22 Apr 2014 in National Assembly:
Thank you hon. Speaker. Two months ago I read a Petition on behalf of the tea farmers in South Imenti Constituency and by extension the whole country because right now tea farmers have missed out on mini bonuses. I want him to be here so that---
view
22 Apr 2014 in National Assembly:
From the Departmental Committee on Agriculture, Livestock and Cooperatives.
view
3 Apr 2014 in National Assembly:
Thank you, hon. Deputy Speaker. I have observed in my constituency that poor students continue to miss out from that education fund. I do not know the criteria HELB uses to identify the poor students---
view
3 Apr 2014 in National Assembly:
There is the issue of poor and deserving students missing out. We still have students from rich backgrounds getting that facility.
view
3 Apr 2014 in National Assembly:
Thank you, hon. Deputy Speaker. The low price of the Macadamia nut is as a result of the ban that was imposed on that important crop. My concern is whether the Ministry is considering lifting the ban so that farmers can fetch better prices and eradicate the cartels that are in the industry.
view
3 Apr 2014 in National Assembly:
Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Kwanza kabisa nampongeza Rais wetu kwa hiyo Hotuba yake ambayo alileta hapa Bungeni; nampongeza kwa kutilia maanani maadili ya Katiba yetu mpya. Pia nampongeza kiongozi wa CORD, Raila Odinga akiwa Marekani. Akihojiwa na waandishi wa habari aliweza kuipongeza Serikali na kuipa alama tano ambayo ni pass na akasema kweli Serikali ya Jubilee imefanya kazi nzuri katika mwaka mmoja. Kwa hivyo, kwa wale ambao labda hawakusikia hio ripoti ya kiongozi mashuhuri Raila Odinga, labda hawasomi---
view
3 Apr 2014 in National Assembly:
Hapana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Mimi sijasema nilisoma kwa magazeti. Nimesema alisema akiwa Marekani. Kwa hivyo, mwenzangu, Mhe Millie, hajui kama hata mimi nina uwezo wa kuongea na Bw. Raila Odinga. Sijui kwa nini anashuku taarifa yangu hapa Bungeni.
view
3 Apr 2014 in National Assembly:
Kwa hivyo, nikiendelea nilikuwa nasema kwamba labda wale wenzangu wa CORD wananishuku. Ninazungumza kwa Kiswahili ndio kila mtu hata mama mboga asikie vile ninasema saa hii. Nasema labda kuna wale wanashuku Serikali haijafanya kazi yoyote. Kama kiongozi anasema hivyo, mbona tunashuku? Nitaendelea kusema kwamba miundo mbinu msingi ndio itasaidia nchi yetu; tumeona Rais amesema kwamba reli kutoka Mombasa mpaka Nairobi baadaye itaenda Malaba.
view
3 Apr 2014 in National Assembly:
Niongezee dakika mbili!
view
3 Apr 2014 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nasema labda Mhe. Ngong’o hana laini nzuri ya kufikia mkubwa wake; kwa hivyo nitaendelea kusema kwamba kile kitu Rais aligusia, na naona kitasaidia Kenya, ni wajibu wa kuhakikisha kwamba wawindaji haramu wamekamatwa na kufungwa. Leo tukizungumza kila mtu anaelewa kwamba wawindaji haramu wameuwa ndovu wetu na vifaru. Kwa hivyo, kulingana na zile sera Serikali imeweka sina wasiwasi kabisa kwamba tutaweza kukamata wale wakora na wale watu ambao wanaharibu nchi yetu. La mwisho ni kwamba ile asilimia 30 ambayo imepewa vijana, akina mama na walemavu, kuna sheria nyingi zimewekwa na Wizara ya Ugatuzi na Mipango. Kwa ...
view