Mohammed Ali Mohamed

Parties & Coalitions

Hon. Mohammed Ali Mohamed

Hon. Mohammed Ali is a former Investigative Journalist with KTN. He initially planned to run for office on an ODM ticket but lost the nominations.He nonetheless went on to win the seat as an independent candidate.

Hon. Mohammed Ali was also a finalist in the People's Shujaaz Awards 2018 edition under the Health category.

All parliamentary appearances

Entries 81 to 90 of 104.

  • 14 Nov 2018 in National Assembly: Kisha kejeli ya Katiba kama alivyosema mwenzangu, hatujakejeli Katiba kwa sababu tuko katika Jumba hili kutunga sheria na wakati mwingini huandikwa, hufutiliwa mbali na kuandikwa tena upya kwa manufaa ya wananchi wa Jamhuri ya Kenya. Sera za afya nchini Kenya ni za kitaifa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 20 Sep 2018 in National Assembly: Mhe. Spika, Shukrani sana kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, ningependa kuweka rekodi sawa kabisa. La kwanza na muhimu zaidi ni kwamba idadi ya Wabunge waliokuwa wakitaka kupiga kura ilikuwa mia asili mia. Ya pili, swali likauliza na Wabunge wote kwa kauli moja wakakubaliana na kupinga na kusema ya kwamba hawatakubali kama wanavyotaka ila kama anavyotaka Wanjiku. Hamna mtafaruku wowote ambao umetokea baina yetu. Wakati ambapo Mwenyekiti aliomba tupige kura, tulikubaliana kwa kauli moja tuweke foleni lakini baadhi ya viongozi ndani ya Bunge, wakiwemo Duale na Mbadi, wakaanza kuiingilia na kuzuia upigaji wa kura. view
  • 20 Sep 2018 in National Assembly: Ya pili, tunataka access to information . Tunataka kujua venye kila Mbunge atakavyopiga kura. Kura tumepiga. Tumemaliza kupiga kura. Na kauli mbiu ni kwamba Wabunge wamekataa. Nitampisha ndugu yangu naye achangie kwa dakika moja yangu. view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: Shukrani sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Langu ni kuunga mkono Hoja hii na kupendekeza kwamba Wizara ya Elimu. Sayansi na Teknolojia iweze kuhakikisha kwamba walemavu wana nafasi katika taifa hili. Sisi Wabunge tunapata shida sana wakati tunapotembelewa na Wakenya wenzetu ambao ni walemavu katika afisi zetu. Ninakotoka katika Kaunti ya Mombasa, kuna visa kama hivyo vingi sana katika afisi yangu. Ni vigumu kuwasaidia kwa sababu Serikali haijaekeza wala kuwafikiria watoto walemavu hasa upande wa kuwapatia elimu bora katika shule za chekechea, msingi, upili na hata chuo kikuu ili waweze kupigania nafasi zao kama Wakenya wengine. Mighairi na hayo, vile ... view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: Shule ambazo zipo nchini kuwahudumia ni chache sana. Mimi ninajua shule mbili pekee. Ile Shule ya Thika ya vipofu na Joy Town ambayo iko Kisumu. Sharti tuwe na shule spesheli katika kila kaunti ili tuweze kusaidia hawa walemavu ambao ni Wakenya wenzetu. Demokrasia tunayopigania ni ya kuleta usawa kwa kila Mkenya. Hizi shule zinahitaji walimu na bajeti. Waalimu ni haba. Ni kweli kwamba waalimu wanaoweza kukidhi mahitaji ya hawa wanafunzi ni wachache mno. Ni lazima Serikali ihakikishe kuna walimu wanapokea mafunzo spesheli ya kuangalia watoto hawa. Ningetaka Serikali itoe bajeti kubwa sana kwa walemavu kwa sababu hawana nguvu kama Wakenya ... view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: Pia tuwekeze katika mambo ya michezo. Tusiseme tu shule bali tuwekeze katika shule hizi na tuangalie kwamba zinapata vifaa spesheli ambavyo pia Wakenya wengine wanapata katika shule mbalimbali. Wazo langu ni kwamba wakati ambapo shule zinaundwa, ni vyema pia wao tuwawekee nafasi ya kuhakikisha wanajihisi kama Wakenya wengine ili waweze kuendelea The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: na maisha kama Wakenya wengine. Naunga mkono Hoja hii na ninaifurahia. Mbunge aliyeileta nampa kongole na kusema kwamba nitasimama na Hoja hii. view
  • 15 Aug 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, naomba kuwasilisha Hoja ifuatayo: view
  • 14 Mar 2018 in National Assembly: KWAMBA, tukifahamu Kifungu cha 43 cha Katiba ya Kenya kimeweka wazi kwamba kila Mkenya ana haki ya kuwa na kiwango bora cha afya kinachojumuisha afya bora ya uzazi; aidha, katika utaratibu wa Ajenda ya Maendeleo ya baada ya Mwaka wa 2015, dunia imewajibikia Afya kwa Wote na kutimiza Lengo Endelevu la Maendeleo la tatu (SDG-3) kuhakikisha na kuendeleza maisha na afya bora kwa wote; tukiafiki, uwekezaji katika sekta bora ya afya ni muhimu kuhakikisha kila mtu anapata huduma za kimsingi za afya bila kuzingatia eneo analotoka au hali yake ya kiuchumi; tukitambua, asilimia 80 hutegemea huduma ya afya ya umma ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus