Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.
26 Oct 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika. Nami pia ningependa kuunga mkono wenzangu wengi ambao wameongea kuhusu Mswada huu. Kutoka mwanzo, mimi niko hapa kupinga vikali sana Mswada huu ambao umeletwa na Mhe. Chepkong’a. Napinga Mswada huu kwa sababu umeletwa eti utekeleze matakwa ya Katiba. Wakati Katiba ilikuwa ikitengezwa, maoni yalitolewa na Wakenya wengi. Kwa wakati huo, tulisema kuwa “Wanjiku, Kadzo, Anyango, Chebet, Kibet na Onyango wameongea. Haikuwa ni maneno ya Wabunge zaidi ya 300 ambao tuko katika Bunge hili la taifa. Wakenya walifikiria kuwa hapo awali kulikuwa na dhuluma za kihistoria katika mambo ya uongozi. Tunajua akina mama wamenyanyaswa kwa misingi ya ...
view
26 Oct 2016 in National Assembly:
na pengine kumstarehesha mzee. Kweli, tunakubali kwamba kuna zile kazi ambazo ni mwafaka kwa kina mama kuzifanya. Lakini wakati huu, nchi yetu, katika Riwaza 2030, ilizungumzia kuwa akina mama ni lazima wajenge uwezo kisiasa, kijamii na pia kiuchumi. Iwapo tutapitisha Mswada ambao unasema eti tutatekeleza sheria hii ya Katiba pole pole, pasina kutueleza kinaga ubaga njia mwafaka itakayotumika, watueleze ni kwa muda gani tutatekeleza na ni idadi ya asimilia ngapi ambayo itaweza kuwekwa kuhakikisha kwamba zaidi ya thuluthi mbili haitakuwa ya jinsia moja. Tunawapenda sana ndugu zangu Wabunge wanaume. Nataka niwaambie kwamba Mswada huu ni wa akina mama. Ni Mswada ...
view
26 Oct 2016 in National Assembly:
, yatafikia uongozi na kuwa sawa na zile jinsia zote. Iwapo sisi ni wakweli kama watunzi wa sheria katika Jamhuri yetu ya Kenya, lazima tuweke sheria za ukweli. Tusiweke sheria tu ati kwa sababu tumesikia Bunge litavunjwa iwapo hatutaweka sheria hii. Mahakama Kuu, tunayoiita kwa Kiingereza Supreme Court, ilitupatia mawaidha na kusema tutengeneze sheria mwafaka itakayotupatia njia sahihi ya kueleweka na kuhakikisha kwamba sheria ambayo iko katika Sura 81 imetekelezwa. Kwa hivyo, tukisema tunapitisha Mswada huu, bado hatujafanya jambo lolote. Bado tutarudi nyumbani hivyo hivyo. Sasa tunasikia kuwa kuna kesi. Kama tutaendelea kwenda hivi, basi sisi tutakuwa mashakani sana kuweza ...
view
26 Oct 2016 in National Assembly:
Ndugu yangu Mheshimwa ananikumbusha kuwa nyege ni kunyegezana. Kunyegezana lazima kuwe na mume na mke. Hakuwezi kuwa na jinsia moja. Kwa hivyo, lazima tujue ya kwamba hizi sheria tunazileta kwa sababu tunataka kesho wale akina mama ambao watakuwa wamejengwa uwezo kwa kupitia sheria hii wawe na nguvu na tajiriba ili waweze kushindana na akina baba, tuwe tuko sawasawa. Ni aibu sana tukiangalia nchi jirani kama Rwanda, Uganda na Tanzania. Akina mama wamejengwa uwezo na wameingia katika viti vile vya kuweka maamuzi katika taasisi za umma katika nchi zao. Sisi Wakenya ambao tumebobea, tukienda Tanzania tunaambiwa kuwa tuko juu lakini, tunataka ...
view
26 Oct 2016 in National Assembly:
hatuelewi zitatekeleza vipi sheria ambazo zimezungumziwa katika sheria mama inayoitwa Katiba? Lazima tuangalie kule tunakotoka na kule tunakoenda. Leo hii tukisema hatutaweza kutekeleza sheria hii, kesho kutwa tutakuwa na Bunge ambalo lina akina mama kumi. Itakuwa ni aibu na fedheha. Lazima pia tuwe tunazingatia nyanja hizo. Leo wewe kama Mbunge mwanaume pengine umejaaliwa watoto wa kike pekee, lazima upitishe sheria ambazo haswa zinamlenga mtoto wa kike. Ijapokuwa ni jinsia, ukweli ni kwamba mama alikuwa amegandamizwa kihistoria, kidesturi, kimila na pia katika mambo ya kupigwa na mambo ya kiuchumi. Tulikuwa tumegandamizwa sana. Hatusemi kuwa sisi tunaomba lakini tunataka tuiweke Kenya yetu ...
view
26 Oct 2016 in National Assembly:
Maanake akina mama watajua kwamba unasimama kidete kuangalia haki zao. Na hata sisi manyumbani tutajua lazima ile haki nyingine tuifanye kwa njia sambamba kwa sababu wametupatia nguvu sana.
view
26 Oct 2016 in National Assembly:
Akina mama tumejaribu sana. Dada yangu Rose Nyamunga amesema kuwa tuliwanunulia dinner . Lakini sisi hatutaki kuwadai. Ile ilikuwa ni mapenzi yetu. Natutaendelea kufanya mengi mazuri ili sisi tuwe kitu kimoja, tuwe na upendo na mapenzi jamani. Wenzetu hapa Tanzania, Makamu wa Rais wao ni mama. Hiyo ndiyo njia ambayo sisi tunastahili kuendelea nayo. Lakini hivi hivi bila kuwajenga kiuwezo akina mama, hatutafikia pale. Na kama tunataka kutajika katika ulimwengu kwa mambo ya uongozi, lazima tuhakikishe akina mama wako mbele, tumewasaidia na wamepata haki yao. Natukifanya hivyo, basi Kenya itakuwa miongoni mwa inchi ambazo zimestawi na kubobea kiuchumi, mambo ya ...
view
26 Oct 2016 in National Assembly:
Kwa hayo mengi ama machache, naomba jamani mtuunge mkono hata mkibadilisha na kuweka hicho kilma ‘ progressive ’. Lakini kama hamutaweza kugeuza kile Kipengele cha 97 ambacho kinazungumzia muundo wa Bunge utakuwa na akina nani, ikiwa hamutakuwa mumezungumza na kutupatia njia mwafaka, tutakuwa tumefanya kazi ambayo haitakuwa na mshahara. Kwa hayo mengi ama machache, mwendo utakuwa ni ule wa aste aste ama kama ni wa kobe, tuungane mikono pamoja Kenya isonge mbele. Asanteni. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
12 Oct 2016 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Chairman. I really do not want to oppose this clause but I am opposing it just because of the wording “extraneous security circumstances”. To me, these words are ambiguous and one can take advantage and use this provision negatively for their own interest and not for the country’s interest. Therefore, we need clarity on this amendment. Otherwise, if you remove these three words, we will support the amendment. Thank you.
view