pekee. KenGen inapata pesa nyingi kutoka kwa wananchi. Kwa hivyo, shirika hili linaweza kujenga vyuo, vituo vya matibabu au shule hata kama ni ya nasari. view
  • 12 Apr 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii. view
  • 12 Apr 2011 in National Assembly: On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. Is the hon. Member in order to continue misleading the House when we know the report which was tabled here by the Chairman of Energy, Communication and Information showed that NOCK had capacity to import 30 per cent of the fuel if they were provided with funds? view
  • 2 Mar 2011 in National Assembly: Ninakushukuru Naibu Spika wa Muda kwa nafasi hii. Nanajua tunapochangia Hoja hii ya kwenda likizo, wananchi katika Taifa nzima wametega masikio katika vyombo vya habari kusikia tunagusia nini. Ningependa kugusia wakimbizi wa kisiasa katika nchi yetu, ama wale tunawaita IDPs. Tunapofunga safari na kwenda nyumbani; tumeamka kwenye nyumba zetu na tutaenda katika nyumba zetu. Lakini kuna Wakenya, ambao ni akina mama, watoto na wanaume, walio katika barabara; wanalala katika viwanja. Swali ninalogusia mimi mwenyewe kila mara ninapotembea, na ninaposikiliza vyombo vya habari, ninasikia kwamba kuna Wakenya ambao wanataabika; ninasimama na kujiuliza swali, je tuko Kenya huru ama Kenya ya kikoloni? ... view
  • 2 Mar 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, hali hii inahusu korti ya kimataifa kwa sababu hiki ndicho chanzo cha yale mambo ambayo tunaongea hapa. Na karibu igawanye nchi nzima. Haya yote yamefanyika tukiwa hapa. Ni dhahiri kwamba, wale wliohusika na mauaji ya halaiki ya wakenya hawajaguzwa. Walioongoza na kuchochea na kusema kwamba wananchi waende wapigane, hawako katika ile orodha inayotajwa hapa ya wale wanaotakiwa kuenda katika korti ya kimataifa. Ni dhahiri tuseme kwamba sheria ya nchi hii inafaa impate aliye mkubwa na aliye mdogo. Ikiwa wakubwa watakuwa wanakosa na kubaki huru na kuongea mambo ya uchochezi, haitawezekana kamwe kwani sheria ni ya kila mtu ... view
  • 2 Mar 2011 in National Assembly: Mambo ya magendo na ulaji rushwa yametajwa hapa. Ukiangalia katika mgao wetu wa Serikali, walioko katika PNU hawataki kutaja magendo yaliyoko upande wao na vile vile walioko katika ODM wanajitetea kivyao. Kwa hivyo, tuwache mambo ya kujivuna hapa. Kama ni uwazi wa kupigana na kasumba ya rushwa, isiwe ni mambo ya baba na mtoto na dada na kabila la mtu. Inafaa kila mhusika abebe mzigo wake mwenyewe, aende mahakamani na kushtakiwa. Haifai kuongea juu ya ufisadi mmoja tu kama ule wa hoteli ya Grand Regency. Je mahindi yetu yalienda wapi? Tunajua ni pesa ngapi nchi hii imepoteza na walioiba wanatumia ... view
  • 2 Mar 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, ni lazima tuchunge matamshi ya viongozi. Inafaa tunapotoka hapa, twende kule nje na kuunganisha taifa letu. Kiongozi anaposimama na kusema kwamba: “Punda amechoka, na barabara ni ya Misri”, anamaanisha nini? Hili ni taifa la Kenya na wala sio Misri. Sisi tuna mtindo wetu wa kufanya mambo. Sisi sio wamisri. Kama kuna mtu wa kuchochea vuguvugu, inafaa aende akafanyie hio vuguvugu nyumbani kwake kwa sababu ana watoto wake kule nyumbani. view
  • 2 Mar 2011 in National Assembly: Ninaunga mkono. view
  • 1 Mar 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika, mbali na kuwa kuna uhuru wa kuvaa, kulingana na mtindo wa Kiafrika na hasa Sheria za Bunge, siwezi kuja hapa kama nimevalia skati, lakini mwanamke anaweza kuvalia suruali ndefu. Kwa hivyo mwanamme yeyote kuvalia vipuli sio tabia nzuri. Tukiyaruhusu mambo haya hapa na kule nyumbani wale waliotuchagua wanatarajia tuwe viongozi wenye hekima na heshima, tutakuwa tukiwahangaisha wananchi. Kwa hivyo, haifai hata kama sio leo kwamba katika siku zijazo wanaume wavalie sindilia au vitambaa vichwani na kuja navyo Bungeni ati kwa sababu ni mavazi. Mtindo wa mavazi na heshima ya Bunge ni lazima vizingatiwe. Kwa hivyo, kuvalia vile ... view
  • 23 Feb 2011 in National Assembly: Madam Temporary Deputy Speaker, there is no time to say anything now. I suggest that we adjourn and then we continue--- view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus