Hon. Mohammed Ali is a former Investigative Journalist with KTN. He initially planned to run for office on an ODM ticket but lost the nominations.He nonetheless went on to win the seat as an independent candidate.
Hon. Mohammed Ali was also a finalist in the People's Shujaaz Awards 2018 edition under the Health category.
2 Oct 2019 in National Assembly:
Loonena ambaye ni Director General wa Kenya Coast Guard na Meja Generali Levi Franklin Mghalu, Kenya Navy Commander . Hawa ni watu ambao wana uwezo. Walikuwa karibu na wangeokoa mtoto huyo mdogo mwenye miaka minne na mamake. Ilichukua takriban dakika 20 watu hao kutafuta usaidizi pasi na kuupata. Kifo cha Mariam Kighenda na Amanda kimesababishwa na Serikali ya taifa na ni sharti walipwe.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Shukran sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Pia mimi ningependa kuchangia na kusema kwamba hii ni aibu hapa nchini Kenya iwapo baada ya kutokea kile kisa cha Mtongwe bado hatujajifunza lolote. Ni aibu kubwa iwapo leo Serikali itatangaza na kusema kwamba haina hewa ya kutosha ama gesi ya kuweza kufika kule chini. Leo Kenya, hatuna fedha za kununua hewa, lakini tuna fedha za kununua vitoa machozi. Leo Kenya, hatuna fedha za kununua hewa, lakini tuna pesa za kununua makumi ya magari kwa viongozi. Leo hii katika Kenya, hatuna pesa ya kununua hewa, lakini tuna pesa za ufisadi.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Hii ni aibu na ni sharti sheria ichukue mkondo wake na kuhakikisha kwamba wahusika wote ambao wamekaa kimya wakiangalia marehemu Mariam Kighenda na mtoto Amanda Mutheu wakiangamia na kufa kifo cha polepole, ni sharti wachukuliwe hatua za kisheria.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Mhusika mkuu, Waziri wa Uchukuzi Bwana Macharia, achukuliwe hatua. Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Ferry Services, Kenya Ports Authority (KPA), Maritime Authority of Kenya na Kenya Coast Guards (KCG) wote wachukuliwe hatua za kisheria, maana hii itakuwa ni hekaya za abunwasi. Tutakuwa tunarudia haya miaka nenda miaka rudi.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Katika Mtongwe Ferry tulipoteza makumi ya watu na tulidhani labda tutajifunza mengi na kuhakikisha kwamba tumeweza kuwa tayari kwa matukio kama haya.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Asante sana. Kama anataka nizungumzie pesa ya ufisadi nitampatia. Shilingi bilioni moja nukta nane iliweza kutolewa kununua feri mpya mbili. Hizo pesa hatujui zimeenda wapi. Ferry mpya hatujapata mpaka sasa. Shilingi milioni 78 zilitolewa kwa Kenya Ferry Services iweze kuweka camera za CCTV ili wale ambao wanakaa mahala na kuangalia matukio yote yanayotokea, wakiona shida yeyote wanaweza kuwafikia wananchi kwa haraka. Hizi ndizo pesa ninauliza ziko wapi na zinafanya nini?
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Nilikuwa ninazungumzia kujiuzulu au kuwachishwa kazi kwa wahusika wote wakuu kama nilivyokuwa nimewataja hapo awali.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Pia, nitazungumzia masuala ya kazi. Vijana wengi wa Pwani hawapewi kazi. Inapofika ni wakati wa kuandika wanajeshi wa maji, vijana wengi walio na ujuzi hawapewi nafasi. Inakuwa ni kupeana kazi kwa kujuana. Bahari ina wenyewe na wenye bahari wanafaa wapewe kazi hii.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Pia, ningependa kuzungumzia katika siku za usoni waanze kufanya mikakati ya kuhakikisha kwamba wameweka kivukio cha daraja ili kuhepusha majanga kama haya.
view