16 Feb 2022 in Senate:
Bi. Naibu Spika, hizi jumuiya za kaunti zitasaidia kuleta maendeleo karibu kwa mambo yatasaidia kaunti zote mbili. La mwisho ni kwamba, kuna maeneo ambayo yana
view
16 Feb 2022 in Senate:
yaani wana nafasi nzuri. Kwa mfano, Mombasa ambayo ni jiji la bahari na ina bandari ya kimataifa lina nafasi nzuri ya kuleta wafanyi biashara kuliko maeneo mengine ambayo hayana raslimali au mawasiliano kama vile Kaunti ya Mombasa.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Kaunti zote zikiungana pamoja kama jumuiya ya kaunti, kwa mfano Mombasa itapata nafasi kubwa ya kujiimarisha kiuchumi. Miji mingi ambayo ina bandari inaimarika kwa sababu ya biashara ya bandari kwa mfano Rotterdam ilioko Uholanzi wameweza kuimarika kwa sababu ya biashara ya bandari katika eneo hilo. Lakini kwetu, biashara ya bandari iliondolewa ikapelekwa Naivasha dry port ili kuimarisha usafiri wa Standard Gauge Railway (SGR). Hii ilikua ni makosa makubwa kwa sababu ile comparative advantage ambayo bandari ya Mombasa ilikua nayo, kuweza kuleta wafanyibiashara kutoka maeneo yote na kuleta mali kutoka sehemu zote, imepungua sasa na utapata biashara zimefungwa hivyo kuathiri kodi ...
view
16 Feb 2022 in Senate:
Kama kaunti hatuna haja ya kuja kupewa ruzuku ndogo. Bi. Naibu Spika, tumepitisha mfumo mpya wa elimu wa Competency Based
view
16 Feb 2022 in Senate:
(CBC) ambayo watoto wengi wamesonga mbele. Wengi wao wanatumia vipakatalishi au tablets katika masomo yao.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Bi. Naibu Spika, mimi na Sen. Farhiya tuko katika Kamati ya Sheria ya Seneti. Hivi majuzi tulikua tunaangalia kanuni ambazo zimeletwa za irrigation. Sheria ya irrigation ilipitishwa kutoka mwaka wa 2016 au 2017, na hivi sasa ndio tunamaliza kupitisha regulations zao. Kwa hivyo, si makosa. Hata tukiweka kwa sheria kwamba lazima walete regulations kwa muda wa miezi sita, haitawezekana, kwa sababu, lazima wazingatie maswala ya public participation, kuzichambua zile regulations mpaka tuone ziko sawa na mambo ya mashauriano baina ya ofisi ya mkuu wa sheria na wizara yote inachukua muda kiasi ambapo haiwezekani kufanya hivyo kwa miezi sita. Lakini ni ...
view
15 Feb 2022 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili nichangie malalamiko yaliyoletwa na Bi. Julia Difu, kuhusu akina mama ambao mimba zao zimeharibika. Malalamishi hayo yanazungumzia mambo mazito kabisa katika sheria yetu na pia Katiba. Kila Mkenya ana haki ya kupewa huduma za afya za hali ya juu. Mambo ya uzazi ni mojawapo ya vitu muhimu sana katika afya ya binadamu. Kwa hivyo, haki za kina mama wanaojifungua lazima zilindwe. Tumeona kwamba sheria inabagua akina mama wanaojifungua kuchelewa na pia wanaojifungua watoto wasio hai. Swala hili lazima liangaliwe kwa haraka kwa sababu Wakenya wengi, hususan akina mama, wanapoteza haki zao ilhali ...
view
15 Feb 2022 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda kunipa fursa ya kuchangia Mswada huu kuhusu elimu ya watoto wenye mahitaji maalum. Kwanza kabisa nawapa kongole Sen. (Dr.) Musuruve na Sen. (Prof.) Kamar kwa kuleta Mswada huu katika Bunge la Seneti. Maseneta hawa wawili wana tajriba katika mambo ya elimu. Kwa hivyo, Mswada huu ambao wameuleta ni wa muhimu sana kuhusu elimu ya wanafunzi wenye mahitaji maalum. Desemba mwaka jana, Siku ya Watu Wanaoishi na Ulemavu, nilibahitika kutembelea shule ya watoto wenye akili thaathira mjini Mombasa, yani Mombasa School for the Mentally Handicapped. Nilipofika pale, watoto wote walikuwa na furaha kwa sababu walikuwa wameelezwa ...
view
15 Feb 2022 in Senate:
kusoma, vitabu na venginevyo lakini swala muhimu ni kwamba kuwe na fedha za kutosha ambazo zinapelekwa katika tahasisi hizi kuhakikisha kuwa wale watoto wanaosoma pale wanapata elimu ya hali ya juu na mazingira yao yako sawa kuweza kuishi katika eneo lile. Ningependa pia kujiunga na wale wenzangu walikuwa wametangulia kusema kwamba Mswada huu ni mzuri sana kwa masomo ya watoto wenye mahitaji maalum. Kwa hivyo, ni jukumu letu kuona kuwa Mswada huu umepitishwa ili wale watoto ambao wanazaliwa na mahitaji maalum kwa mfano, viziwi, vipofu, bubu, wale ambao akili zao zina tahadhira waweze kupata elimu ambayo itawasaidia maishani mwao na ...
view
27 Jan 2022 in Senate:
Thank you, Madam Deputy Speaker. This is a
view