Mohammed Ali Mohamed

Parties & Coalitions

Hon. Mohammed Ali Mohamed

Hon. Mohammed Ali is a former Investigative Journalist with KTN. He initially planned to run for office on an ODM ticket but lost the nominations.He nonetheless went on to win the seat as an independent candidate.

Hon. Mohammed Ali was also a finalist in the People's Shujaaz Awards 2018 edition under the Health category.

All parliamentary appearances

Entries 61 to 70 of 104.

  • 27 Feb 2019 in National Assembly: The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika. Naomba kuendeleza Hoja ifuatayo: KWAMBA, tukitambua kuwa Ibara ya 43 ya Katiba imebainisha kuwa kila mtu ana haki ya kupata kiwango bora zaidi cha afya kinachojumuisha haki ya kupata matunzo ya kiafya na kutonyimwa matibabu ya dharura; aidha, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: ikifahamika kwamba gharama za matunzo ya kitabibu katika taasisi za kiafya za kibinafsi zingali ghali mno, hivyo kuwalazimu Wakenya wengi kupendelea kusaka huduma hizo kwa hospitali za umma; tukizingatia kwamba,licha ya bei nafuu ya matibabu katika hospitali za umma ikilinganishwa na hospitali za kibinafsi, bado Wakenya wengi hawamudu na hivyo basi kutumbukia kwenye madeni, ufukara na dhiki wanaposhindwa kulipa malimbikizi ya gharama za matibabu yao na ya wapendwa wao; Bunge hili linahimiza Serikali ya Kitaifa kufutilia mbali gharama zote za matibabu ya wagonjwa wote wanaofariki wakipokea matibabu katika hospitali za umma na za rufaa. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Nitaanza mjadala wangu kwa kulitaka Bunge hili, kuweza kutunga sheria ya kufutilia mbali ada dhidi ya maiti. Hii ni kwa sababu tunajua wazi ya kwamba huwezi dai maiti. Kwa nini nasema tuweze kufutilia mbali ada hizi? Nina sababu zangu ambazo niliweza kupata baada ya kuzunguka mashinani na kuzungumza na wananchi wapendwa wa Jamhuri ya Kenya. Waliweza kunipatia malalamiko yao kuhusiana na maiti kuzuiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Sababu za vifo kwanza, tunasema kila nafsi itaonja mauti, kwa sababu ni Mwenyezi Mungu hupeana na pia ni yeye huchukua. Lakini kuna kuonja maiti kwa sababu ya udhalimu wa serikali iliyo mamlakani ambayo haitaki kuangalia maslahi ya mwananchi wa kawaida. Sababu ya kwanza inayosababisha vifo katika hospitali za umma humu nchini ni usimamizi mbovu wa visa vya maradhi. Kwa mfano, mwaka uliopita niliweza kuleta mjadala katika Bunge hili nikiitaka Serikali iweze kujenga hospitali moja ya rufaa katika kaunti zote 47 humu nchini. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Tunaposema visa vya maradhi vinatokana na usimami mbovu, utaona maskini ambao ni asilimia kubwa nchini Kenya, wanapokuwa wagonjwa, wanakimbilia mambo ya ajabu, ajabu. Kwa mfano, maskini akiwa mgonjwa na hawezi kupata pesa za kukimbia hospitalini, yeye atakimbia kwa waganga ajaribu kugangwa kule ili apate matibabu kwa sababu hana pesa za kwenda hospitalini. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Pili, madaktari wa kienyeji - tunawaita madaktari miti shamba - asilimia kubwa inaamini ya kwamba wanaweza kupambana na visa mbali mbali vya kiafia. Tatu, kuna madaktari gushi. Tunaona katika vyombo vya habari na kushuhudia ya kwamba kuna madaktari gushi ambao hawajasomea taaluma hiyo na wanaenda mitaani na kufungua kliniki ovyo ovyo na kutibu watu bila ya leseni inayotakikana. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Lingine ni kwamba maskini huashiria kujitibu, maskini labda ana saratani na hajui. Lakini anaona dawa yake ya kipekee ya kupona ni kununua tembe ya Panadol ajigange polepole nyumbani kwa sababu hana nguvu za kufikia hospitali. Mwisho, nyingine nitazungumzia ni viongozi wa dini. Siku hizi tumekuwa na viongozi ambao badala ya kuhubiri neno, wanahubiri meno. Kazi yao sasa ni kudaganya wananchi na kuwapa imani ya kwamba wanaweza watibu, na hivyo basi kuwachezea. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Ukosefu wa taaluma ndiyo umetuletea matatizo haya yote. Ndiyo unaosababisha maafa mengi katika hospitali na uhaba wa vifaa vya matibabu. Mwaka uliyopita niliweza kusimama ndani ya Bunge hili na kusema maswala mengi kuhusiana na madaktari, magonjwa na vile vile uhaba mkubwa wa madaktari nchini Kenya. Pia, nilisimama katika Bunge hili na kusema ya kwamba saratani ambayo ni ya tatu nchini Kenya kusababisha vifo, hadi wa leo hatujafikiria kuweza kupambana nayo. Hii ni kwa sababu sisi tuna madaktari 23 wa saratani Kenya nzima, kwa Wakenya milioni 45. view
  • 20 Feb 2019 in National Assembly: Kila siku katika kila mwaka tunapata visa 38 vya saratani. Upasuaji ni jambo lingine ambalo nilizungumzia. Tuna madaktari 18 wa upasuaji ambao hawawezi kujimudu. Madaktari The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus