3 Aug 2021 in Senate:
Kwa hivyo, Mswada huu utaweka mfumo maalum ambao utasaidia kutoza asilimia fulani ya mapato ili waliadhirika na raslimali kama zile wasaidike. Nimefurahi pia kwamba katika Mswada huu, CRA imepewe jukumu la kufanya
view
3 Aug 2021 in Senate:
ya fidia itakayolipwa kwa jamii husika. Hili ni jambo nzuri. Mambo ya faini yamezungumziwa. Ninakubaliana na Seneta wa Kericho kwa kusema kwamba faini ya million mbili ni kidogo sana. Inafaa iwe asilimia fulani ya kiwango cha pesa zinazopatikana na mwekezaji. Kila alichotoa katika eneo lile kiwe ni aslimia fulani ambayo atalipa kama faini iwapo hataweza kutimiza sheria hii. Itajulikana kwamba mtu akikosa, lazima alipe kiwango fulani ili sheria ifuatwe. Iwapo faini hii aitabadilishwa, basi kuwe na kipengeo cha kusema kwamba, mbali na kulipa faini ya million mbili, tano au kumi, lazima alipa faida kwa jamii husika. Bila ya kuzungumza mengi, ...
view
3 Aug 2021 in Senate:
ya fidia itakayolipwa kwa jamii husika. Hili ni jambo nzuri. Mambo ya faini yamezungumziwa. Ninakubaliana na Seneta wa Kericho kwa kusema kwamba faini ya million mbili ni kidogo sana. Inafaa iwe asilimia fulani ya kiwango cha pesa zinazopatikana na mwekezaji. Kila alichotoa katika eneo lile kiwe ni aslimia fulani ambayo atalipa kama faini iwapo hataweza kutimiza sheria hii. Itajulikana kwamba mtu akikosa, lazima alipe kiwango fulani ili sheria ifuatwe. Iwapo faini hii aitabadilishwa, basi kuwe na kipengeo cha kusema kwamba, mbali na kulipa faini ya million mbili, tano au kumi, lazima alipa faida kwa jamii husika. Bila ya kuzungumza mengi, ...
view
29 Jul 2021 in Senate:
Asante Naibu Spika. Ninatoa kauli yangu kuhusiana na ripoti hii. Nimeiangalia kwa mtazamo fagia nanikaona kwamba katika mapendekezo yao, moja nikuwa malalamiko ya walalamishi yarejeshwe katika Wizara pamoja na taasisi nyingine yakachunguzwe. Lakini, wao waliamini kwamba Bunge la Seneti ndio mahali ambapo wataleta malalamishi yao kama hatua yao ya mwisho. Kwa hivyo, mimi sikubaliani na uamuzi huo kwa sababu nikuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
view
29 Jul 2021 in Senate:
Bi. Naibu Spika, Kiswahili kinaendelea kusomwa. Nashukuru, Sen. Mutula Kilonzo Jr., kwa kunikosoa.
view
29 Jul 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
29 Jul 2021 in Senate:
Nimasikitiko kwamba umempa Sen. Kinyua nafasi ya kuongea juu ya hoja ya nidhamu, lakini katika hoja yake, hakuna nidhamu yoyote ambayo imevunjwa. Bi. Naibu Spika, mapendekezo ya Kamati hayaridhishi. Wamekubali kwamba watu walifutwa kazi kinyume cha sheria. Tukiangali Kifungu cha 37 cha Sheria ya Uajiri, mfanyikazi akifutwa kiholela, anafaa kulipwa ridhaa na kama inawezekana arejeshwe kazini. Hawa wamezungushwa mwaka mzima na sasa wameambiwa wapeleke malalamiko yao kwa Wizara yachunguzwe tena. Sisi kama Bunge la Seneti, hatukubali mapendekezo hayo kwa sababu yatailetea kejeli Bunge hili. Kwa hivyo, naomba kama waliotangulia walivyosema kwamba, hii ripoti irudishwe tena kwa Kamati na waweze kutekeleza ...
view
28 Jul 2021 in Senate:
Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa Mchapishaji wa Serikali za Kaunti. Ninauunga mkono kwa sababu umekuja katika wakati mwafaka. Tumeona kutoka ugatuzi uanze karibu miaka nane sasa, tumekuwa na changamoto nyingi za serikali za kaunti kuweza kuchapisha Miswada yao kwa wakati na kuwasilisha stakabadhi muhimu ambazo zinatumika kuendesha Serikali ya nchi.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Kwa mfano, serikali nyingi za kaunti zinapata shida kuwasilisha Miswada yake kwa mchapishaji mkuu wa Serikali na kuchapishwa kwa wakati. Swala la kuchunga sheria lina wakati maalum ambao unatakikana kufanyika. Kwa hivyo, iwapo mchapishaji wa Serikali atachelewea kuchapisha Miswada ile, taratibu zinazotakikana kufuatwa ili Mswada ule uwe sheria unachelewa na kupunguza nafasi ya serikali za kaunti kufanya kazi na kutumikia wananchi wake.
view
28 Jul 2021 in Senate:
Kwa hivyo, kuwepo kwa mchapishaji katika serikali za kaunti utasaidia pakubwa msongamano wa Miswada na notisi katika ofisi ya mchapishaji mkuu wa Serikali. Vile vile, itazipa fursa serikali za kaunti kuwasilisha Miswada yake kwa wakati katika bunge za kaunti na wananchi kujua ni arifa gani zimetolewa kuhusiana na malipo na nyingine muhimu katika maisha yao. Bw. Spika, uwepo wa mchapishaji wa kaunti utasaidia kuelimisha umma katika kaunti zetu. Kupata gazeti ya Serikali rasmi Mombasa inachukuwa wiki moja kutoka Nairobi. Lakini ikichapishwa pale, itapatikana kwa haraka na wananchi watajua ni Mswada au sheria gani zimechapishwa ili wachangie wakati wa mikutano wahusika. ...
view