Hon. Mohammed Ali is a former Investigative Journalist with KTN. He initially planned to run for office on an ODM ticket but lost the nominations.He nonetheless went on to win the seat as an independent candidate.
Hon. Mohammed Ali was also a finalist in the People's Shujaaz Awards 2018 edition under the Health category.
26 Feb 2020 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kumpongeza Mhe. Keter kwa kuleta maoni na fikira za vijana katika Bunge Hili. Hakika, kama taifa tunalo tatizo kubwa. Tangu enzi za hayati Mzee Jomo Kenyatta, hayati Daniel Toroitich arap Moi, Rais Mstaafu Mwai Kibaki na sasa, Rais Uhuru Muigai Kenyatta vijana wamekuwa ni wakupewa ahadi kwa midomo tu wakati ambapo wanatakikana kutimiza malengo ya watu fulani. Asilimia sabini na tatu ya wakenya ni vijana. Ni dhahiri hiyo asilimia sabini na tano haionekani. Kuingia katika Bunge hili, kupata kazi na kutafuta riziki katika Jamhuri ya Kenya imekuwa ngumu sana kwa vijana wetu. ...
view
26 Feb 2020 in National Assembly:
Bunge. Huwezi kupata ujuzi wa Bunge ukiwa nje. Huwezi kupata ujuzi wa kuwa daktari ukiwa nje. Wewe ni mwanagenzi, hupewi nafasi ya kuweza kujifunza.
view
26 Feb 2020 in National Assembly:
Jambo lingine ni kuhusu masuala ya elimu. Ningependa kumkosoa Prof. Magoha kidogo na kusema kwamba ukiweka akili yako katika vyuo vikuu sana na usahau kuwekeza katika vyuo vya anuwai, basi kutakuwa na matatizo chungu nzima. Mimi siwezi kuwa profesa. Sote hatutoshi kuwa maprofesa. Sote hatutoshi kuwa madaktari au wahandisi. Kuna wale wanaoongozwa na talanta ya Mwenyezi Mungu. Wengine wamepewa talanta ya kucheza mpira, wengine wamepewa talanta ya kuimba, na wengine wamepewa talanta ya kufanya sarakasi. Ni sharti tutoe nafasi hizi kwa vijana ili waweze kukuza talanta zao.
view
26 Feb 2020 in National Assembly:
Vikwazo ambavyo vimewekewa vijana – masuala ya vyeti vya kuthibisha tabia njema, KRA PIN, CRB, EACC, na hata ada ya kupata leseni kutoka NTSA ya Ksh3,000 – inakuwa ni kama dhuluma na kejeli kwa vijana. Ninapotazama siasa za nchi zinavyoenda na kuangalia masuala ya BBI, ambayo inasema ni kuwaleta Wakenya pamoja, hamna mtu ana pingamizi nalo lakini ukiangalia misafara ya BBI, hamna sauti ya vijana, ambao ni asilimia 73 ya Wakenya wote. Hamna sauti ambayo imekwa pale ya kusema itazungumzia masuala ya vijana peke yake. Building Bridges Initiative itatumia vijana kuwasilisha hoja yao na matakwa yao lakini itahakikisha kwamba hao ...
view
26 Feb 2020 in National Assembly:
Kutakuwa na athari kubwa sana katika taifa hili iwapo masuala ya vijana hayatatatuliwa. Hii ni kwa sababu itafika mahali ambapo vijana watachoka katika taifa hili na tukifika hapo, kurudi nyuma itakuwa vigumu. Saa hizi ukiangalia ni kama kwamba kuna vuguvugu la tatu ambalo lina njaa, hasira, limedhulumiwa na linaogopa kuingia katika karne ya kuitwa wazee sasa.
view
26 Feb 2020 in National Assembly:
Tukiingia katika Bunge hili tulikuwa vijana chipukizi, lakini sasa tunaanza kuaga miaka hiyo ya thelathini na tano na kuanza kuitwa wazee. Lakini hatujatimiza tuliloletwa kutimiza katika Bunge hili kwa sababu hiyo nafasi imekuwa ni haba. Hiyo nafasi ya kuleta idadi kubwa hapa imekuwa ngumu. Nchi zinazoendelea na kustawi duniani, nchi zinazofanya vyema na kutoa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
26 Feb 2020 in National Assembly:
mfano mzuri ni zile ambazo kazi zinaekezwa kwa vijana. Nchi ambayo inaendeshwa na vijana inakwea kisiasa, kiuchumi na inahakikisha ya kwamba nchi hiyo inakuwa mfano bora kwa mataifa mengine. Ni lazima tuwe waangalifu katika hii nchi yetu, na hili suala litatuletea matatizo katika siku za usoni. Iwapo hatutawasaidia hawa vijana, basi Kenya itakuwa katika hali mbaya sana.
view
26 Feb 2020 in National Assembly:
Ninamalizia kwa kusema ya kwamba Mhe. Keter ameleta wazo nzuri katika Bunge la taifa, na mimi naliunga mkono na ninatumai ya kwamba haya yote yaliyoweza kuzungumziwa na Wabunge wengine yatasikizwa na kuhakikisha ya kwamba nafasi ya vijana imepatikana katika Jamhuri hii ya Kenya. Asante
view
10 Feb 2020 in National Assembly:
Shukrani sana, Mheshimiwa Spika. Kwa niaba ya wakaazi wa Eneo Bunge la Nyali, familia yangu, ninatoa risala za rambirambi kwa familia ya hayati Daniel Toroitich arap Moi. Hakika, atakumbukwa kwa mambo mengi mazuri na tunamuomba Mwenyezi Mungu amfutie dhambi zake na hata za siri na amlaze pema panapolazwa wema.
view
2 Oct 2019 in National Assembly:
Shukrani sana Mheshimiwa spika kwa kunipa fursa hii. Ningependa kuwaunga wenzangu mkono na kuungana na taifa nzima kwa ujumla kutoa rambirambi zetu kwa marehemu Mariam Kighenda na mtoto wake, Amanda. Licha ya hayo, umesema ya kwamba utatutengea muda tuzungumzie jambo hili kwa sababu, iwapo hakutakuwa na suluhu, tutakuwa na matatizo chungu nzima katika siku za usoni. Kwanza kabisa, inaelekea kuwa siku ya tatu Serikali ikiwa imenyamaza na kuangalia tu bila usaidizi wowote. Leo Waziri wa Uchukuzi amemuamrisha Katibu wa Kudumu katika wizara afike pale na kusaidia katika shughuli za kupata maiti. Pesa nyingi zimetolewa katika Huduma ya Kenya Ferry . ...
view