Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1231 to 1240 of 1995.

  • 17 May 2021 in Senate: Bunge la Kaunti ya Wajir wameweza kusema na kutenda. Wameleta mashtaka katika Bunge hili na mashtaka hayo yameweza kuthibitishwa. Bunge hili halina budi ila kumpeleka gavana wa Kaunti ya Wajir nyumbani ili aende akafanye mambo mengine. view
  • 17 May 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 17 May 2021 in Senate: Mwisho ni kwamba tumeona uhuru wa bunge la kaunti ya Wajir. Tungependa kuona mabunge yote 47 katika Jamhuri ya Kenya yakiwa na uhuru wa bunge la Kaunti ya Wajir kwani hilo ndilo litasaidia wananchi kutekeleza ugatuzi katika nchi yetu. Hatuwezi kuwa na mabunge ya kaunti ambayo mara nyingi yako kitandani na magavana. Hiyo ni kurejesha nyuma maazimio ya wale ambao walileta ugatuzi katika nchi yetu ya Kenya. view
  • 17 May 2021 in Senate: Bw. Spika, naunga mkono ripoti hii. Bila shaka, nitapiga kura ya kumpeleka gavana huyu nyumbani. Asante sana. view
  • 11 May 2021 in Senate: Asante Bw. Spika kwa fursa hii ya kuchangia Mswada wa Marekebisho ya Katiba ulioletwa katika Seneti. Kwanza, ningependa kuwapongeza waasisi wa Mswada huu kwa kutupa fursa ya kurekebisha Katiba yetu wakati tuna amani na hakuna msukosuko wowote katika Jamhuri ya Kenya. view
  • 11 May 2021 in Senate: Katika Kifungu cha kwanza cha Katiba yetu kinasema kwamba uwezo umepewa wananchi, na uwezo huo unafaa kutekelezwa kulingana na Katiba. Nguvu zote zimerejeshwa kwa wananchi, na nguvu zile zinafaa kutekelezwa kulingana na vile Katiba inavyoamrisha. Kifungu cha pili kinasema kuwa hakuna mtu wala taasisi yoyote ya Serikali inaweza kutekeleza jukumu lolote kama haijaruhusiwa na Katiba. Kwa hivyo, Katiba ndiyo mwanzo wa kila kitu katika sheria zetu. Kifungu cha 94 kinasema kuwa uwezo wa kutunga sheria umekabidhiwa Bunge. Hakuna taasisi isipokuwa Bunge inayo uwezo wa kutunga sheria ya kitaifa. Katika kutazama marekebisho haya, ni jukumu la Bunge kuangalia kwa undani kabisa, ... view
  • 11 May 2021 in Senate: Bw. Spika, vifungu ambavyo vinaangazia marekebisho ya Kabtiba vinaanzia 255 hadi 257. Kifungu cha 257 kinazungumzia kurekebisha Katiba kupitia popular initiative. Kifungu cha 257 kinasema kwamba ikiwa moja kati ya Nyumba mbili za Bunge itakataa kupitisha Katiba hii--- Marekebisho yanayoambatana na Kifungu 251(1) ni lazima yafanyiwe kura ya maoni, yaani referendum. view
  • 11 May 2021 in Senate: Iwapo tutapitisha ama tutakataa, ni lazima marekebisho haya yaende kwa wananchi kupitia kura ya maoni, kwa sababu ni mambo ambayo tunataka kurekebisha, na yanaingia katika msingi wa Bunge. Sisi kama Bunge tuna jukumu muhimu katika swala hili. view
  • 11 May 2021 in Senate: Katika kufanya haya marekebisho, ni lazima kuwa Bunge, ambalo ndilo taasisi inayotunga sheria katika Jamhuri ya Kenya, ichunguze yale marekebisho kuhakikisha kuwa yanaambatana na sheria. Iwapo haiambatani na Katiba, tuyarekebishe ili tuwe na Katiba inayoambatana na Katiba ilioko sasa. Hatuwezi kusema kwamba Bunge iwe mshangiliaji katika marekebisho haya. view
  • 11 May 2021 in Senate: Bw. Spika, nikizingatia yale marekebisho yanayotakinana, lengo na madhumuni ni malengo mazuri. Kwa mfano, lengo la--- view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus