9 Nov 2021 in Senate:
Bi Spika wa Muda, kuna ulinzi wa mashahidi. Kuna watu karibu watatu ambao walichukuliwa kama mashahidi wakati wa vita vya Al-Shabaab. Wote baada ya muda wakaondolewa ulinzi wao na wote wakauliwa. Mmoja alichinjwa katika sehemu ya Marafa kule Malindi. Ipo haja ya kuongeza ufadhili wa ulinzi wa mshahidi. Bila ya kuwalinda mashahidi, kesi nyingi hususan za polisi zitaweza kupotea bila kuwa na mwelekeo wowote. Kitu kingine ambacho ningeweza kuipongeza kamati ni pendekezo lao la kuwa na msaada wa kisaikolojia kwa wale ambao wame athiriwa. Kuna wazazi ambao kwa Kiingerea tunawita “single parents” ambao labda mtoto wake mmoja pekee yake ndiye ...
view
4 Nov 2021 in Senate:
Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa iliyoletwa na Senata wa Narok, Sen. Olekina. Ni wazi kuwa Serikali ya Kenya haina hamu ama haina nderemo ya kupambana na ufisadi. Kwa sababu kutoka Rais alipotoa maagizo kwamba uchunguzi ufanywe kuhusiana na sakata ya Kenya Medical supplies Authority (KEMSA) mpaka sasa hatujaona ripoti yoyote. Tuliambiwa faili ilipelekwa kwa Director of Public Prosecutions (DPP) na ikaregeshwa kufanywa marekebisho na mpaka sasa hakuna yeyote ambaye amepelekwa mahakamani kuhusiana na kashifa hii. Bi Spika wa Muda, wafanyaji kazi wadogo sasa wako hatarini ya kupoteza kazi yao kwa makosa ambayo sio yao. ...
view
4 Nov 2021 in Senate:
Madam Temporary Speaker, I also want to join my colleagues, Sen. Sakaja, Sen. Olekina and Sen. Dullo, to emphasize the fact that when we request for Statements in this House, they are supposed to be acted upon so that we report back to our constituents on what has happened on those Statements. It is not proper for a Statement to be read in this House and then a committee kills it. A petition was brought here by residents of Buxton Estate sometime early this year, but up to now, there is no report. We just have a ping-pong game. They ...
view
4 Nov 2021 in Senate:
Asante Bwana Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati ya Ajira na Huduma za Jamii. Jana nilikatizwa nilipokuwa natoa sababu za kutokuwa na ufahamu baina ya waajiri na wale wafanyi kazi ambao wanatoka hapa Kenya kuenda kufanya kazi kule Saudi Arabia na kwengineko. Lugha ni jambo ambalo linaleta shida baina ya wafanyikazi na waajiriwa wao. Waajiri wengi wanatumia lugha ya Kiarabu na Wakenya wengi wanatumia Kiingereza, Kiswahili na lugha zao za mama. Kwa hivyo, mawasiliano baina ya muajiri na mfanyajikazi wake inakua ni shida. Kitu kingine ni kwamba hakuna mafunzo wanayopewa wale ambao wanasafiri kuenda sehemu ...
view
4 Nov 2021 in Senate:
Nilimjibu nikamwambia, ‘you are the one who was paid to take her there so, why
view
4 Nov 2021 in Senate:
Aliniambia, ‘she complained she was sick and was taken to a public hospital. She
view
4 Nov 2021 in Senate:
hivyo tu. Did we send herfor honeymoon? Of all the girls we have sent, it is only her who is complaining. We dideverything within our capabilities.”
view
4 Nov 2021 in Senate:
Ningependa aniache nimalize kwa sababu akinipa Taarifa---
view
4 Nov 2021 in Senate:
Singependa aniarifu kwa sababu inahitilafiana na mwongozo wangu ambao nimeuweka kuweza kuchangia swala hili. Naipongeza Kamati hii kwa kuja na mapendekezo haya. Wengi wa wale amabo wanapata shida sio kwamba hawawezi kufanya kazi, bali kwa sababu mazingira ya kazi sio mazuri kama walivyokuwa wametarajia. Ni bora kwamba kuwe na njia ambayo ikiwa mtu ameshindwa kufanya kazi, kama ni kurejeshe nauli ya ndege, aruhusiwe kurejesha nauli ya ndege na apewe tiketi yake ya ndege kurudi Kenya. Akifika Kenya familia ama wale wahusika warejeshe pesa ya watu ya ndege. Si kwamba mtu aendelee kuzuiliwa, katika sehemu za Ughaibuni bila ya kuwa na ...
view
3 Nov 2021 in Senate:
Bwana Spika wa Muda, kuna wale ambao wanataka kuongea kwa muda mrefu. Hatuwakatazi kwa sababu ni haki yao ya kidemokrasia katika Bunge hili. Kuna wale ambao wanataka kuongea kwa muda mchache. Kuweza kupata ule uwiano, wale ambao wanataka kuongea kwa muda mchache wapewe nafasi waongee waondoke. Wale wanataka dakika 10 au 20 watamaliza.
view