26 May 2020 in Senate:
Shule nyingi ambazo ziko katika maeneo ya mashambani zimesahaulika kivifaa na kiwalimu. Katika shule hizo matokeo ya mitihani ya kitaifa huwa si bora. Taarifa hii imeletwa katika wakati muafaka. Suala hili haliko Kitui pekee yake, liko katika sehemu nyingi ambazo waalimu kama hao wamenyimwa vyeo na marupurupuru yao. Aidha marupurupu wanayopata hayaambatani na vyeo hivyo. Kwa hivyo, hamu yao ya kufanya kazi haipo.
view
26 May 2020 in Senate:
Iwapo suala hilo halitachunguzwa vizuri ina maana kwamba nchi nzima wanafunzi watapata hasara kwa sababu walimu wanaowasomesha hawana motisha. Naomba kamati ambayo itashughulikia suala hili iingilie ndani na isisimame Kitui pekee, bali Kenya nzima ili liweze kutatuliwa mara moja.
view
26 May 2020 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono ripoti ya sita ya Kamati maalum ya COVID-19. Kwanza, ningependa kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati hii. Tumeweza kufanya mikutano zaidi ya 55 kwa muda mchache. Katika mikutano hiyo yote walihudhuria ilikuwa wazidi asilimia 70 katika kila mkutano. Kwa hivyo, imeonyesha ya kwamba Maseneta ambao wako katika kamati hii pamoja na wafanyikazi wa Bunge ambao wanatumikia Kamati hii wamejitolea asilimia mia kwa mia katika kuihudumia. Mbali na kupongeza Mwenyekiti na Maseneta wote ambao wako katika Kamati, pia nawapongeza wafanyikazi wa Bunge ambao wako seconded katika Kamati ile. Kamati imeweza kufanya mahojiano ...
view
26 May 2020 in Senate:
tukaweza kubadilisha mfumo wa kuweza kupambana na ugonjwa wa UKIMWI. Ilikuwa ukiingia katika vituo vile unashauriwa ya kwamba ukiugua ugonjwa huo si mwisho wa maisha utaweza kuishi, kuendelea na maisha kama kawaida bora uweze kunywa dawa, kuomba na kuishi maisha ya positivethinking.
view
26 May 2020 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, lazima Wizara ya Afya iwe na mfumo wa kuondoa unyanyapaa ili wananchi waweze kupewa ushauri nasaha ili ukiingia pale kufanyiwa uchunguzi wa virusi vya korona una uhakika kwamba si hukumu ya kifo. Katika sehemu nyingi kama vile mji wa kale, wananchi wengi walikataa kufanyiwa uchunguzi wa korona wakati ule mass testing ilipoletwa wengi hawajajua jambo gani watafanya baada ya kupatikana na virusi vya korona. Ilikuwa pia serikali imeweka malipo ya wale ambao The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard ...
view
26 May 2020 in Senate:
wanakwenda karantini na wale wanalazwa hospitali kutibiwa ugonjwa wa korona. Kwa hivyo, wengi waliogopa kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi na ndio maana ikawa uchunguzi unafeli. Swala la kufanya cessation of movement yaani kuzuia watu wasiingie na kutoka old Town na Eastleigh, sheria hii ilichukuliwa bila kufanya mashauriano na wakazi wa sehemu zile. Sehemu yoyote kama vile Sen. Sakaja alitangulia kusema ikifanywa uchunguzi sasa itapatikana kwamba asilimia mbili na nusu ama asilimia tatu ya wananchi katika eneo lile wana virusi vya korona. Kwa hivyo, ni virusi watu wanaishi navyo lakini havijaambukiza ikafika kiwango ambacho watu wanapata ugonjwa wa korona na kuweza ...
view
26 May 2020 in Senate:
wanaweza kupata huduma ambazo zinazotakikana kupigana na COVID-19, ili kuhakikisha kwamba hakuna maambukizi yanayoongezeka kutokana na utepetevu kwa upande wa Serikali.
view
26 May 2020 in Senate:
Siku hizi imekuwa ni mtindo kwamba kila Saa Tisa Serikali inatoa tarakimu za watu walioambukizwa COVID-19 na vile vile waliopona. Tarakimu hizo hazisaidii kuhakikisha kwamba maambukizi yanapungua, isipokuwa yameweza kuongezeka na inakuwa shida kwa wataalamu wetu kutoa mwongozo kamili ni vipi tutaweza kupambana na Virusi vya Korona.
view
26 May 2020 in Senate:
Tumeona katika nchi jirani, Rais Magufuli ijapokuwa watu walisema kwamba haelewi, ameona kwamba ipo haja ya maisha kuendelea Virusi vya Korona vikuwepo au visikuwepo, kwa sababu ni ugonjwa kama ugonjwa mwingine. Tuliwapoteza watu 200 kwa mafuriko katika nchi ya Kenya hivi majuzi na watu wengine 20 kwa sababu ya polisi kutekeleza curfew na kudhulumu haki za binadamu kwa kupigwa.
view
26 May 2020 in Senate:
Swala la kijana ambalo Sen. Sakaja alizungumzia ni kitu ambacho kiko wazi katika macho ya wananchi, kwamba polisi walitumia silaha kinyume na sheria kwa sababu walipiga risasi wakati ambao haukuwa salama. Wananchi wanaendelea kupata shida katika sehemu nyingi. Kwa mfano, tumeona ripoti leo kwamba katika sehemu za Old Town na Eastleigh watu wanawalipa askari polisi ili waweze kuingia na kutoka kwa sababu ya maswala ya Virusi vya Korona. Mhe. Bi. Spika wa Muda, vile vile, tumeona kwamba biashara katika zile kaunti ambazo hazikuwekwa cessation of movement imepungua pakubwa. Nimesafiri leo asubuhi kutoka Mombasa kuja Nairobi. Nimeona kwamba sehemu za Ukambani, ...
view