16 Feb 2022 in Senate:
Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu kuhusu uimarishaji wa rasilimali za kaunti ambao umeletwa Bungeni na Sen. Nyamunga ambaye ni Seneta Maalum. Nadhani Mswada huu umekuja wakati mzuri, japokuwa kulingana na malengo na maazimio yake, ulifaa kupitishwa miaka saba au nane iliyopita, kwa sababu kwa sasa kaunti zetu nyingi zinategemea mgao wa Serikali ili kuendesha miradi yao ya maendeleo. Maendeleo inaweza kufanywa kwa msaada; maendeleo inatakikana kufanywa na rasilimali za kaunti ambazo zinapatikana katika eneo hilo. Mswada huu utasaidia pakubwa kuziwezesha kaunti zetu kuangalia zaidi rasilimali walizonazo kuliko kuomba Seneti kuwaongeza pesa kila mwaka ilhali ...
view
16 Feb 2022 in Senate:
Bi. Naibu Spika, yasikitisha kwamba hatujaweza kupata matunda ya wazo hili la jumuiya ya kaunti za Pwani ijapokuwa sisi katika Pwani tulikuwa wa kwanza katika nchi ya Kenya kuja na fikra kwamba hizi kaunti zinaweza kuungana pamoja zikaweza kuendesha mambo ambayo yatasaidia kaunti zote katika eneo lile.
view
16 Feb 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Kwa mfano, kaunti zote za Pwani zina shida kubwa ya maji. Mombasa inapata maji yake kutoka Mzima Springs ambayo iko karibu kilomita 200 kutoka Kaunti ya Mombasa. Maji mengine yanatoka Baricho ambayo pia ni karibu kilomita 200 kutoka Kaunti ya Mombasa. Baricho iko katika Kaunti ya Kilifi.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Bi. Naibu Spika, ukiangalia Kwale, pia wana shida ya maji. Mombasa, Kilifi, Tana River na Lamu wana shida ya maji. Lakini hatujaweza kuthibiti hii rasilimali ya maji ya Mzima Springs ili kuona kwamba tuna peleka maji maeneo yote katika Kaunti hizi za Pwani. Uzembe wetu ama kulala kwetu, bado tunatarajia Serikali Kuu iweze kutusaidia kuweza kuimarisha rasilimali hii ambayo ni muhimu sana katika maisha ya binadamu. Jambo lingine ambalo pia linatukwaza kule Pwani ni uchumi samawati yaani blue
view
16 Feb 2022 in Senate:
ambayo sasa ndio eneo jipya la kuimarisha uchumi, pia inatupiga chenga. Tukiangalia, tuna ufuo wa bahari kutoka Vanga, nyumbani kwa Mhe. Boy, mpaka Kiunga, upande wa kaskazini katika eneo la Lamu. Utapata ya kwamba ijapokuwa tuna bahari hatuna usafiri wa bahari, kwa mfano kutoka Lamu kwenda mpaka Kwale. Kuna usafiri wa kutoka Shimoni kwenda mpaka kisiwa cha Pemba na Zanzibar. Lakini sisi katika Kenya hatuna usafiri wa kutoka Shimoni mpaka Mombasa ama Kilifi mpaka Mombasa ama Mombasa mpaka Lamu ili kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanapata usafiri wa njia rahisi ambao uko salama. Safari ya Lamu inafanywa zaidi ya magari ambapo ...
view
16 Feb 2022 in Senate:
ambayo yanatoka Kilifi. Kwa hivyo, jiwe lile likitolewa Kilifi, limetozwa kodi na likiingia Mombasa pia linatozwa kodi. Mpaka juzi mahakama ikasitisha kodi ambayo inalipishwa na kaunti ya Mombasa kwa bidhaa kama hizo. Tunaona kwamba bidhaa zetu zinakuwa ghali na mara nyingi tunadidimiza wananchi wetu katika maeneo yale. Kwa mfano, jiwe likitoka Kilifi likifika Mombasa, linalipishwa Kshs60 lakini jiwe likitumiwa Kilifi, halilipishwi zaidi ya Kshs40. Kwa hivyo, tunaona kwamba hizi kodi ambazo zinalipishwa katika kila kaunti kwa mfano rasilimali ama bidhaa ya samaki imetoka Lamu inakuja Mombasa; italipishwa ushuru Lamu, ilipishwe ushuru Kilifi na ilipishwe ushuru Mombasa. Maeneo matatu yanalipisha ushuru ...
view
16 Feb 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
16 Feb 2022 in Senate:
haina haja ya kulipisha kodi. Kama Kwale imeweza kulipisha kodi, Mombasa haina haja ya kulipisha kodi ili wananchi waweze kupata bidhaa kwa urahisi na bei nafuu.
view
16 Feb 2022 in Senate:
Tunasema regional economic blocs, yaani jumuiya za kaunti zinaweza kusaidia pia pakubwa kuweza kuimarisha raslimali ambazo ziko katika maeneo mawili tofauti. Kwa mfano, machimbo ya titanium ina hayo madini ambayo yanachimbwa na kupelekwa soko la nje. Katika maeneo fulani kule Kilifi kuna madini ya titanium ambayo hayajachimbwa. Kutumia ukaribu wa Kilifi na Mombasa utaweza kusaidia pakubwa kuimarisha biashara ya uchimbaji wa madini katika eneo la Kilifi wakati hayo machimbo yatamaliza madini yao.
view