Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1001 to 1010 of 1995.

  • 1 Dec 2021 in Senate: Kwa sasa, hakuna yeyote ambaye amesimamishwa kazi ama kuzuiliwa au kushtakiwa kwa masuala ya ufisadi. Ufisadi ni donda sugu ambalo lazima Serikali hii na Serikali zitazokuja liweze kudhibiti. Bila kufanya hivyo, Wakenya wengine wataendelea kulia bila ya kupata huduma wanazostahili kupata kwa sababu ya ufisadi. view
  • 1 Dec 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, jambo lingine limenisikitisha ni kuona kuwa Mhe. Rais hakuzungumzia kikamilifu uchumi samawati yaani blue economy. Uchumi huo ni muhimu katika nchi yetu kwa sababu tuna ufuo wa bahari na maziwa Victoria na Turkana ambako shughuli za uchumi samawati zinafanyika. Mhe. Rais aligusia tu kijujuu. Maendeleo yanayofanyika katika sekta hii ni ya chini sana na hajatoa natija yeyote kwa Wakenya kuhusiana na suala hili. view
  • 1 Dec 2021 in Senate: Kwa mfano, kudhibiti vyombo vya kuhifadhi samaki wanapovuliwa kwa wingi, barabara katika sehemu ambazo wanavuvi wanavua na zile bandari zinapokea samaki wale, hazijapewa kipaumbele katika maendeleo ya uchumi samawati. view
  • 1 Dec 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, sisi watu wa Pwani tuna tumbojoto kuhusiana na ripoti zilizotolewa kuwa sehemu ya bandari ya Kenya itabinafsishwa kupitia shirika la Kenya National Shipping Line ambalo limeingia mazungumzo na shirika la Mediterranean Shipping Company (MSC). view
  • 1 Dec 2021 in Senate: Mwaka jana kulitolewa Executive Order ambapo mashirika ya Kenya Ports Authority (KPA), Kenya Railways Corporation (KRC) na Kenya Pipeline Company (KPC) yaliletwa pamoja na Industrial and Commercial Development Corporation (ICDC) ambalo ni taasisi ya Serikali ili kuwa na usimamizi moja, kupitia kwa Wizara ya Fedha. view
  • 1 Dec 2021 in Senate: Mhe. Rais hakuzungumzia suala hili ili kutoa mwongozo. Je, suala hili limeleta natija ama la? Ni mambo gani yamezuia kupatikana kwa maendeleo kwa usafirishaji wa mizigo na kudhibiti mambo ya reli, kama ilivyokuwa imekusudiwa na mpaka sasa haijakamilishwa. view
  • 1 Dec 2021 in Senate: Swala hili la kubinafsishwa kwa bandari limetia sana tumbojoto wakazi wa Pwani kwa sababu bandari ndio mtaji mwenyezi Mungu amewajalia nalo. Kwa hivyo, hatutakuwa tayari wakati wowote kuwacha mtaji huu uweze kuharibika. view
  • 1 Dec 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, masuala ya usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Mombasa yalistahili kuzungumziwa kwa sababu Serikali inalazimisha mizigo yote ibebwe na shirika la Standard Gauge Railways (SGR), shirika la reli la Kenya. Hata hivyo, kuna uhuru wa biashara nchini. Kuna wale wanaofanya biashara za malori na za kibinafsi wanastahili kupewa nafasi kufanya hivyo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 1 Dec 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, kwa kumalizia pia ni kwamba, tumeona kuwa maswala ya usafirishaji wa mizigo ni njia moja ambayo itasaidia Wakenya kuweza kujikomboa, hususan watu wa Mombasa na wengine ili kuweza kupata biashara katika kaunti zetu. Ukiangalia mkondo wa barabara kutoka Mombasa mpaka Malaba, kuna biashara nyingi ambazo zinafanyika katika barabara hiyo. Biashara zile ninawezakufilisika iwapo hatutaweza kuwa na usafirishaji wa mizigo kwa njia nyingine mbali na njia ya reli. Nikimalizia, bado tuna changamoto nyingi ambazo nchi inatakikana kuzikabili na kuziepuka. Changamoto hizi tunaweza kuzikabili tu wakati nchi yetu itakuwa na amani. Tutakuwa tunavuta Kamba katika sehemu moja. Hususan ... view
  • 10 Nov 2021 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kumaliza mchango wangu kwa ripoti hii. Niliposimama jana, nilikuwa nimeeleza kuwa baadhi ya wale ambao walichukuliwa na hadi leo hawajapatikana ni kijana anayejulikana kwa jina la Mubarak Husni. Alichukuliwa tarehe 25/3/2018. Niliweza kuleta Taarifa hapa katika Bunge la Senati na hadi leo, habari za kijana huyu, pahali alipo, ama kama yuko hai au ashafariki hazijulikani. Haki Afrika ambayo ni kundi la haki za kibinaadamu ambayo inafanya kazi Mombasa kimeweza kutoa ripoti yake. Mpaka sasa, mwaka huu wa 2021 peke yake, kufikia tarehe 30/10/2021, watu 42 wameweza kuchukuliwa bila ya sababu yeyote. Kati ya ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus