17 May 2021 in Senate:
Kwa muktasari, hayo ndio mambo ambayo nimeweza kupitia katika ripoti hii. Kamati Teule imethibitisha kwamba shtaka moja limeweza kuthibitishwa. Hii ina maana kwamba sisi kama Maseneta, tunapaswa kukubaliana na ripoti ya Kamati hiyo kwa
view
17 May 2021 in Senate:
sababu wameweza kuthibitisha kwamba kumekuwa na ubadhirifu wa fedha katika Kaunti ya Wajir kiasi ya kukosekana baadhi ya huduma za afya katika kaunti ile.
view
17 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, tumesema mara kwa mara katika bunge hili kwamba afya ni huduma muhimu ambayo inafaa kutolewa kwa usawa kwa wananchi katika kaunti zetu. Kumekuwa na ubadhirifu wa fedha za COVID-19 takriban kaunti zote 47 katika Jamhuri yetu ya Kenya. Tumeona kwamba ukosefu wa huduma za afya hususan katika kaunti zilizo mbali na miji mikuu kama kaunti ya Wajir ilioko mbali na miji mikuu. Wakaazi wa Kauti ya Wajir hulazimika kusafiri kwa muda mrefu ili waweze kupata hudum za afya ikilinganishwa na kaunti za mjini kama Nairobi, Mombasa na Kisumu.
view
17 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, swala kuu ni kwamba, je, hili swala hilo moja lilothibitishwa, laweza kumpata gavana wa Kaunti ya Wajir na hatia ya kumwondoa mamlakani? Ndio, kwa sababu Gavana hakuweza kutekeleza majukumu yake kulingana na sheria ambayo imewekwa nchini. Maseneta wengine wamejadili kwamba makosa kama hayo yapo pia katika serikali ya kitaifa. Seneta wa Nandi alisema kwamba hata Mhe. Mutahi Kagwe, Waziri wa Afya katika Serikali ya Kitaifa pia anafaa kutolewa ofisini lakini swala ni kwamba hata yeye anaweza kuleta hoja hapa bungeni na ikithibitishwa, pia Mhe. Kagwe ataenda nyumbani.
view
17 May 2021 in Senate:
Bunge la Kaunti ya Wajir wameweza kusema na kutenda. Wameleta mashtaka katika Bunge hili na mashtaka hayo yameweza kuthibitishwa. Bunge hili halina budi ila kumpeleka gavana wa Kaunti ya Wajir nyumbani ili aende akafanye mambo mengine.
view
17 May 2021 in Senate:
Mwisho ni kwamba tumeona uhuru wa bunge la kaunti ya Wajir. Tungependa kuona mabunge yote 47 katika Jamhuri ya Kenya yakiwa na uhuru wa bunge la Kaunti ya Wajir kwani hilo ndilo litasaidia wananchi kutekeleza ugatuzi katika nchi yetu. Hatuwezi kuwa na mabunge ya kaunti ambayo mara nyingi yako kitandani na magavana. Hiyo ni kurejesha nyuma maazimio ya wale ambao walileta ugatuzi katika nchi yetu ya Kenya.
view
17 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, naunga mkono ripoti hii. Bila shaka, nitapiga kura ya kumpeleka gavana huyu nyumbani. Asante sana.
view
17 May 2021 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia ripoti ambayo imeletwa na Kamati Teule kuhusiana na kuondolewa mamlakani kwa Gavana wa Wajir. Kwanza Kabisa ningependa kuipongeza Kamati hii kwa kuweza kuja na ripoti ambayo imekubalika na wanachama wote wa Kamati. Ni nadra sana kuweza kupata Wanakamati kukubaliana na masuala ambayo yamewekwa mbele yao. Kwa hivyo, naipongeza Kamati ambayo inaongozwa na wakili Seneta Okong’o Omogeni pamoja na wanachama wote ambao walikuwa wakihudumu katika Kmati hiyo.
view
17 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, jambo la pili ni kuipongeza Bunge ya Kaunti ya Wajir kwa kuweza kufanya uchunguzi na kuleta mashtaka haya mbele ya Kamati na Bunge la Seneti, na wakaweza kudhibitisha. Ijapokuwa wameweza kudhibitisha shtaka moja peke yake. Bw. Spika nimeipitia ripoti hii kwa mtazamo fagia, yaani kwa haraka haraka, na nimeona kwamba baadhi ya yale mashtaka ambayo yaliweza kuwasilishwa mbele ya Bunge hili yaliweza kudhibitishwa ijapokuwa Kamati iliweza kuwa na uamuzi tofauti. Mashtaka yote ambayo yalifikishwa mbele ya Bunge la Seneti ni mashtaka ambayo ni magumu sana ama ni serious sana, kiasi ambacho kinaweza kumpeleka nyumbani gavana wa Wajir. Tukiangalia ...
view
17 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, shtaka la pili lilikuwa linahusu uajibikaji; ukosefu wa uajibikaji juu ya matumizi ya rasilmali za Kaunti ya Wajir na vile kushindwa kuwajibika kutoa hesabu za fedha kiasi cha bilioni mbili zilizotumika kama madeni ambayo yamelimbukizwa. Shtaka la tatu dhidi ya Gavana huyo ni kushindwa kupeleka Medium Term Strategy (MTS) ya mwaka wa 2020/2021. Shtaka hilo lilipelekwa katika Bunge la Kaunti la Wajir mwezi wa tatu. Ni wazi kwamba shtaka hilo limethibitishwa mbele ya Kamati Teule.
view