1 Dec 2021 in Senate:
Nampongeza Mhe. Rais pia kwa juhudi zake katika mabadiliko ya tabianchi yaani
view
1 Dec 2021 in Senate:
kwa wale hawajui Kiswahili. Mhe. Rais wetu alisafiri mpaka Scotland na akatoa hotuba. Ujumbe wa Kenya katika mkutano huo ulikuwa na kazi kubwa na ulionyesha mambo mengi ambayo nchi yetu inafanya ili kudhibiti madadiliko ya tabianchi.
view
1 Dec 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, nilipendezwa na mwongozo wake katika maswala ya afya ambapo amejenga hospitali kadhaa katika Kaunti ya Jiji la Nairobi. Sehemu nyingi za Nairobi zilikuwa hazina huduma za afya na aliweza kuzifikisha huduma hizo. Vile vile kina mama wajawazito waliojifungua walitajwa. Mhe. Rais alionyesha kuna kazi kubwa ambayo ameifanya lakini bado kuna mengi yanastahili kufanywa.
view
1 Dec 2021 in Senate:
Hali ya taasisi za kiafya katika kaunti zetu imeimarika kwa sababu ya kujitayarisha na janga hili la korona na bado janga hili halijakwenda. Inafaa tuwe macho ili kuhakikisha janga hili lisiturudie tena. Katika Hotuba yake, Mhe. Rais ameangazia mambo mengi ambayo yanaonyesha kwamba baada ya kushirikiana na Mhe. Raila Odinga, Waziri Mkuu wa Zamani, imeonekana hali ya nchi imekuwa tulivu, usalama ukaimarika na watu wanaendesha mambo yao na kushukisha joto la kisiasa ambalo tunaona limeanza kupanda tena.
view
1 Dec 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, nampongeza baba na kiongozi wa chama chetu, Mhe. Raila Amolo Odinga kwa kuona mbele kwake na kuja pamoja na Mhe. Rais Uhuru Kenyatta ili kushukisha chini joto la kisiasa na kuimarisha uchumi wa nchi hii wakati ulikuwa unayumbayumba kutokana na kura zilizopigwa mwaka wa elfu mbili kumi na saba.
view
1 Dec 2021 in Senate:
Baadhi ya mambo ni mazuri. Hata hivyo, kuna mambo mengi ambayo Serikali inastahili kufanya. Kwanza kabisa ni haki za binadamu. Kwa muda wa miaka minne au mitano iliyopita, tumeona watu wakidhulumiwa na haki za kibanadamu kutoheshimiwa kupitia kwa mauaji ya watu kiholela au extrajudicial killings . Wengine kutekwa nyara bila kujulikana wamepelekwa wapi.
view
1 Dec 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, Kenya ni nchi ambayo inalindwa na Katiba na sheria. Ni nchi ambayo ina taasisi ya mahakama. Licha ya matatizo ya hapa na pale, taasisi hii imekua inafanya kazi yake vizuri zaidi kuliko mahakama za nchi zingine za Afrika na kwingineko. Lakini, ongezeko la watu wanaouliwa kiholela katika mikono ya polisi imekuwa juu sana.
view
1 Dec 2021 in Senate:
Mwaka huu, mashirika ya Haki Africa na Independent Medical Legal Unit (IMLU) wamerekodi visa zaidi ya sabini ambavyo watu wamepoteza maisha yao kiholela au kupotezwa bila kufuata sheria. Ripoti hiyo tuliijadili hapa wiki mbili zimepita na haina haja ya kuongezea. Mhe. Rais angefaa kutoa mwongozo au msimamo wake kwamba ataendelea kuongoza nchi hii kupitia katiba na sheria ambayo iko katika nchi.
view
1 Dec 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, Wakenya wengi katika maeneo ya Pwani na ukanda wa Kaskazini ya Kenya, yaani Northern Kenya ; wanaishi katika hofu kwa sababu hawajui ni wakati gani watakamatwa na familia zao hatizapata fursa ya kuwaona tena. Hotuba ya Mhe. Rais ilikuwa kimya kabisa kuhusu suala la ufisadi. Hapo awali mwaka jana, wakati janga la korona lilipoingia na zabuni za korona zilipoanza kutoka, fedha nyingi zilitolewa na kupotezwa bila ya kuletwa zile bidhaa ambazo zilikusudiwa kununuliwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard ...
view
1 Dec 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, hatujapata ripoti yeyote kuhusu mwongozo au maazimio ambayo Mhe. Rais alitoa kuhusiana na uchunguzi wa masuala ya korona mpaka sasa. Katika uongozi wa Mhe. Rais katika muhula wa mwaka elfu mbili kumi na tatu mpaka elfu mbili kumi na saba, tuliona wakati fulani Mawaziri waliambiwa wakae kando ili uchunguzi uweze kufanywa kuhusiana na masuala ya ufisadi.
view