Mohammed Ali Mohamed

Parties & Coalitions

Hon. Mohammed Ali Mohamed

Hon. Mohammed Ali is a former Investigative Journalist with KTN. He initially planned to run for office on an ODM ticket but lost the nominations.He nonetheless went on to win the seat as an independent candidate.

Hon. Mohammed Ali was also a finalist in the People's Shujaaz Awards 2018 edition under the Health category.

All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 104.

  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninasema kwamba leo ninaomba Mariam Kighenda na Amanda Mutheu watusamehe kwa sababu tumefeli kama nchi na tutarekebisha tuweze kuhakikisha kwamba matukio kama haya hayatatokea tena katika siku za usoni. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Mungu alaze mioyo yao mahali pema, panapo lazwa wema. view
  • 2 Oct 2019 in National Assembly: Asante. view
  • 27 Feb 2019 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Naomba kujibu Hoja ambayo tulizungumzia wiki iliyopita. Kwanza kabisa, nitaanza kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wabunge wote waliochangia Hoja hii ya kufutilia mbali ada za matibabu katika hospitali za umma za rufaa pindi mtu anapofariki. Natoa shukrani zangu kwa Wabunge wote waliochangamka na kuchangia Hoja hii wakiomba ya kwamba ipasishwe ili tuweze kupunguza mzigo wa wananchi wa Jamhuri ya Kenya. Kuongezea tu kidogo ni kwamba Hoja hii itasaidia katika gharama ya mwananchi wa kawaida iwapo itapasishwa. Kwa mfano, sisi Wabunge hatuna mamlaka kwa sababu ya… view
  • 27 Feb 2019 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika, utumizi wa neno “kupasishwa” au neno “kupitisha” utategemea lugha unayoitumia. Unaweza kuzungumza Kiswahili cha Mvita au cha Kenya. Kwa hivyo, kuna tofauti lakini yote ni moja. Hoja inapitishwa katika Bunge na Wabunge. view
  • 27 Feb 2019 in National Assembly: Mheshimiwa Naibu Spika, kuweka wazi wacha tuseme “iwapo Bunge hili litapitisha Hoja hii ambayo tulileta wiki iliyopita”. Kwa ufupi, Hoja hii itasaidia mwananchi wa kawaida katika masuala ya gharama ya maisha kwa sababu sisi Wabunge hatuna mamlaka dhidi ya mambo fulani yanayotendeka katika taifa hili. Kwa mfano, swala la afya liko katika ugatuzi. Ni swala ambalo wahusika wakuu katika kaunti ni magavana ambao wanafaa wasaidie katika mambo haya lakini sio wote. Wengine wamezembea katika majukumu yao, hivyo basi kutuletea kazi kubwa zaidi. Wiki iliyopita sikuweza kugusia mambo mawili. Katika Hospitali ya Kitaifa ya Rufaa ya Kenyatta, kila wadi ina vitanda ... view
  • 27 Feb 2019 in National Assembly: Katika mradi wa Linda Mama, Serikali inawajibika na kulipia akina mama ada ya Kshs17,000. Swali tunalofaa tujiulize ni kwamba katika huu mradi wa Linda Mama, je ikizidi Kshs17,000… view
  • 27 Feb 2019 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika. Katika mradi wa Linda Mama, Serikali inalipa Kshs17,000 lakini hii haimudu kujifungua kwa upasuaji ambao kwa lugha ya kimombo ni Caesarean Section . Je, hatima ya mwanamke anayejifungua kwa upasuaji iko vipi? Je, hatima ya mtoto ambaye anazaliwa kabla ya siku yake iko vipi? Hivi ndivyo vipengele ambavyo tunaangalia kwa undani na kuhakikisha ya kwamba mwananchi wa kawaida amesaidika. Tutahesabu watu na tutatumia Kshs6 bilioni. Pia, kuna kauli mbiu ya kura ya maoni ambapo zaidi ya Ksh18 bilioni itatumika. Hizi pesa zitatumika kwa mambo ambayo hayana uzito kwa mwananchi wa kawaida. Badala hizi pesa zitumike katika ... view
  • 27 Feb 2019 in National Assembly: Nasimama kuzungumzia fundi wa mbao, mfanyikazi wa mjengo, mama wa mboga, dereva wa matatu, kondakta na wafanyikazi wote wa jua kali ambao wanapopoteza wapendwa wao, miili yao inazidi kuzuiliwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti na baadaye kutupwa. Naomba Bunge hili lipitishe Hoja hii na tuweze kuendelea mbele kujenga Jamhuri ya Kenya. view
  • 27 Feb 2019 in National Assembly: Asante sana. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus