Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 141 to 150 of 2123.

  • 29 Oct 2024 in Senate: Mr. Speaker, Sir, we wanted to hear Sen. Osotsi’s evidence so that we know whether he has substantiated his claims. However, the onus is on you to rule. We needed to listen to what Sen. Osotsi had to say about those allegations. Thank you. view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Asante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii, pia niongeze kauli yangu kuunga mkono Ripoti ya uwiano kuhusiana na sheria ya ugawaji wa pesa. Mhe. Naibu Spika, hii ni mara ya pili tumeleta Ripoti ya uwiano kuhusu maswala ya sheria ya ugawaji wa pesa kati ya Serikali Kuu na Serikali za County. Hapo awali, tulileta uwiano ambapo tulikubaliana kwamba pesa ambazo zinastahili kwenda kwa county ni Shilingi 400.1 bilioni. Ripoti pia imesema kuwa tumekubaliana kwamba Shilingi 387 bilioni, ziende katika kaunti zetu. Hii ilitoka kwa sababu Mswada wa Fedha mwaka wa--- view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Bwana Naibu Spika, kuna maswala ya Lamu hapa na sijui kama yanahusiana na view
  • 27 Oct 2024 in Senate: ama--- view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Asante, Mhe. Naibu Spika. Lamu ilikuwa inachemka hapa. Kwa hivyo, pesa zimepunguzwa tena mpaka Shilingi 387 bilioni, kwa sababu ya kuondolewa kwa mswada wa fedha wa mwaka 2024 kutokana na maandamano ya Gen Z na mambo mengine. Mhe. Naibu Spika, la msingi ni kuwa, ni lazima kaunti zetu zijue kwamba fedha kutoka kwa serikali zinapungua. Ijapokua fedha zinaongezeka kwa kiwango, kwa mfano, mwaka huu tumeongeza Shilingi 2 bilioni, lakini tukiangalia katika maswala ya asilimia, zile pesa ambazo zilitoka katika Serikali Kuu kuja kwa kaunti mwaka 2013 mpaka sasa zinateremka chini. Hii ya sasa ni asilimia 13 ama 15 ya zile ... view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Kwa hivo, Mhe. Naibu Spika, ipo haja ya kaunti zetu kujaribu kuingia mifukoni wakusanye pesa ambazo wanatarajiwa kukusanya. Kama ni maswala ya kuleta mifumo ya kiteknolojia ya kukusanya pesa ifanyike hivyo ili pesa zinazokusanywa kutoka kwa kaunti ziwe zinajulikana na vile vile zitumike kwa matumizi ambayo yatasaidia maendeleo katika kaunti zetu. Haiwezekani mpaka sasa county zingine zinakusanya pesa kwa mkono. Mtu anatoka asubuhi na vitabu kumi akiregesha labda ni vitabu viwili na pesa ambazo amekusanya hazijulikani na wala hazifanyiwi hesabu na haziingii katika hesabu ya view
  • 27 Oct 2024 in Senate: mwisho wa mwaka. Lazima county zetu zijitahidi ili ziweze kukusanya pesa za view
  • 27 Oct 2024 in Senate: Kwa mfano, Nairobi City County, yatarajiwa kukusanya zaidi ya Shilingi 60 bilioni, lakini mpaka sasa wako katika Shilingi 12 bilioni au 13 bilioni. Mombasa County wana uwezo wa kukusanya Shilingi 10 bilioni, lakini sasa tuko kwa bilioni tano, nusu ya uwezo wake. Kwa hivyo, ipo haja ya kaunti zetu, si kila mwaka wapige kelele kuwa pesa zinazokuja kutoka Serikali Kuu ni kidogo. Wanafanya nini kukusanya hizi fedha? Hizi fedha zikifika kwao zinaleta maendeleo? Hospitali hazina madaktari wa kutosha na vile vile wafanyakazi katika masoko hawako. Kwa hivo, ni lazima county zetu pia zijitahidi. Isiwe kwamba lawama inaenda kwa Serikali Kuu ... view
  • 24 Oct 2024 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa na Seneta Hamida. Maswala ya afya yanazidi kudorora katika kaunti zetu. Sio Mama Lucy Kibaki Hospital peke ambapo huduma zimelemaa na kuwa na ukosefu wa fedha. Tunapozungumza sasa hivi, hospitali ya Mrima, Likoni, Kaunti ya Mombasa, kina mama waliojifungua wamezuiliwa katika hospitali hiyo kwa sababu hawajalipa gharama za kujifungua. Mradi wa Linda Mama ulikua unasaidia kina mama kujifungua katika hospitali zetu na mbali na kutolipishwa, walikua wakitoka hospitali na zawadi ndogo ndogo za kusaidia maisha yao. Kwa hivyo, kuna umuhimu wa hili swala la afya kuangaliwa kwa undani zaidi. Kila ... view
  • 23 Oct 2024 in Senate: On a point of information, Mr. Temporary Speaker, Sir. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus