10 Jul 2024 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia Ripoti ya Kamati ya Sheria Endelezi ya Bunge la Seneti katika kuchunguza na kuidhinisha Kanuni za Sheria ya Afya ya Kijamii, zilizoletwa hapa Bungeni na zilizochapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali namba 492004 na 482004. Ningependa kuipongeza Kamati hii ikiongozwa na Sen. Mwenda Gataya Mo Fire kwa umaahiri wake kuchunguza kanuni kama hizi. Kamati ilifanya kazi sana na ikampa Waziri muda wa kutosha kuja kwa Kamati ili kuidhibitishia kwamba alifuata sheria ambazo zinahusika katika kutengeneza sheria kama hizi. Inafaa ieleweke kwamba kwanza, ile haki ya Waziri kutengeneza kanuni kama hizi ...
view
10 Jul 2024 in Senate:
iwapo sheria mama, itakinzana na kanuni, basi sheria mama ndiyo huwa inachukua kipau mbele kwa sababu imetungwa na wale waakilishi wa wananchi, moja kwa moja. Bw. Spika wa Muda, jambo la nne ni kuwa Wizara ama jopo husika lililotayarisha maswala haya ama kanuni hizi halikuweza kupambanua maswala fulani yaliyo muhimu katika maswala haya. Kwa mfano, halikuweza kupambanua mfumo wa mchango wa kila mwaka kwa kila familia. Haikuweza pia kuchanganua majukumu ya Serikali kuu na yale ya serikali za kaunti na vile vile, mambo mpito yanayotakikana kuzumgumziwa katika sheria kama hii. Tunapozungumzia mambo mpito ni kwamba, tumetoka katika sheria ya NHIF ...
view
10 Jul 2024 in Senate:
. Kwa hivyo, ni lazima sheria iregeshwe na ichunguzwe tena upya ili iambatane na sheria na zile kanuni zimewekwa kulingana na sheria zilizopitishwa na Bunge hili. Katika Kamati hii ya sheria endelezi, kuna mfumo tunaotumia kwa sasa ambao unampa yule aliyetengeneza kanuni fursa ya kuja mbele ya Kamati kueleza mapendekezo ambayo anataka kuyapeleka. Kamati pia inamshauri vile atakavyofanya ili kuhakikisha kwamba, akileta zile kanuni baada ya kuchapishwa kwa Gazeti Rasmi, haziwezi kukataliwa. Kuna wizara nyingi zilizokubali mfumo huo, lakini masikitiko ni kuwa Waziri wa Afya hakuihusisha kamati kikamilifu katika masuala haya ili iweze kupambanua mambo yanayotakiwa kurekebishwa. Hii ingewezesha kanuni ...
view
10 Jul 2024 in Senate:
Kwa hiyo, kanuni hizi hazitatufaa kusaidia ile azma ya Serikali kuona kwamba wananchi wanapata afya bora kulingana na ruwaza yetu ya mwaka 2030 inavyosema. Naunga mkono kamati hii. Hizi kanuni zitupiliwe mbali. Mhe. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii.
view
10 Jul 2024 in Senate:
Yes, Mr. Temporary Speaker, Sir.
view
10 Jul 2024 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kwanza, ningependa kusema haikuwa nidhamu kwa Seneta wa Migori kujaribu kukata laini tukiwa hapa tunasubiri kama Maseneta tuliomtangulia katika Bunge hili. Pili, naunga mkono Hoja ya kupeleka vikao ya Seneti katika Kaunti ya Busia. Nilikuwa katika vikao vya kwanza vya Uasin Gishu, Eldoret kisha tukaenda Kitui na majuzi, Turkana. Vikao hivi vinapeleka Bunge kwa watu. Ukiangalia sehemu nyingi, serikali ni gavana na labda county commissioner. Tunapozuru maeneo haya na kuweka vikao inaeleza taasira kwamba serikali sio gavana na county commissioner pekee. Serikali ina vitengo vingi ambavyo vinapaswa kupeleka huduma mashinani. The electronic version of the Senate ...
view
10 Jul 2024 in Senate:
Kama Sen. Cheruiyot, Kiongozi wa Wengi, alivyotangulia kusema, tulipoenda Kitui wakati tulipokuwa katika Kamati ya Sheria ikiongozwa na Sen. Cherarkey, tulizuru Gereza la Kitui tukapata kuwa wananchi wengi wamewekwa rumande kwa makosa madogo ambayo wengine walihitaji Shilingi elfu tatu pekee ili wapate bond waweze kuenda nyumbani na kusubiri kesi zao kusikizwa. Sisi kama Maseneta tuliokuwa pale tulichanga na kuwatoa watu karibu 100 siku hiyo. Nimesahau jina la jaji aliyekuwa anahudumu katika Kaunti ya Kitui lakini alikuwa amehudumu Mombasa pia. Aliweza kupitisha faili zote za wale watu waliokuwa jela na baadaye karibu wafungwa wengine 100 walioweza kutoka jela baada ya hukumu ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, having read the Petition, I am seeking your indulgence to allow me to comment on it. If you will allow me, three minutes will be adequate for me.
view