11 Nov 2009 in National Assembly:
The other issue is on our ability to deal with issues. When we talk about foreigners coming here to help us achieve peace because we are fighting one another and people are being displaced, we do not command any respect outside. So, we need to work on issues that will earn us respect. If you look back, you will see that there was violence in this country in 1992. Kenyans were killed and many others displaced. A commission of Inquiry was appointed, led by Mr. Kiliku. A report was written and recommendations made but no action was taken. Kenya cannot ...
view
11 Nov 2009 in National Assembly:
Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii inayohusu wakongwe na wazee wa nchi hii. Nataka kumshukuru Waziri na Wizara yake kwa mambo muhimu sana walioweza kuyajadili na kuyaleta mbele ya Bunge hili ili yaweze kuungwa mkono, huku tukizingatia na kufahamu kwamba wazee wameteseka sana katika nchi yetu. Nchi zingine duniani haswa zile ambazo zimeendelea, zimeweka mikakati ya kuwasaidia wakongwe. Wahenga walisema kwamba palipo wazee hapaharibiki jambo. Kwa hivyo, tunastahili kuwalinda wazee wetu kwa kuwafanyia mambo yanayofaa. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninataka kumuuliza Waziri kwa unyenyekevu, aangalie zaidi pesa anazotoa; Kshs1,500. Ikiwa Serikali italipa watu ...
view
2 Sep 2009 in National Assembly:
Ahsante sana Bw. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Kati ya waliozungumza mbele yangu, hakuna aliyesema kwamba uteuzi wa Jaji Ringera unafaa. Hata hivyo, jambo muhimu ni kwamba Hoja iliyo mbele yetu inahusu likizo yetu baada ya kuketi hapa Bungeni kwa muda wa siku kadhaa. Sasa, tunatakiwa kuchukua likizo twende nyumbani ili tuweze kuwatumikia wananchi.
view
2 Sep 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu wa Spika, nimesema kwamba hata tukipitisha kura ya kutokuwa na imani leo, au jana, bado itakuwa tumepitisha tu hiyo kura. Ninasema kwamba tuchukue likizo twende tukawafanyie kazi watu waliotuchagua, na tuangalie shida zao. Tumezungumza hapa. Sasa ni wakati wa kwenda mashinani na kuwafanyia wanachi kazi. Tukirudi hapa, tulete Hoja ya kutokuwa ba imani na Bw. Ringera, tuichangie na kuipitisha.
view
2 Sep 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu wa Spika, hata hivyo, kazi ya Bw. Ringera imewekewa vikwazo na viongozi wenyewe. Hakuna mwizi anayekamatwa katika nchi hii ukose kuona wawakilishi wa watu katika Bunge hili katika stesheni za polisi wakijaribu kumtoa. Kama hawamtoi mwizi kupitia muungano wa kisiasa, wanamtoa kupitia misingi ya kikabila, wakisema: âHuyu ni mtu wetu. Hapaswi kulaumiwa.â
view
2 Sep 2009 in National Assembly:
Kama Bw. Ringera angekuwa anafanya kazi katika nchi ambayo inampa uhuru wa kufanya hivyo, na viongozi wanaoamini kwamba wezi ni lazima wakamatwe, hangekuwa na shida. Lakini mwizi akimatwa, viongozi fulani husema: âTunatoa mwito Kamishna wa Polisi afutwe na waliokuweko mbeleni wafutwe.â Hii ni kwa sababu sisi wenyewe hatutaki kutii sheria lakini tunataka kumuandama mtu mmoja kwa misingi ya kikabila.
view
2 Sep 2009 in National Assembly:
Ni wezi wangapi walioko katika Serikali na ambao hawajazungumziwa? Haifai kuleta jina la Mkenya hapa na kulikandakanda kwa maneno machafu kwa sababu amepata nafasi ya ajira. Kama ni hivyo, tuangalie nyuma na kuwatoa wezi wote Serikalini kwa sababu tunawafahamu, na wako kwenye madaraka. Waliotoka wameiba na mali yao inajulikana. Wanatembea nayo na hakuna mtu anayewahusisha na uhalifu. Leo hii, hakuna mtu anayetaka kubanduka kutoka kwa Msitu wa Mau. Tumeweka siasa za kikabila na kila kitu.
view
2 Sep 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu wa Spika, nchi hii haina sheria ya mnyonge. Bw. Ringera hawezi kuja hapa kujitetea. Wale wanaopinga uteuzi wake zaidi, wakipewa nafasi hiyo, watatumikia na kusema: âHewala!â Tuchukueni likizo twende nyumbani.
view
2 Sep 2009 in National Assembly:
Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii kwa nguvu zangu zote.
view
2 Sep 2009 in National Assembly:
Madam Temporary Deputy Speaker, I wish to thank you for giving me the opportunity to support this very important Motion that has been brought by hon. Kaino. Madam Temporary Deputy Speaker, it is extremely important to recognize that this country has suffered since the time we attained Independence. I do remember that when I was a young boy, immediately after Independence, Kenya was given food by the late President J.F. Kennedy. We have continued on the same pace since that time up to today. The planning by the Government has been extremely wrong. After 46 years since Independence, we are ...
view