Johnson Nduya Muthama

Born

20th October 1954

Post

Parliament Building, P. O. Box 41842-00100 Nairobi

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

info@jnmholdings.co.ke.

Telephone

0733900300

All parliamentary appearances

Entries 791 to 800 of 1060.

  • 25 May 2011 in National Assembly: Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nitaongea kwa dakika tano ili tutumie dakika kumi na tano. view
  • 25 May 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, inafaa Waziri afahamu kwamba Wakenya wanahitaji majengo mazuri na imekuwa kikwazo kikubwa sana kuweza kufanya ujenzi huo. Kikwazo kikubwa sana ni bei ya vifaa vya ujenzi. Ningependa Waziri aangalie sana bei ya simiti. Mfuko mmoja wa simiti sasa ni zaidi ya Kshs800 ilhali simiti kutoka Misri inaweza kupatikana kwa Dola Mbili au Kshs150. Hatujui ni kwa nini bei ni ghali hapa kwetu. Majengo ya kiajabu yametapakaa nchini kwa sababu wananchi hawawezi kujimudu. Jambo la pili ni kwamba wananchi wa nchi hii wametengwa katika kupata kandarasi za kufanya kazi. Utapata kijana ambaye amesoma na kuhitimu na ... view
  • 25 May 2011 in National Assembly: Jambo la tatu ni kwamba tunataka vijana wetu waliosoma watumiwe kuangalia ndugu zetu ambao wanaanzisha majengo yao bila ujuzi. Kuna wahandisi ambao wanaweza kwenda na kuwakashifu wanaofanya kazi duni. Kwa hivyo ikiwa tumewasomesha watoto wetu na wameajiriwa na Wizara, tunataka watembee wakitoa huduma zao na wasingojee majengo yajengwe halafu yaporomoke na kuanza kuwalaumu waliojenga na kuwaambia kwamba hawana ujuzi wa kutosha. Tunalipa karo kuwasomesha watoto wetu ili wasaidie nchi. view
  • 25 May 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo la nne ni kwamba katika Schedule ya Pili, kuna maneno ambayo hayaelezi sawa sawa hali ya mikutano ya halmashauri hii. Wanaposema kwamba inatakiwa mikutano minne katika mwaka na kila miezi mbili kuwe na thibitisho kwamba mkutano umefanyika. Hii inamaanisha mikutano sita. Jambo hili linaweza kuleta mtafaruku katika mpangilio wa mambo haya. Tunafaa kuhakikisha kwamba vyombo na vitu vinavyotengenezwa hapa nchini vinauzwa kwa bei ya kuwasaidia wananchi. view
  • 25 May 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache ninaunga mkono. view
  • 18 May 2011 in National Assembly: Asante, Bw. Spika. Kulingana na arifa ya Waziri Mkuu katika Bunge hili ni kuwa alipofika pale mpakani, aliwaona wavamizi wakitayarisha mashamba kwa minajili ya kulima na kupanda. Je, wavamizi hao bado wana endelea na shughuli zao za kulima na kupanda au wametimuliwa? Ikiwa Serikali haijafaulu kuwaondoa mahali hapo, itafanya nini? Ni lini wavamizi hawa wataondolewa kutoka nchi ya Kenya? Je, usalama wa taifa letu ni shwari? view
  • 18 May 2011 in National Assembly: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. I do not think the Prime Minister got my question clearly. My question was: If, truly, we found those invaders planning to plant in Kenya, when is the Government going to take steps to remove them and stop them from farming in Kenya? So, the question is about what the Government is currently doing about the situation. view
  • 11 May 2011 in National Assembly: Thank you, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. I want to make very brief remarks. First of all, I want to congratulate the Minister for demonstrating very clearly that we can have hardworking Ministers. The Minister is focused and he has tried to see the implementation process of the new Constitution going through. Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir, I want to just pinpoint a few issues here. (a) The Independent Electoral and Boundaries Commission that is coming into place should not mess up with things by misusing its independence. In 1992, 1997, 2002 and 2007, there were problems with elections results. ... view
  • 10 May 2011 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru kwa kunipa nafasi ili niichangie Hoja hii ya maana sana, inayohusu Wakenya waliopoteza maisha yao. Nikimshukuru mhe. Wamalwa kwa kuileta Hoja hii, ningependa kuwasihi Wabunge wenzangu tuzungumzie masuala ya taifa la Kenya, na tusitaje kabila hili ama view
  • 10 May 2011 in National Assembly: ile. Wakati mwananchi wa Kenya anapopoteza maisha yake, awe ni wa kabila moja ama ingine, taifa nzima la Kenya linahusika. Katika nyakati kama hizo, tunastahili kuungana na kuzungumzia maisha ya Wakenya. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo la pili ni kwamba ni lazima tuielewe nchi yetu na nchi yetu ituelewe vilivyo, tukifahamu kwamba tumezingirwa na mataifa ambayo wakati mwingine, na kwa sababu fulani, hawana imani ama upendo na nchi yetu ya Kenya. Tumeweza kuhusika kwenye masuala ya mauaji ya Wakenya. Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani yuko hapa. Ni vigumu sana kujua mtu anayekuvizia atashambulia boma lako ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus