3 Dec 2024 in Senate:
Ni lazima pia tumpe kongole kwa uamuzi huo ama jukumu hilo ambalo alichukua yeye binafsi kupendekeza kwa mkurugenzi wa Benki Kuu wakati huo, kuandisha Mpesa kama njia moja ya kutuma pesa. Mpesa imeweza kusambaa ulimwengu mzima hivi sasa. Kila sehemu matumizi ya pesa kwa njia ya Dijitali yanazidi kukua. Kuna mambo mengi mapya ambayo yanahitajika kuingia kwenye mfumo wetu wa fedha. Haya yote, tuna imani kwamba Bw. Nyaoma atasaidia pakubwa kuhakikisha kwamba hizi mbinu za biashara na fedha kama
view
3 Dec 2024 in Senate:
zitatumika ili kupanua uchumi wetu. Soko la fedha likipanuka ina maana kwamba uchumi wetu pia utapanuka na itakuwa ni faida kwa Wakenya ambao wanastahili kupata huduma hizi ambazo ziko sehemu nyingi za ulimwengu. Vilevile Wakenya waweze kuzitumia waone kwamba fedha zao zinakua. Kwa hayo mengi, naunga mkono ripoti hii.
view
26 Nov 2024 in Senate:
On a point of order, Mr. Temporary Speaker, Sir.
view
26 Nov 2024 in Senate:
Mr. Temporary Speaker, Sir, I have heard the distinguished Senator from Kakamega County repeatedly saying, ‘standing obviation’. I know he is a gynaecologist, but it is standing ovation. There is a difference between obviation and ovation.
view
26 Nov 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, aliyekua Seneta na Waziri wa Kilimo, Mhe. Linturi, hakutimuliwa katika Bunge. Mswada wa kumuondoa mamlakani ulishindwa katika Bunge la Taifa. Kwa hivyo, si sawa kwa Mhe. Mundigi kusema kwamba alitimuliwa. Angalia HANSADI.
view
26 Nov 2024 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Rais ya Hali Halisi ya Taifa iliyotolewa mnano tarehe 21.11.2024 kuambatana na Kifungu Cha 132(1) ( C) cha Katiba yetu. Ninampongeza Rais kwa kutekeleza jukumu hili la kikatiba ambalo ni muhimu sana la kujuza Bunge kwa mujibu wa Katiba. Bw. Spika wa Muda, ni masikitiko kwamba katika Hotuba yake, Rais hakuzungumzia maswala ya ugatuzi. Hotuba yake yote haikugusia maswala ya serikali za kaunti ambazo ni kiungo muhimu katika nchi yetu. Ikumbukwe kwamba tulikuwa na mvutano kuhusu Division of Revenue Bill ambapo mpaka wiki iliyopita ndipo Kamati ya Uwiano ...
view
26 Nov 2024 in Senate:
nyara na mwishowe kupatikana wameuawa. Wengi wa waliouawa ni vijana ambao walishiriki katika maandamano ya Gen Z. Vile vile, tulitarajia Rais kuzungumzia tuhuma ambazo Gen Z walikuwa nazo wakati walipokuwa wanaandamana hadi kwenye Bunge hili mwezi wa sita mwaka huu. Hata hivyo, Rais hakugusia hayo. Kwa hivyo, ni wazi kwamba Rais pamoja na washauri wake hawasikii wala kufuata mambo mengi ambayo yanaathiri Wakenya. Ijapokuwa Kenya yetu ni democrasia, maswala ya mauaji ya kiholela, utekajinyara, na ukandamizaji wa haki za kibinadamu kupitia mambo kama vile mauji na mengineyo yanatia doa nchi yetu kwa sababu Kenya ni mwanachama wa Community ofNations . ...
view
26 Nov 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Temporary Speaker, Sir. I beg to lay the following Paper on the Table of the Senate today, 26th November, 2024 - The report of the Mediation Committee on the Division of Revenue Amendment Bill 2024(National Assembly Bill No.38 of 2024), on behalf of the co-chair of the Mediation Committee. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate.
view