Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1041 to 1050 of 1995.

  • 7 Oct 2021 in Senate: Mhe. Spika, maswala ya ajira ni maswala ambayo yako katika kaunti zote katika Jamhuri yetu ya Kenya. Ijumaa iliyopita tulikuwa Mombasa na Kamati ya Seneti ya Ajira, Maswala ya Wafanyikazi na Huduma za Jamii, ambapo tulikuwa tunachunguza maswala ya kudhulumiwa kwa wavuvi ama mabaharia wa Kenya ambao wanafanya kazi katika meli za Wachina. view
  • 7 Oct 2021 in Senate: Mhe. Spika, hii ni fursa adimu ambayo Wabunge hawa wamepata leo na tunatarajia kwamba watakaporudi Nandi wataweza kutumia ule ujuzi ambao wameweza kupata kuweza kutekeleza majukumu yao kwa njia ambayo ni ya hali ya juu na ya kitaalamu kabisa. Asante, Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii. view
  • 7 Oct 2021 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir! view
  • 7 Oct 2021 in Senate: Mr. Speaker, Sir, the Senator for Nandi County keeps referring to the MCAs of Nandi County Assembly as “my MCAs.” Does he own them? view
  • 6 Oct 2021 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I was uncomfortable with Sen. Mutula Kilonzo rehashing the same arguments that he had during the debate over these regulations. A view
  • 6 Oct 2021 in Senate: has already been proposed by the Senate Minority Leader and we all agreed to it. Sen. Mutula Kilonzo Jnr. does not have to rehash the arguments that he made during the submissions. view
  • 5 Oct 2021 in Senate: Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada huu wa Ushirikiano Baina ya Taasisi za Umma na Waekezaji wa Kibinafsi Katika Miradi ya Maendeleo. Mswada huu umekuja wakati mwafaka kabisa kwa sababu ijapokuwa Serikali imepanga kufanya miradi mingi ya kimaendeleo, miradi mingi imekwema kwa sababu ya ukosefu wa fedha za kutosha. Mswada huu utakapopita utasaidia pakubwa miradi ya maendeleo nchini kwa sababu pesa nyingi ambazo zinahitajika kutekeleza miradi zitapatikana kupitia kwa waekezaji wa kibinafsi. Mpango huu utasaidia kupatikana kwa pesa nyingi ambazo zitatumika kutekeleza miradi na huduma nyingine nchini. Bi. Naibu Spika, tumeona kwamba tayari kuna miradi inayotekelezwa ... view
  • 5 Oct 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 5 Oct 2021 in Senate: Kuna miradi ya nyumba ambayo kupitia kwa ‘affordable housing’ huwa ni nyumba za kiasi za wananchi. Miradi kama hiyo inaweza kufanyika katika kila kaunti. Hata hivyo, pesa zinazohitajika na zile zinazotoka katika Serikali kuu na kupelekwa katika serikali za kaunti kutekeleza miradi ya kawaida hazitoshi. Kwa mfano, kule kwetu Mombasa, kuna Likoni, Changamwe, Hadija na Mzizima estates ambazo zinatekelezwa na waekezaji wa kibinafsi. Jambo hili limezua utata. Kama kungekuwa sheria ya uwazi kama hii tungeweza kujua ni akina nani ambao wamefaidika na miradi hii. Ripoti ingewasilishwa katika Bunge la Kaunti ya Mombasa ili kuhakikisha kuna uwazi katika kutoa zabuni za ... view
  • 5 Oct 2021 in Senate: Bw. Spika wa Muda, Public Private Partnership kwa Kiswahili ni Ushirikiano wa Umma na Waekezaji wa Kibinafsi. Tunajua kuwa lugha ya Kiswahili inakuwa. Nafurahi kuwa uko hapo na utasaidia pakubwa kuweza kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Bunge hili. Lakini pia ningeomba Bunge liajiri mtaalamu mmoja wa lugha ya Kiswahili ili mambo kama haya yaweze kutafsiriwa ili iwe rahisi zaidi kwa wale Wabunge wanaotaka kuongea kwa lugha ya Kiswahili. Asante Mhe. Spika. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus