Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1221 to 1230 of 1995.

  • 17 May 2021 in Senate: Gavana wa Kaunti ya Wajir pia alishtakiwa kwa kosa la kukiuka vifungu 176(i) na 185 vya katiba. Maelezo ni kuwa Gavana alipuuza Bunge la Kaunti la Wajir katika kupeleka rasilmali zinazofaa katika bunge hilo la kaunti. Ni wazi kwamba PublicFinance Management (PFM) Act, 2012 inasema kwamba fedha za serikali ya kaunti na fedha za bunge la kaunti zinafaa kuwekwa tofauti lakini kufikia sasa, mabunge mengi ya kaunti yanategemea ruzuku kutoka serikali za kaunti. Fedha hizo hutolewa siku ambayo gavana au waziri wa fedha wa kaunti ile anapopenda. Nilihudumu katika kamati ya uhasibu la bunge hili. Tulishuhudia tukio hilo katika kaunti ... view
  • 17 May 2021 in Senate: Bw. Spika, pia kulikuwa na shtaka la kukosa kuteuwa kamati ya County Budget view
  • 17 May 2021 in Senate: kinyume na Kifungu cha 187 cha Public Finance Management(PFM) Act, 2012 . Ingawa shtaka hilo halikuweza kuthibitishwa na Kamati Teule, ilikuwa view
  • 17 May 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 17 May 2021 in Senate: wazi kwamba hapakuwa na taratibu zilizowekwa kutekeleza kifungu hicho cha sheria. Sheria inasema kuwa kamati hiyo inafaa kuteuliwa haraka iwezekanavyo. Gavana huyu alichaguliwa mwezi wa nane mwaka wa 2017. Sasa tuko mwezi wa nne mwaka wa 2021. Takriban miaka minne zimepita, Gavana huyu akihudumu bila kamati hiyo muhimu kulingana na sheria. view
  • 17 May 2021 in Senate: Shtaka lingine dhidi ya Gavana huyu ni kuwa alikosa kutoa taarifa rasmi kwa Bunge la Kaunti ya Wajir kupitia county address . Hiyo ni moja kati ya mambo muhimu kwa sababu ile hotuba gavana anayotoa kwa bunge la kaunti, Gavana hutoa mwongozo wa mambo anayotarajia kufanya katika mwaka ule. Ni muhimu kwa magavana kutoa hotuba hiyo ili kuhakikisha kwamba wabunge wote wa bunge la kaunti wana uelewano kwamba sheria zote zitakazoletwa katika bunge lao mwaka ule zitakuwa za mtazamo gani. Swala hilo pia halikuweza kuthibitishwa na Kamati Teule. view
  • 17 May 2021 in Senate: Bw. Spika, vile vile kulikuwa na shtaka la kukosa kuthibitisha kupeleka katika bunge la kaunti ripoti ya mwaka kuhusiana na utekelezaji wa sera na mipango ya baadaye. Hili pia ni jambo muhimu kwa serikali zetu za kaunti kwa sababu zinaipa fursa mabunge hayo kujua ni mambo gani serikali za kaunti zinaweza kufanya na njia ambazo wananchi wataweza kuchangia maswala yale. view
  • 17 May 2021 in Senate: Kwa muktasari, hayo ndio mambo ambayo nimeweza kupitia katika ripoti hii. Kamati Teule imethibitisha kwamba shtaka moja limeweza kuthibitishwa. Hii ina maana kwamba sisi kama Maseneta, tunapaswa kukubaliana na ripoti ya Kamati hiyo kwa sababu wameweza kuthibitisha kwamba kumekuwa na ubadhirifu wa fedha katika Kaunti ya Wajir kiasi ya kukosekana baadhi ya huduma za afya katika kaunti ile. view
  • 17 May 2021 in Senate: Bw. Spika, tumesema mara kwa mara katika bunge hili kwamba afya ni huduma muhimu ambayo inafaa kutolewa kwa usawa kwa wananchi katika kaunti zetu. Kumekuwa na ubadhirifu wa fedha za COVID-19 takriban kaunti zote 47 katika Jamhuri yetu ya Kenya. Tumeona kwamba ukosefu wa huduma za afya hususan katika kaunti zilizo mbali na miji mikuu kama kaunti ya Wajir ilioko mbali na miji mikuu. Wakaazi wa Kauti ya Wajir hulazimika kusafiri kwa muda mrefu ili waweze kupata hudum za afya ikilinganishwa na kaunti za mjini kama Nairobi, Mombasa na Kisumu. view
  • 17 May 2021 in Senate: Bw. Spika, swala kuu ni kwamba, je, hili swala hilo moja lilothibitishwa, laweza kumpata gavana wa Kaunti ya Wajir na hatia ya kumwondoa mamlakani? Ndio, kwa sababu Gavana hakuweza kutekeleza majukumu yake kulingana na sheria ambayo imewekwa nchini. Maseneta wengine wamejadili kwamba makosa kama hayo yapo pia katika serikali ya kitaifa. Seneta wa Nandi alisema kwamba hata Mhe. Mutahi Kagwe, Waziri wa Afya katika Serikali ya Kitaifa pia anafaa kutolewa ofisini lakini swala ni kwamba hata yeye anaweza kuleta hoja hapa bungeni na ikithibitishwa, pia Mhe. Kagwe ataenda nyumbani. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus