Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1171 to 1180 of 1995.

  • 6 Jul 2021 in Senate: Asante, Sen. Wetangula. Hatuwezi kuwa na nchi ambayo inafanya mambo kinyumenyume. Yataka tuwe na mikakati dhabiti kupambana na janga la Virusi vya Korona. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Jambo la mwisho ni kuwa wanaosafiri kwenda nchi jirani ya Tanzania kwa sasa, wanatakiwa kuwa na cheti kinachoonyesha kwamba hawana virusi vya Korona. Wakiingia Tanzania kupitia mpaka wa Horohoro, wanalazimishwa kupima tena kwa Dola 25 za Marekani. Sheria inayotumika kwa wanaosafiri kwa ndege ni tofauti na wale wanaosafiri kwa basi. Ina maana kwamba kama nchi, hatuko tayari kupambana na janga hili. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Kama Bunge ni lazima turegeshe ile Kamati ya Virusi vya Korona, ili ipambane na masuala haya siku kwa siku ili kuona kwamba wananchi wetu wanalindwa. Unyanyapaa ndilo swala kubwa linakumba wanaougua au waliopoteza wapendwa wao kutokana na virusi vya Korona. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Mswada huu wa huduma za afya kwa jamii. Mswada huu umekuja katika wakati mwafaka, wakati ulimwengu unapambana na janga la Corona. Ningependa kumpongeza Dr. Zani kwa kuleta Mswada huu katika Bunge kujadiliwa. Mswada huu unatoa fursa kwa sheria kutambua majukumu ya wafanyikazi wa afya ambao wengi wamejitolea kuhakikisha kwamba wananchi kule mashinani wanapata huduma za afya, wengine hata bila malipo. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Ukiangalia kwa mfano wakunga wale wanaozalisha akina mama wakati wanajifungua, wale ngariba ambao wanapasha tohara wakati vijana wanatiwa jandoni, wengine sasa wanatoa huduma kwa wenye magonjwa kama vile Saratani, kisukari na magonjwa mengi ambayo ni gharama kubwa kupeleka mgonjwa katika zahanati ama hospitali ya kisasa kuweza kupata huduma kama hii. Ugonjwa kama Saratani kwa mfano, umeingia katika vijiji vyetu na wengi wanapata huduma kwa wale ambao ni wafanyikazi wa jamii. Mswada huu utasaidia pia pakubwa kuweza kupambana na mikurupuko ya maradhi tofauti, kwa mfano mikurupuko ya maradhi kama kipindupindu, bilharzia na mengineo ambayo hutokea vijijini ambayo inabidi wananchi watembee safari ... view
  • 6 Jul 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: iwapo sheria hii itapita huduma za matibabu zitakuja mashinani, madawa yataweza kupatikana mashinani na vile vile huduma kama vile za X-ray na vipimo za damu zitaweza kupatikana kwa njia rahisi ili kuhakikisha kwamba wananchi wanatibiwa kwa gharama isiyokuwa kubwa. Vile vile, zile stakabadhi ambazo zitapatikana katika kijiji kile itasaidia pakubwa pia kupanga mikakati ambayo itasaidia pakubwa kuboresha huduma za afya katika maeneo hayo na afya ya wananchi katika zile sehemu ambazo zimelengwa. Kwa hivyo, Mswada huu utachangia pakubwa afya katika nchi yetu na katika kaunti zetu. Vile vile, itasaidia kuhakikisha kwamba kuna afya kwa wote katika nchi yetu ya Kenya. ... view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Bw. Spika wa Muda, naomba Maseneta wenzangu waunge mkono Mswada huu ili kuhakikisha kuwa tuna sheria ya msingi ambayo itatambua kazi ambazo zimekuwa zikifanywa kutoka jadi. Kama nilivyosema awali, kuna watu kama vile wakunga wa kuzalisha kina mama, ngariba wa kupasha watoto tohara na wale ambao wanahudumia wananchi ambao wameathirika na ugonjwa kama vile ukimwi. view
  • 6 Jul 2021 in Senate: Wengi wa waathiriwa wa ukimwi wanahudumiwa nyumbani kwao. Wale wanaofanya kazi hiyo ni watu wanaojitolea kufanya kazi bila malipo. Kwa hivyo, Mswada huu utasaidia pakubwa kuwaweka katika hali ya kuridhisha kikazi na vile vile kihuduma kwa wananchi wetu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus