Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1201 to 1210 of 1995.

  • 17 May 2021 in Senate: On a point of order, Mr. Speaker, Sir. I beg to move that we proceed to hear the Governor, unless any Member has a burning issue to debate. view
  • 17 May 2021 in Senate: Asante sana, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia ripoti ambayo imeletwa na Kamati Teule kuhusiana na kuondolewa mamlakani kwa Gavana wa Wajir. Kwanza Kabisa ningependa kuipongeza Kamati hii kwa kuweza kuja na ripoti ambayo imekubalika na wanachama wote wa Kamati. Ni nadra sana kuweza kupata Wanakamati kukubaliana na masuala ambayo yamewekwa mbele yao. Kwa hivyo, naipongeza Kamati ambayo inaongozwa na wakili Seneta Okong’o Omogeni pamoja na wanachama wote ambao walikuwa wakihudumu katika Kmati hiyo. view
  • 17 May 2021 in Senate: Bw. Spika, jambo la pili ni kuipongeza Bunge ya Kaunti ya Wajir kwa kuweza kufanya uchunguzi na kuleta mashtaka haya mbele ya Kamati na Bunge la Seneti, na wakaweza kudhibitisha. Ijapokuwa wameweza kudhibitisha shtaka moja peke yake. Bw. Spika nimeipitia ripoti hii kwa mtazamo fagia, yaani kwa haraka haraka, na nimeona kwamba baadhi ya yale mashtaka ambayo yaliweza kuwasilishwa mbele ya Bunge hili yaliweza kudhibitishwa ijapokuwa Kamati iliweza kuwa na uamuzi tofauti. Mashtaka yote ambayo yalifikishwa mbele ya Bunge la Seneti ni mashtaka ambayo ni magumu sana ama ni serious sana, kiasi ambacho kinaweza kumpeleka nyumbani gavana wa Wajir. Tukiangalia ... view
  • 17 May 2021 in Senate: matumizi ya rasilimali za fedha za Bunge la Kaunti ya Wajir kinyume na vifungu vya 201(a) na 183 vya Katiba yetu na sheria ya 149 and 169 vya Public Finance Management(PFM) Act, 2012. Ijapokuwa mashtaka haya hayakuweza kuthibitishwa, ni wazi kwamba ushahidi ulikuwapo wa kuhukumu au kupata na hatia Gavana huyu kuhusiana na swala hilo. view
  • 17 May 2021 in Senate: Bw. Spika, shtaka la pili lilikuwa linahusu uajibikaji; ukosefu wa uajibikaji juu ya matumizi ya rasilmali za Kaunti ya Wajir na vile kushindwa kuwajibika kutoa hesabu za fedha kiasi cha bilioni mbili zilizotumika kama madeni ambayo yamelimbukizwa. Shtaka la tatu dhidi ya Gavana huyo ni kushindwa kupeleka Medium Term Strategy (MTS) ya mwaka wa 2020/2021. Shtaka hilo lilipelekwa katika Bunge la Kaunti la Wajir mwezi wa tatu. Ni wazi kwamba shtaka hilo limethibitishwa mbele ya Kamati Teule. view
  • 17 May 2021 in Senate: Gavana wa Kaunti ya Wajir pia alishtakiwa kwa kosa la kukiuka vifungu 176(i) na 185 vya katiba. Maelezo ni kuwa Gavana alipuuza Bunge la Kaunti la Wajir katika kupeleka rasilmali zinazofaa katika bunge hilo la kaunti. Ni wazi kwamba PublicFinance Management (PFM) Act, 2012 inasema kwamba fedha za serikali ya kaunti na fedha za bunge la kaunti zinafaa kuwekwa tofauti lakini kufikia sasa, mabunge mengi ya kaunti yanategemea ruzuku kutoka serikali za kaunti. Fedha hizo hutolewa siku ambayo gavana au waziri wa fedha wa kaunti ile anapopenda. Nilihudumu katika kamati ya uhasibu la bunge hili. Tulishuhudia tukio hilo katika kaunti ... view
  • 17 May 2021 in Senate: Bw. Spika, pia kulikuwa na shtaka la kukosa kuteuwa kamati ya County Budget view
  • 17 May 2021 in Senate: kinyume na Kifungu cha 187 cha Public Finance Management(PFM) Act, 2012 . Ingawa shtaka hilo halikuweza kuthibitishwa na Kamati Teule, ilikuwa wazi kwamba hapakuwa na taratibu zilizowekwa kutekeleza kifungu hicho cha sheria. Sheria inasema kuwa kamati hiyo inafaa kuteuliwa haraka iwezekanavyo. Gavana huyu alichaguliwa mwezi wa nane mwaka wa 2017. Sasa tuko mwezi wa nne mwaka wa 2021. Takriban miaka minne zimepita, Gavana huyu akihudumu bila kamati hiyo muhimu kulingana na sheria. view
  • 17 May 2021 in Senate: Shtaka lingine dhidi ya Gavana huyu ni kuwa alikosa kutoa taarifa rasmi kwa Bunge la Kaunti ya Wajir kupitia county address . Hiyo ni moja kati ya mambo muhimu kwa sababu ile hotuba gavana anayotoa kwa bunge la kaunti, Gavana hutoa mwongozo wa mambo anayotarajia kufanya katika mwaka ule. Ni muhimu kwa magavana kutoa hotuba hiyo ili kuhakikisha kwamba wabunge wote wa bunge la kaunti wana uelewano kwamba sheria zote zitakazoletwa katika bunge lao mwaka ule zitakuwa za mtazamo gani. Swala hilo pia halikuweza kuthibitishwa na Kamati Teule. view
  • 17 May 2021 in Senate: Bw. Spika, vile vile kulikuwa na shtaka la kukosa kuthibitisha kupeleka katika bunge la kaunti ripoti ya mwaka kuhusiana na utekelezaji wa sera na mipango ya baadaye. Hili pia ni jambo muhimu kwa serikali zetu za kaunti kwa sababu zinaipa fursa mabunge hayo kujua ni mambo gani serikali za kaunti zinaweza kufanya na njia ambazo wananchi wataweza kuchangia maswala yale. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus