Hon. Mohammed Ali is a former Investigative Journalist with KTN. He initially planned to run for office on an ODM ticket but lost the nominations.He nonetheless went on to win the seat as an independent candidate.
Hon. Mohammed Ali was also a finalist in the People's Shujaaz Awards 2018 edition under the Health category.
20 Feb 2019 in National Assembly:
wa figo ni 16. Hatuna maabara. Ikiwa leo mtu ni mgonjwa na hakuna maabara ya figo, inakuwa matatizo. Huyo mtu anafariki kwa sababu Serikali imeshindwa kusaidia wananchi wa Jamhuri ya Kenya kwa kuekeza katika afya.
view
20 Feb 2019 in National Assembly:
Juzi nimeona kuna mgomo wa nesi. Wamesema kwamba hawalipwi vizuri na wataendelea kugoma. Mimi nawaunga mkono. Endeleeni kugoma mpaka siku ile mtaheshimiwa na muweze kuangaliwa, ili Wakenya waweze kuhudumiwa. Tangu hao manesi waanze kugoma, watu wengi wamefariki hospitalini. Hii si makosa ya mwanachi wa kawaida. Ni makosa ya Serikali. Madaktari Kenya nzima ni 11,000 kwa Wakenya milioni 45.
view
20 Feb 2019 in National Assembly:
Asante, Naibu Spika. Unajua wakati tuna mjadala mzito kama huu, ambao unasimamia maswala ya maskini wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mwezangu asijaribu kuleta mchezo ndani ya kazi. Lakini nesi ni sawa tu. Ni kama kusema nurse kwa Kizungu. Kwa hivyo, tunasema nesi ama daktari. Sipingani na hilo, ila tu kwamba ni lugha hauelewi. Lakini asante sana. Nilikuwa nazungumia madaktari na kusema kwamba tuko na elefu 11 dhidi ya Wakenya milioni 45. Dawa ni sababu ingine ya kufanya watu wetu wazidi kuumia. Hospitali zetu hazina dawa. Wagonjwa huenda hospitalini, mtu anapiga foleni kuanzia asubuhi hadi jioni na hapati dawa. Kifo chake ...
view
20 Feb 2019 in National Assembly:
Nambari ya nne ni udhalimu wa Serikali. Leo niko radhi kusema kwamba Serikali imefeli wananchi wa Jamhuri ya Kenya. Serikali haiwekezi katika mambo ya maana. Leo Serikali inatoa bajeti kubwa kwa NYS, lakini haiwezi kutoa bajeti kubwa kwa afya. Tukitoa bajeti kubwa kwa National Youth Service (NYS), inaporwa na watu. Hatutoi bajeti kwa afya kuhakikisha kwamba tumeboresha hospitali zetu au kuhakikisha tuna vifaa spesheli vya kupambana na maradhi aina mbalimbali. Leo katika Bunge hili, tuna Wabunge 13 ambao wana saratani. Inafaa ituume na kusema kwamba hata sisi ni wagonjwa. Kwa nini tusiwatetee wale wako nje kwa sababu tuna nguvu na ...
view
20 Feb 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Nakubaliana na kauli mbiu yako lakini inafaa ujue Serikali ni sisi na Serikali ni wananchi wa Jamhuri ya Kenya. Bila ya wananchi, sisi hatuwezi kukaa hapa. Lakini nimekubaliana na kauli mbiu yako na nasema asante sana. Nilikuwa nazungumzia udhalimu wa Serikali kwa kufeli kuwahudumia wananchi wa Kenya kiafya na kusema kwamba imekataa kuwekeza katika afya. Nataka pia kuzungumzia ugatuzi wa afya kwa sababu kule mashinani, tunapata shida sana. Hatuwezi sisi kama Wabunge kutatua masuala ya afya mashinani kwa sababu ya ugatuzi. Hii imeleta balaa. Kuna baadhi ya viongozi kutoka kaunti mbali mbali ambao, badala ya ...
view
20 Feb 2019 in National Assembly:
usimamizi wa hospitali au masuala ya matatizo yanayotokea. Juzi katika runinga tuliona jamaa ameenda katika hospitali ya Kenyatta akaiba mtoto wake kwa sababu ameshindwa kulipa Sh56,000. Na waibe watoto wawapeleke nyumbani kama serikali inashindwa kuwaangalia. Kwa nini tunaona vituko kama hivi vinatokea? Tunaona mtu anaenda hospitalini sio mwizi wa kawaida bali mwizi ambaye amedhulumiwa na anataka mtoto wake. Ni mwizi ambaye amepewa bei ambayo haiwezi. Mfuko wake hauwezi na Serikali hata haina huruma na maskini huyo inachukua pesa yake kwa kifua na kama huna pesa inachukua mtoto wako kwa kifua. Hatuwezi kuzalisha shida kila siku kukicha katika Jamhuri hii ya ...
view
13 Feb 2019 in National Assembly:
Mhe.Naibu Spika, naomba kutoa azimio la Hoja ifuatayo: KWAMBA, tukitambua kuwa Ibara ya 43 ya Katiba imebainisha kila mtu ana haki ya kupata kiwango bora zaidi cha afya kinachojumuisha haki ya kupata matunzo ya kiafya na kutonyimwa matibabu ya dharura; aidha ikifahamika kwamba gharama za matunzo ya kitabibu katika taasisi za kiafya za kibinafsi zingali ghali mno, hivyo kuwalazimu Wakenya wengi kupendelea kusaka huduma hizo kwa hospitali za umma; tukizingatia kwamba licha ya bei nafuu ya matibabu katika hospitali za umma ikilinganishwa na hospitali za kibinafsi, bado Wakenya wengi hawamudu, hivyo basi kutumbukia kwenye madeni, ufukara na dhiki wanaposhindwa kulipa ...
view
14 Nov 2018 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika, naomba kutoa taarifa ya Hoja ifuatayo: KWAMBA, tukitambua kuwa Ibara ya 43 ya Katiba imebainisha kuwa kila mtu ana haki ya kupata kiwango bora zaidi cha afya kinachojumuisha haki ya kupata matunzo ya kiafya na kutonyimwa matibabu ya dharura; aidha, ikifahamika kwamba gharama za matunzo ya kitabibu katika taasisi za kiafya za kibinafsu zingali ghali mno hivyo kuwalazimu Wakenya wengi kupendelea kusaka huduma hizo kwa hospitali za umma; tukizingatia kwamba licha ya bei nafuu ya matibabu katika hospitali za umma ikilinganishwa na hospitali za kibinafsi bado Wakenya wengi hawamudu hivyo basi kutumbukia kwenye madeni, ufukara na dhiki ...
view
14 Nov 2018 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Kwanza nitoe kongole kwa Wabunge wote kwa kuienzi lugha ya taifa ya Kiswahili. Maana leo hii Bunge limekuwa la mahajam. Naona leo watu wamefurahia kwa kuweza kuwasilihisha maswala haya. Kukosoa tu, kwanza kabisa nitaanza kwa kusema kwamba hakuna Hoja bure katika taifa hili. Kila Hoja ina maana yake.
view
14 Nov 2018 in National Assembly:
Asante, Mhe. Naibu Spika. Mhe. mwenzangu alianza kwa kusema yeye anafahamu na kuelewa Kiswahili. Kongole ni kukupongeza kwa kuzungumza lugha ya taifa ya Kiswahili. Hata hivyo, nikiendelea nataka kusema kwamba alivyosema Mhe. mwenzangu ni kwamba hili ni Bunge la Taifa. Lengo letu kuu hapa Bungeni ni kutunga sheria za taifa. Nikiangalia Hoja ambayo nimeleta mbele yenu siku ya leo, kulikuwa na hali ya utata wakati wa kupiga chapa lakini nadhani tulikuwa tunasema wakipokea matibabu katika hospitali za rufaa…
view