Mohammed Ali Mohamed

Parties & Coalitions

Hon. Mohammed Ali Mohamed

Hon. Mohammed Ali is a former Investigative Journalist with KTN. He initially planned to run for office on an ODM ticket but lost the nominations.He nonetheless went on to win the seat as an independent candidate.

Hon. Mohammed Ali was also a finalist in the People's Shujaaz Awards 2018 edition under the Health category.

All parliamentary appearances

Entries 91 to 100 of 104.

  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, hili ni wazo ambalo liliwahi kuletwa na Rais Uhuru Kenyatta Juni mwaka uliopita. Rais alipendekeza kwamba katika kila kaunti, kuwe na hospitali ya rufaa. Ningependa kutoa utaratibu wa mambo fulani ambayo yanachangia kuwepo kwa hospitali hizi kwa sababu asilimia 80 ya Wakenya ni wale ambao hawawezi kufikia huduma hizi za afya. Nitaanza kwa kutoa mifano ambayo imesalia katika historia ya Kenya. Nitaanza na kwangu nyumbani kule Mombasa. Kuna mtoto mdogo kwa jina la Satrin Osinya au Baby Osinya aliyepigwa risasi na akakaa na risasi kichwani kwa takriban siku nne kabla ya kuletwa Nairobi ili afanyiwe ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Leo napendekeza na kusema kwamba kila kaunti ipewe hospitali yake ya rufaa ili mwananchi wa kawaida aweze kufikiwa. Si kusema tu zijengwe bali pia nasema zile zilizopo hapo zinaweza boreshwa zaidi na kuwekwa katika kiwango cha Level 6 ambayo itaweza hudumia mwananchi wa kawaida aliye na matatizo chungu nzima. Hospitali ambazo ningelipenda zianze kufanyiwa ukarabarati wa hali ya juu na kuanza kufikia wananchi kufika ile kiwango ya Level 6 ni Meru, Embu, Mombasa, Kakamega, Busia, Jaramogi, Garissa na Kisii ambazo ni Level 5. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Mhe. Spika wa Muda, nadhani utashangaa nikikwambia ya kwamba taifa hili lina madaktari wa kutibu saratani yani oncologists, kwa lugha ya kimombo wanaohudumia Wakenya takriban 45 milioni madaktari 23 peke yake. Hawa madaktari ni wa kibinafsi. Namaanisha nini? Wanahudumu katika hospitali ambazo ni za wale ambao wana nguvu kama Aga Khan University Hospital na Nairobi Hospital. Mkenya wa kawaida hawezi kuenda kutibiwa ugonjwa wa saratani katika hospitali hizo. Miaka 55 imepita tangu Kenya ipate Uhuru na tunajipiga kifua tukisema tumeendelea, na ilhali tuna madaktari wa upasuaji yaani neurosurgeon 18. Hii ni aibu iwapo tuna madaktari 18 Kenya nzima. Leo tunajipiga ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Leo Mbunge katika Bunge hili akisikia anasokotwa na tumbo kidogo tu, yeye ana daktari wake wa kipekee. Yeye ana nguvu za kwenda katika hospitali na kuhudumiwa mara ya kwanza. Kule mashinani, kuna watu ambao tumbo zao zinanguruma kama mitambo ya kuchapia mahindi lakini hawajui wataenda wapi, kwa sababu hawana daktari wa kibinafsi, hospitali haziko karibu na iliyoko karibu iko katika kaunti nyingine. Haya ndiyo mambo ambayo nataka tuangalie. Kwa mfano, Kenya nzima madaktari waliosomea taaluma mbalimbali ambazo nimezitaja kama vile saratani, upasuaji na figo ni 425. Nitakupatia utaratibu tu wa kukuonyesha athari ambazo zinaweza kutupata iwapo hatutaweza kushughulikia janga hili, ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Katika kaunti ya Kwale, watu 649,331 wanahudumiwa na madaktari 65. Hawa ni watu takriban 700,000. Sehemu kama Nyeri ambayo ina watu takriban 700,000 wanahudumiwa na madaktari 143. Kiambu ambayo ina watu takriban 1.6 milioni wanahudumiwa na madaktari 278. Kisumu ambayo idadi yake inakaribia milioni moja, wanahudumiwa na madaktari 163. Ukiangalia kaunti ya Kisii ambao ina idadi ya 1.2 milioni wana madaktari 163, utaona ya kwamba wanahitaji madaktari 989 zaidi. Kisumu wanahitaji madaktari 800. Kiambu wanahitaji madaktari 1,343. Hizi tu ni baadhi ya sehemu ambazo zinaathiriwa sana. Hii ndiyo sababu ambayo imetuleta katika Bunge hili. Tulienda kupiga kampeini na tukawaahidi wananchi ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Madaktari waliosajiliwa na Serikali na ambao wanajulikana Kenya nzima ni 11,000. Hawa wanahudumia Wakenya 45 milioni. Kati ya hawa madaktari 11,000, wanaofanya kazi, view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: kwa lugha ya kimombo, ni 6,000 peke yake. Hivi sasa tunapozungumza, kuna wale ambao ni watahiniwa, tunawaita interns kwa lugha ya kimombo, ni 1,000. Wakimaliza kusoma, hawana mahala pa kuenda. Watajiunga na wenzao 1200 ambao hawana kazi na wako nje. Kwa ufupi, nasema taifa hili linahitaji madaktari 34,445. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Nitaendelea bado kwa kueleza ni kwa nini hasa tunataka hizi hospitali ziweze kuhudumia wananchi. Nitaanza na masuala ya rufaa. Leo mgonjwa akiwa Nyeri, Kiambu, Mombasa ama Turkana, ataenda katika hospitali iliyoko hapo. Hospitali za maskini ni hospitali za Panadol, dawa ya maumivu tu, maana hawana dawa zingine. Wakienda katika hizi hospitali, iwapo wana kesi nyeti, ni lazima waletwe Nairobi. Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ina madaktari 264. Wale ambao wanasimama pale casualty kwa matibabu ya dharura ni sita. Kwa mfano, Hospitali ya Coast General inapokea zaidi ya watu 50 kwa siku moja kutoka kaunti mbalimbali waliotumwa kwa sababu vifaa ama ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Mwaka wa 2015/2016, Serikali ya Kenya ilitumia Kshs.38bilioni kwa mashine za kisasa katika hospitali lakini kwa sasa hazifanyi kazi, kwa sababu hatuna madaktari wanaopata mafunzo ya kuzitumia. Mwaka uliopita 2015/2016, iliangaziwa katika vyombo vya habari ya kwamba mashine za kisasa za saratani na figo zimekuja. Watu walifurahi na wakasema kweli ugatuzi umezaa matunda. Ugatuzi wakuleta mashine bila daktari wa kujua kuzitumia nikutia gunia upepo kwa maana haina faida. Ninaposema kutia gunia upepo na maanisha ya kwamba unatia gunia upepo lakini linatoa. Kwa hivyo, haujazi. Inakuwa ni kazi ya bure. Je, kujenga hospitali moja ya rufaa katika kaunti moja itagharimu Serikali ... view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Kaunti ya Kilifi ina madaktrari wa upasuaji wa caesarean section 18. Ina madaktari wa upasuaji 18 peke yake. Idadi ya vitanda ni 610. Wagonjwa wanaokwenda kutibiwa kila siku ni zaidi ya 10,852. Watu wanaokufa ni 1,410. Wanakufa kwa sababu ya magonjwa ya kiajabuajabu. Magonjwa yanayo tiba lakini tunayachukulia mzaha mzaha. Leo, Mombasa tunakufa kwa sababu ya Chikungunya; eti ukiumwa na mbu, wewe kwisha. Hatuna wataalamu wa kupambana na magonjwa. Maradhi ya ajabuajabu yanatokea na hatuwezi saidika. Asilimia kubwa ya Wakenya hata hawana ile Bima ya Afya ya Kitaifa. Hawawezi kujitetea na hawajui la kufanya. Angalia Kaunti ya Mombasa. Idadi ya ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus