10 May 2022 in Senate:
Asante Mhe. Spika kwa nafasi hii.
view
23 Mar 2022 in Senate:
Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuambatana na Kanuni 48(1) ya Kanuni Za Kudumu za Seneti kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Barabara na Uchukuzi kuhusu ujenzi wa Mahakama mpya katika Kaunti ya Mombasa. Bi. Naibu Spika, katika Kauli hiyo, Kamati inapaswa kuangazia yafuatayo: (1) Kueleza kilichosababisha jumba hilo la mahakama kuwa na nyufa hata kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Tume ya Mahakama nchini. (2)Kueleza aliyepewa kandarasi ya ujenzi huo na sababu za kutokuwa na usimamizi wa kisawasawa wa kandarasi hiyo. Kueleza japo jumba hilo limeidhinishwa rasmi na kaunti ilhali usalama wa watumiaji wa jumba hilo haujahakikishiwa. ...
view
23 Mar 2022 in Senate:
Asante Bi Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi. Uchaguzi ni gharama kubwa sio kwa serikali pekee yake lakini pia kwa wagombea tofauti ambao wanagombea viti tofauti katika uchaguzi huo. Kuna haja ya kudhibiti matumizi wakati huu wa uchaguzi kwa sababu kuna wengine ambao wako tayari kununua uchaguzi ili sauti ya wale ambao wana haki au wale wanyonge isiweze kusikizwa. Kwa hivyo Mswada huu umekuja wakati muafaka, wakati tunajitayarisha kuenda katika uchaguzi mkuu wa tarehe tisa mwezi wa nane mwaka huu. Itasaidia pakubwa sheria hii ikipitishwa ili kuweka wazi na kudibiti matumizi wakati ...
view
23 Mar 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
23 Mar 2022 in Senate:
Kwa hivyo, naunga mkono sheria hii na ninaomba Maseneta wote waizingatie ili tuweze kuipitisha kwa haraka ili iweze kusaidia na iwe ni mchango mkubwa kuleta uchaguzi ambao utakuwa wa haki na usawa katika inchi yetu. Asante Bi. Naibu Spika.
view
22 Mar 2022 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuleta Hoja ya nidhamu. Mwaka jana, tulileta Taarifa hapa kuhusiana na kutolipwa mishahara kwa wafanyikazi wa Shirika la Posta la Kenya . Taarifa hiyo ilipelekwa kwa Kamati ya Habari, Teknolojia na Mawasiliano. Baadaye, walileta taarifa hapa iliyosema mishahara imelipwa. Hata hivyo, jambo hili limekuwa likirudiwa kila mara. Ninapozungumza hapa leo, miezi mitatu imepita sasa tangu wafanyikazi wote wa Shirika la Posta la Kenya hawajalipwa mishahara. Ni jambo la aibu tena la kusikitisha, kwamba Shirika kama hili ambalo lilikuwa na nguvu na uwezo hapo nyuma, sasa linawadhalilisha na kuwatesa wafanyikazi wake. Sasa ...
view
22 Mar 2022 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, ni swala la kitaifa kwa sababu kwa miezi mitatu, wafanyikazi hawajalipwa. Shirika ninalozungumzia hapa ni la Kiserikali wala sio la mtu binafsi. Kwa hivyo, lazima Serikali ijue na itueleze kwa nini wafanyikazi hao hawajalipwa.
view
22 Mar 2022 in Senate:
Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa ugavi wa raslimali kwa kaunti zetu. Ningependa kupongeza kwa Mswada huu kwa sababu unaongeza kiasi fulani cha pesa kwa serikali za kaunti. Inavyojulikana, kaunti zetu zinaongeza huduma katika
view
22 Mar 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
22 Mar 2022 in Senate:
maeneo yao. Vilevile, miradi wanayoifanya inaanza kukamilika na hivyo kuhitaji pesa nyingi kuweza kutekelezwa kila mwaka. Kwa hivyo, ongezeko la pesa italeta afueni sana kwa kaunti zetu kwa sababu pesa hizo zitasaidia pakubwa katika kurahisisha huduma. Kuna mambo matano ningependa kugusia katika swala hili. La kwanza, kuna pesa za Managed Equipment Services (MES). Hapo nyuma, Kamati yetu ya Seneti iliyochunguza mradi huu ilipata kulikuwa na utepetevu mwingi katika kupeleka hivi vifaa kwenye kaunti zetu. Mpaka sasa, kuna kaunti zingine ambazo hazijaweza kutumia vifaa vile. Uchunguzi nilioufanya ni kwamba ongezeko la Kshs7 bilioni utasaidia kufunga pengo lililoko sababu kandarasi nyingi zinakamilika ...
view