26 May 2020 in Senate:
ambao walikuwa katika ile ndege iliyoshambuliwa na jeshi la Ethiopia walikaa Mogadishu kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu bila kazi. Hiyo ndiyo ilisababisha kutoweza kurudi nyumbani kujiunga na familia zao. Kazi ile ilipotokea, ilikuwa mara yao ya kwanza mwezi ule na wakashambuliwa na kufariki. Tumeona kwamba swala la Wakenya kurejea nyumbani wakati huu ambao kuna shida limetatiza Serikali. Ijapokuwa Serikali inategemea zile foreign remittance s ili kuinua hali yake ya fedha za kigeni, sasa imewatupa mkono watu wengi ambao wako nje kwa sababu hawakuweza kuwarejesha nyumbani kujiunga na familia zao. Ripoti yetu ya Sita ambayo imetolewa imechangiwa pakubwa na ...
view
26 May 2020 in Senate:
. Pia, kuna madaktari wengi ambao wamefunga zahanati zao kwa sasa kwa sababu hakuna wagonjwa wanaoenda pale. Ipo haja ya hazina kuwekwa ili wananchi waweze kupewa mikopo au ruzuku kulingana na kodi ambayo mtu anapeleka kwa Shirika La Ukusanyaji Ushuru (KRA) kila mwaka. Mhe. Bi. Spika wa Muda, bila kuongea zaidi ya hapo, ninaunga mkono Ripoti hii na kuomba Maseneta wajitokeze kwa wingi siku ya Jumanne tuhakikishe kwamba tumepitisha ule Mswada wa COVID-19 Pandemic Bill, 2020, ili kuhakikisha kwamba tuna mwongozo wa muda mrefu kwa maswala kama haya. Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii.
view
22 May 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipatia fursa hii kuchangia Mswada wa Kiranja wa upande wa wengi katika Bunge la Seneti. Kabla sijatoa maoni yangu, ningependa kumsahihisha ndugu yangu, Sen. Madzayo, aliposema kwamba Sen. (Prof.) Kindiki katika siasa alinoga. Nafikiria lengo lake lilikuwa kusema kwamba ‘alilamba lolo’. Kunoga ni kufanya vizuri zaidi kuliko vile ambavyo inatarajiwa. Niko hapa kwanza kusema kwamba ndugu yetu, Sen. (Prof.) Kindiki, ni mtu mwenye tajriba kubwa. Ni mtu ambaye alifanya kazi yake kama Naibu wa Spika kwa uzoefu mwingi na vile vile kwa hekima kubwa. Maamuzi aliyofanya ni ya kuaminika na yameweza kutumika hata katika mahakama za ...
view
22 May 2020 in Senate:
hivyo, itakuwa ni ile mambo kiingereza tunaita “musical chairs.” Leo inapigwa kwa huyu na kesho inapigwa kwa yule na hakuna njia ambayo tunaweza kujitetea. Sisi Waswahili tunasema muungwana akivuliwa nguo huinama. Nitamalizia hapo na ninaunga mkono Hoja hii.
view
5 May 2020 in Senate:
Asante sana Mhe. Spika. Kwanza, ningependa kuwapongeza
view
5 May 2020 in Senate:
kutoka Kaunti ya Narok kwa kuweza kuleta Petition yao katika Bunge la Seneti. Tulikuwa na Petition kama hiyo kutoka Kaunti ya Nyamira ambayo nafikiri The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
5 May 2020 in Senate:
inazingatiwa na Kamati ya Sheria na Haki za Binadamu za Bunge. Wakati fulani, wale ambao walikuwa wameleta hiyo petition, walikuwa wameamua kwamba waiondoe hiyo
view
5 May 2020 in Senate:
kwa sababu walikuwa wameona kwamba malalamishi yao yamewezwa kutekelezwa. Mhe. Spika, matatizo yako katika mabunge ya kaunti na vile vile yako katika ofisi ya Auditor kwa sababu ile miradi yetu gushi ambayo imefanyika ama imedaiwa kufanyika, haingii katika ripoti ya Auditor. Kwa hivyo, ikiwa haikuandikwa katika ripoti ya Auditor, hakutakuwa na swali ambalo litaulizwa na Auditor kwa mfano: Kwa nini barabara hii ilikuwa inatakikana itengenezwe na haikutengenezwa? Mhe. Spika, ofisi ya Contoller of Budget pia inahusika katika mambo kama haya kwa sababu wao ndio wanajuwa pesa ngapi zimetolewa na ni kwa miradi gani. Kwa hivyo, mwisho wa mwaka, ile miradi ...
view
5 May 2020 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ya Seneta wa Nairobi, Sen. Sakaja. Swala la watu kufurushwa katika makaazi yao limekuwa ni jambo la kawaida katika nchi hii. Kule Mombasa, imekuwa kila wiki unapata ripoti za watu kufurushwa, hasa maeneo ya Bamburi. Imekuwa ni kama mchezo wa paka na panya. Hii ni kwa sababu hata ukimwonyesha mhusika Officer Commanding Police Station (OCS) kwamba hakuna amri ya korti yoyote inayotekelezwa hivi sasa, anakwenda mpaka siku za Jumapili ambapo watu wameenda kanisani na kufurusha wanachi ambao wako nyumbani. Bw. Spika, kisa cha Nakuru cha juzi kilikuwa ni cha kusikitiza, ...
view