5 May 2020 in Senate:
Bw. Spika, Jumapili ni siku ya kanisa. Kama watu waenda kanisani ama hawaendi, ni suala jingine. Jumapili twajuwa ni siku ya kanisa kama vile Ijumaa ni siku ya ibada ya Waislamu. Kwa hivyo, kama watu wanaenda au hawaendi, hiyo ni siku ya amani, watu wanapumzika na hakuna kazi inayofanyika. Swala la Nakuru; mwenye biashara Mombasa Maize Millers halali. Yadi yake ilivamiwa usiku wakati kuna curfew. Sisi tunajuwa ya kwamba mwananchi akipatikana barabarani wakati wa curfew, huwa ni hatia kubwa. Unapelekwa quarantine na baada kumaliza quarantine, unalipishwa. Kuna wengine walipigwa wakauliwa wakati wa
view
5 May 2020 in Senate:
. Lakini, genge la majambazi walivamia yadi ya Mombasa Maize Millers usiku wakavunja magari, wakaiba mali, wote wakisimamiwa na polisi katika Kaunti ya Nakuru. Bw. Spika, hii inamaanisha kwamba tuna Serikali ya kihuni. Hatuna Serikali ambayo inaheshimu sheria na utengamano. Waziri wa Afya anasema kwamba tuondoe kutanagamana kwa sababu ya COVID-19, lakini wale wanaofurushwa Kariobangi, wanasongamana. Polisi wanaokuja kufurusha watu hatujui kama wana COVID-19 ama hawana. Wao wanatangamana na watu katika maeneo ambayo hakuna njia yeyote ambayo tunaweza kuwatengenisha. Bw. Spika, nchi yetu imekuwa sasa ni mtu mwenye nguvu afanye vile anavyotaka kwa sababu unaeza kutoa watu usiku wa manane ...
view
5 May 2020 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir, for giving me this to support the Statement by the Senator of Makueni County, Sen. Mutula Kilonzo Jnr. Court services have ground to a halt as a result of the delay in the appointment of these judges. The Court of Appeal had branches in Mombasa, Nakuru and Kisumu counties. All of them have been disbanded and the court brought to Nairobi. It means that court services are no longer devolved. We have to spend a lot of money to come to Nairobi to access services of the Judiciary.
view
5 May 2020 in Senate:
I beg that this Statement be dealt with as soon as possible because legal services are grinding to a halt in this country. Thank you, Mr. Speaker, Sir.
view
17 Mar 2020 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kuairishwa kwa Seneti kama ilivyokarabatiwa na Seneta Ochilo-Ayacko. Kwanza, ningependa kuipongeza Serikali kwa kuwa wazi kwamba janga la Corona limefika katika nchi yetu ya Kenya, na kwamba, tayari tunawaathiriwa wanne ambao wameweza kutambuliwa na kuwekwa katika quarantine. Pili, kule Kaunti ya Mombasa siku ya Jumamosi, tulikuwa na mkutano uliosimamiwa na Gavana wa Kaunti ya Mombasa na vilevile Kaunti Kamishna wa Mombasa ili kuweka mikakati ya kupambana na janga hili la Corona. Jambo la kufurahisha ni kuwa, tayari Kaunti ya Mombasa tumejitayarisha na tuna vyumba maalumu ambavyo vimetengwa katika ...
view
17 Mar 2020 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, ijapokuwa kuna janga la Covid-19, tusifunge macho kwa masuala mengine. Kwa mfano, juzi kwenye barabara ya Mombasa kuelekea Malindi, watu 16 walipoteza maisha yao kutokana na ajali barabarani. Tunaomba the National Transport and Safety Authority (NTSA) iangalie swala hilo. Hatuwezi kuwa tunajitahidi tusipoteze maisha kwa sababu ya Covid-19, ilhali watu wengine wanapoteza maisha katika barabara. Asante.
view
12 Mar 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika. Ningependa kuongezea taarifa ambayo imeombwa na Sen. Loitiptip. Mpango huu wa scholarship upo kwa shirika la Kenya Maritime Authority (KMA), Mombasa. Kwa hivyo, ningependa wakati Kamati itaenda Lamu kuchunguza, ipitie Mombasa waulize ni wangapi ambao wamepewa scholarship kutoka kaunti za Pwani. Madhumuni ya mradi wa LAPPSET ni kuinua hali ya maisha ya wakaazi wa kaunti hizi sita. Kwa hivyo, KMA itueleze ni wangapi kutoka Mombasa au kaunti jirani wamefaidika na mradi wa ufadhili wa masomo. Tumeona kwamba wengi wanaopata ufadhili wanatoka sehemu zingine na kupuuza matakwa ya wenyeji.
view
11 Mar 2020 in Senate:
Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa ambayo imeletwa Bungeni na Sen. Charargei. Ni jambo la kusikitisha kwamba NEMA imeamua kufunga Kiwanda cha Kusaga Miwa cha Kibos wakati ambapo wakulima wengi wanategemea kiwanda hicho kuuza miwa yao na kupata riziki ya kuwasomesha watoto wao ambao wako shuleni na vyuoni vikuu. Na pia kukimu mahitaji ya maisha. Ni lazima NEMA ifanye kazi katika hali tunayoita public interest au faida za jamii. Wajibu wao mkubwa ni kwa kusaidia umma kusonga mbele. Kwa hivyo, wanapofunga kiwanda wakati ambapo hakuna kiwanda kingine karibu na hapo ambapo wananchi wanaweza kupeleka miwa yao, ina ...
view
10 Mar 2020 in Senate:
Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kutoa rambirambi zangu kwa familia, jamaa na ndugu wa marehemu Mhe. Dori ambaye hadi kufa kwake alikuwa Mbunge wa Msambweni na pia Mwenyekiti wa Muungano wa Wabunge wa Pwani, yaani, Coast Parliamentary Group .
view
10 Mar 2020 in Senate:
Ningependa kunukuu kitabu kitakatifu cha Quran kinachosema kwamba “Kila nafsi itaonja mauti”. Kifo cha ndugu yetu Mhe. Dori kilikuwa cha ghafla na twaomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.
view