10 Nov 2021 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
10 Nov 2021 in Senate:
Ahsante sana, Mheshimiwa Spika. Nimemskiza ndugu yangu, Sen. Cheruiyot, na ninashangaa ya kwamba anajaribu kutetea uvunjaji wa sheria. Anasema ya kwamba mtu anaweza akauawa ama kupelekwa mahali pasipo julikana na familia wala wakili wake baada ya kushikwa, kupelekwa mahakamani na mahakama kuamuru ya kwamba hana hatia na hakuna ushahidi wa kutosha kumuhukumu. Hao watu hupotea
view
10 Nov 2021 in Senate:
kiasi ya kwamba hakuna mtu yeyote katika jamhuri ya Kenya ambaye anaweza sema ya kwamba yuko mahala fulani. Tuko katika Bunge, na ni hapa ambapo tunatunga sheria. Hatuwezi tukasema ya kwamba ni haki kwa askari kuchukua mtu. Taasisi ambayo imeundwa na katiba kuangalia kama kuna ushahidi ama la ni mahakama. Mahakama ikisema ya kwamba polisi hawana ushahidi wa kutosha basi hao watu wachunguzwe. Hao watu wataendelea kuchunguza mpaka polisi waone ya kwamba hao sio tishio kwa usalama wa taifa. Sio sawa kusema ya kwamba polisi wako na haki.
view
9 Nov 2021 in Senate:
Asante Bi. Spika kwa kunipa fursa hii ya kuunga mkono Ombi lililo letwa Bunge hili na Sen. Halake. Bi. Naibu Spika, ni wazi kuwa kuna misaada mingi ya kujenga demokrasia katika Kenya. Nchi nyingi za kimagharabi ambazo zinasaidia kukuwa demokrasia wako mbele zaidi ya Kenya katika swala la demokrasia. Kwa hivyo barua ambayo iliandikwa na Katibu katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni kuzuuia balozi kusaidia au kutoa msaada kwa maswala ya demokrasia, haifai kabisa. Tumeona kwa muda mrefu na kwa miaka mingi Serikali imeshindwa kufanya masomo ya uraia yaani civic education kwa sababu pesa ambazo wako nazo hazitoshi
view
9 Nov 2021 in Senate:
kusimamia maswala ya elimu ya uraia. Baadhi ya pesa hizi ambazo zinatoka katika inchi za kigeni, zinatumika kuelimisha Wakenya kuhusiana na maswala la demokrasia. Kwa hivyo, ni makosa kwa Katibu huyu kuandika barua kuzuia balozi kutoa misaada. Hii ni kwa sababu misaada sio pesa pekee. Kuna misaada ya masomo na ya watu kupewa nafasi kusafiri kuenda kuangalia demokrasia nyingine zinafanya vipi. Kwa hivyo, kuzuiliwa kwa misaada hii ni pigo kubwa kwa taifa kwa sababu hatutaweza kusonga mbele kidemokrasia. Tumeona kwamba demokrasia yetu bado inayumba yumba. Hii ni kwa sababu, wakati wa kura ikifika, watu wanashikilia raho zao kwa hofu kwamba ...
view
9 Nov 2021 in Senate:
Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Ripoti ya Kamati ya Haki, Maswala ya Kisheria na Haki za Binadamu ya Seneti kuhusiana na swala la mauaji ya kiholela ya polisi. Hiyo ni pamoja na kupotezwa kwa Wakenya wengi ambao wanaendelea kupotea kila siku kupitia kwa vitengo vya polisi. Kutoka Seneti hii ianze kazi mnamo Mwezi wa Tisa, 2017 kumekuja Taarifa takriban 20 zinazungumzia maswala ya watu kuuliwa kiholela na polisi pamoja na wale ambao wanapotezwa na polisi hao. Bi Spika wa Muda, hata hivi sasa tunavyo zungumza, watu wanaendelea kupotezwa na wengine wanachukuliwa. Kwa mfano, Abdul ...
view
9 Nov 2021 in Senate:
Bi Spika wa Muda, mwingine ambaye amechukuliwa ni kijana anayeitwa Muhamed Abubakar Said ambaye alitekwa nyara mnamo tarehe 14 Oktoba mwaka huu maeneo ya Mombasa karibu na Msikiti wa Musa. Mpaka leo, hajulikani yuko wapi. Mwingine aliyechukuliwa ni Prof. Hassan Nandwa ambaye alichukuliwa tarehe 18 mwezi huu na akachiliwa jana maeneo ya Makueni, mahali ambako alikuwa hajulikani. Kwa hivyo, ni visa ambavyo vinaendelea kila siku. Juzi nilifurahi kwamba mahakama ilitoa amri mpaka zile kumbukumbu za simu zile za Safaricom waliombwa wazilete mahakamani kuonesha vipi mwelekeo wake kutoka alipochukuliwa mpaka pale alipokuwa amefikishwa. Mnamo mwezi wa Nne nafikiri mwaka wa 2019, ...
view
9 Nov 2021 in Senate:
Kiingereza habeas corpus, polisi walikuwa wanapewa masaa 24 kumleta mhusika kortini ama wamuachilie. Lakini sasa mahakama inaweza kutoa amri kwamba aje baada ya siku saba. Kwanza ukipeleka kwa cheti cha dharura, watakuambia kwamba nenda ukapeleke makaratasi kwa Mwanasheria Mkuu ama kwa DPP. Yakipelekwa kwa DPP, akija kortini anasema: “Sijapata maelezo kutoka kwa Inspector General of Police (IG), nipe siku saba, kumi au 23.” Ni njia ya kuaihirisha kesi wakati swala la haki za kibinadamu ni la dharura. Lazima hatua ichukuliwe pale pale. Sheria inawapa polisi masaa 24 kumshika mtu. Ikizidi zaidi ya hapo ni jambo la dharura. Kwa hivyo ni ...
view
9 Nov 2021 in Senate:
Bi Spika wa Muda, kuna ulinzi wa mashahidi. Kuna watu karibu watatu ambao walichukuliwa kama mashahidi wakati wa vita vya Al-Shabaab. Wote baada ya muda wakaondolewa ulinzi wao na wote wakauliwa. Mmoja alichinjwa katika sehemu ya Marafa kule Malindi. Ipo haja ya kuongeza ufadhili wa ulinzi wa mshahidi. Bila ya kuwalinda mashahidi, kesi nyingi hususan za polisi zitaweza kupotea bila kuwa na mwelekeo wowote. Kitu kingine ambacho ningeweza kuipongeza kamati ni pendekezo lao la kuwa na msaada wa kisaikolojia kwa wale ambao wame athiriwa. Kuna wazazi ambao kwa Kiingerea tunawita “single parents” ambao labda mtoto wake mmoja pekee yake ndiye ...
view
4 Nov 2021 in Senate:
Asante Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa iliyoletwa na Senata wa Narok, Sen. Olekina. Ni wazi kuwa Serikali ya Kenya haina hamu ama haina nderemo ya kupambana na ufisadi. Kwa sababu kutoka Rais alipotoa maagizo kwamba uchunguzi ufanywe kuhusiana na sakata ya Kenya Medical supplies Authority (KEMSA) mpaka sasa hatujaona ripoti yoyote. Tuliambiwa faili ilipelekwa kwa Director of Public Prosecutions (DPP) na ikaregeshwa kufanywa marekebisho na mpaka sasa hakuna yeyote ambaye amepelekwa mahakamani kuhusiana na kashifa hii. Bi Spika wa Muda, wafanyaji kazi wadogo sasa wako hatarini ya kupoteza kazi yao kwa makosa ambayo sio yao. ...
view